Pages

Translate

Friday 31 January 2014

WASHINDI WA MIMI NI BINGWA WAREJEA

Washindi wa Airtel ‘Mimi ni Bingwa’ warejea kutoka Old Trafford

Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando (katikati) akifurahia jambo pamoja na washindi wa tiketi wa promosheni ya Airtel Mimi ni Bingwa mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam baada ya safari yao iliyogharamiwa kila kitu ya kwenda Old Trafford kuangalia mechi moja kwa moja kati ya Manchester United na Cardiff City iliyochezwa Jumanne usiku.
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando (kushoto) akiwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam na washindi wa tiketi wa promosheni ya Airtel ya Mimi ni Bingwa walioondoka nchini Jumapili wiki hii kwa safari iliyogharamiwa kila kitu ya kwenda Old Trafford kuangalia mechi moja kwa moja kati ya Manchester United na Cardiff City iliyochezwa Jumanne usiku.
Baadhi ya washindi wa tiketi kupitia promosheni ya Mimi ni Bingwa inayoendeshwa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel wakishuhudia mechi kati ya Manchester United na Cardiff City iliyochezwa hivi karibuni kwenye uwanja wa Old Trafford nchini Uingereza.Wa kwanza kulia ni Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando ambaye aliambatana na washindi hao.
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando (kushoto) akiwa pamoja na mmoja kati ya washindi wa promosheni ya Mimi ni Bingwa Bw na Bibi Dickson Lyatuu muda mfupi baada ya kushuhudia mechi kati ya Manchester United na Cardiff City nchini Uingereza hivi karibuni.
Mchezaji wa zamani wa klabu ya Manchester united Denis Irwin ( wapili kushoto) akiwa katika picha na Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando (anayefatia) pamoja na mmoja kati ya washindi wa promosheni ya Mimi ni Bingwa kabla ya kuangalia mechi kati ya Manchester United na Cardiff City iliyochezwa hivi karibuni kwenye uwanja wa Old Trafford nchini Uingereza. NA MICHUZI BLOG

WASHINDI wa awamu ya kwanza ya promosheni ya Airtel Mimi ni Bingwa jana waliwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere wakitokea Old Trafford ambapo walikwenda kushuhudia mechi ya moja kwa moja ‘live’ kati ya klabu ya Manchester United na Cardiff City.

Watanzania hao wamekuwa sehemu ya washabiki wa soka waliokuwa na furaha kushuhudia klabu ya Manchester United ikishinda 2-0 dhidi ya Cardiff City, wakati mchezaji Juan Mata akiichezea timu hiyo kwa mara ya kwanza katika uwanja wa Old Trafford, hawakuweza kuficha furaha yao ya kuwa moja ya tukio hilo la kihistoria.   

Akizungumza mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege, moja kati ya washindi wa tiketi ya Airtel Mimi ni Bingwa, Bw. Leonard Dickson Lyatuu kutoka Arusha, ambaye alisafiri na mke wake, alisema safari hiyo imekuwa ya manufaa sana katika maisha yao na kampuni hiyo ya simu imeweza kutekeleza yale yote waliyowaahidi washindi wa tiketi katika promosheni ya Airtel Mimi ni Bingwa. 

“Ninafuraha ya kipekee kuweza kurejea nyumbani salama baada ya safari yenye mafanikio makubwa ya kwenda Old Trafford. Suala nililojifunza nikiwa Manchester ni kwamba bado Tanzania inahitaji kufanyakazi kubwa ili kuziwezesha timu zetu kuendelea katika ulimwengu wa soka. Nawashukuru Airtel kwa kunipa mimi na mke wangu nafasi ya kuwa sehemu ya historia hii na kuweza kuyatekeleza yote waliyotuahidi,” alisema.

Meneja Uhusiano wa Aitel Tanzania, Bw. Jackson Mmbando alisema wakati wa ziara ya kutembelea Old Trafford, timu ya washindi kutoka Tanzania ilionyeshwa ni jinsi gani Manchester United inawajali wachezaji wake waliostaafu, suala linalosaidia kuongeza hari katika timu na kutumia uzoefu kuiboresha timu.

“Huu ni mfano ambao wadau wetu wa michezo wanahitaji kuuiga. Tunatakiwa kuwathamini wachezaji wetu wa zamani na kutumia uzoefu wao ili kuzibadilisha timu zetu kuwa bora kimchezo kitaifa na kimataifa,” alisema.

Kwa upande wake, Andrew Muta Temwa, mshindi wa tiketi kutokea Bukoba alisema fursa ya kukutana na kocha Sir Alex Ferguson ilikuwa ni kama ndoto kwake. 

“Sikutarajia kama siku moja nitakutana na Sir Alex Ferguson moja kwa moja ‘Live’. Kupitia safari hii, Airtel imeweza kuzifanya ndoto yangu kuwa kweli. Nataka kuwahakikishia washiriki wengine wa Mimi ni Bingwa waendelee kucheza ili nao wapate fursa ya kushinda pesa taslim kupitia promosheni hii ya Airtel,” alisema.

Awamu ya kwanza ilijumuisha, Bw. Leonard Dickson Lyatuu kutoka Arusha, Andrew Muta Temwa mkazi wa Bukoba, Ashraf Mohamed Adam kutoka Tanga na Salma Farid Mugheiry kutoka Dar es Salaam na wenza wao.

Airtel ilitangaza kuwa mbali na tiketi, zawadi kubwa ya shilingi milioni 50 sasa iko tayari kushindaniwa mwishoni mwa droo, ambayo kila mshiriki wa promosheni ya Airtel Mimi ni Bingwa ana nafasi ya kujishindia kwa kutuma ujumbe mfupi (SMS) wenye neno “BINGWA” kwenda namba 15656, na kujibu maswali mengi iwezekanavyo.     


Washindi wa safari ya Old Trafford toka promosheni ilipoanza mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka jana ni pamoja na  Msemwa George Makuzi kutoka Dar es salaam, Edwin Edmund Kajimbo kutoka Iringa, Michael Joseph Shirima kutoka Kinondoni jijini Dar es Salaam, Bw. Shaibu Rashid Dege, Mtendaji wa kijiji cha Nang’olo wilayani Kilwa – mkoani Lindi, Leonard Dickson Lyatuu kutoka Arusha, Joseph Steven Mambo kutoka Kawe jijini Dar es Salaam, Emmanuel Mahenge Jacob kutoka Njiro in Arusha, Rashid Jacob Kagombola kutoka Bukoba mkoani Kagera, Harrison Wilson Mwambogolo kutoka Kigogo jijini  Dar es Salaam na Salma Farid Mughery kutoka Dar es Salaam.

MTANGAZAJI LYANGA WA EARADIO AFARIKI

 

 Mbunifu Msaidizi na Mtangazaji wa Habari za Michezo wa East Africa Radio Kenneth Kidago Lyanga amefariki dunia nyumbani kwake Mwenge Mlalakua, Jijini Dar es Salaam.


TANZANIA INAKOPESHEKA

Waziri wa Fedha na Uchumi, Saada Mkuya.

DAR ES SALAAM

LICHA ya deni la taifa kuongezeka na kufikia Sh27 trilioni mwaka jana, Serikali imesema bado ina sifa za kuendelea kukopa kutokana na mapato ya ndani kuwa madogo.


Akizungumza Dar es Salaam jana, Waziri wa Fedha na Uchumi, Saada Mkuya alisema jambo linalozingatiwa na Serikali ni kuhakikisha fedha za mikopo zinatumika kwa shughuli za kukuza uchumi.


“Deni la taifa linajumuisha deni la Serikali kutoka vyanzo vyake vya mapato ya ndani na nje ya nchi pamoja na deni la nje ambalo Serikali imelidhamini kwa sekta binafsi,” alisema Mkuya.


Alisema hadi kufikia Desemba mwaka jana, deni la taifa lilifikia Sh27 trilioni, kati ya kiwango hicho deni la nje ni Sh20.2 trilioni na ndani ni Sh6.8 1 trilioni, huku deni la nje la sekta binafsi likifika Sh3.5 trilioni.


“Tunaendelea kukopa na deni linaongezeka. Linaongezeka kwa mikopo inayochukuliwa na ile ambayo haijalipwa,” alisema.


Akitaja sababu za kuongezeka kwa deni hilo alisema: “Linaongezeka kwakuwa nchi bado inaendelea kukopa, kuendelea kuwepo kwa madeni ya nyuma kutokana na muda wake wa kuyalipa kutofika, kuongezeka kwa watu na shughuli za kiuchumi pamoja na kuwepo kwa madeni ambayo kwa mujibu wa mikataba yanatakiwa kusamehewa.”


Alisema kutokana na kuwepo kwa orodha ndefu ya nchi zinazokopa, hivi sasa Tanzania imejikita zaidi katika kukopa mikopo yenye masharti ya kibiashara ambayo ni tofauti na mikopo yenye masharti nafuu.


Hata hivyo, Mkuya alisema kila mwaka Serikali inafanya tathmini kama inaweza kuhimili deni kutokana na shughuli za kiuchumi ndani ya nchi. “Tathmini ya mwisho tumefanya Septemba mwaka jana, haifanywi na Serikali pekee, inahusisha pia Shirika la Kimataifa la Fedha (IMF) na Benki ya Dunia (WB),” alisema Mkuya.


Waziri huyo alivitaja viashiria vinavyoonyesha kuwa nchi ina uwezo wa kuhimili deni kuwa ni thamani ya deni la nje ikilinganishwa na uchumi wa nchi (GDP),”


“Deni la nje sasa hivi ni asilimia 25 ambayo ni sawa na asilimia 24.8 ya uchumi wa nchi. Lakini ukomo wa kukopa kwa kutumia kiashiria hiki ni asilimia 50 ya deni, hivyo bado tuna vigezo vya kukopa maana tupo katika asilimia 24.”


Alisema thamani ya leo la deni lote la taifa kwa uchumi wa nchi ni asilimia 40.5 na kwamba ukomo wake ni asilimia 74.


“Lakini hilo halitufanyi kukopa zaidi, ila kutokana na hali ya uchumi tutakopa katika vyanzo nafuu,” alinena.MWAANANCHI

AIBA MTOTO WA MWEZI MMJO NA KUTOROKA NAE

MKAZI wa Bunju B, Grace Chapanga(34), anashikiliwa na Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa tuhuma za wizi wa mtoto mchanga wa kike mwenye umri wa mwezi mmoja. 


Kamanda wa Kanda hiyo, Kamishna wa Polisi Suleiman Kova alisema Chapanga alimuiba mtoto huyo, Veis Venus Desemba 27 mwaka jana katika maeneo ya Mwenge jijini Dar es Salaam.

Alisema mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo baada ya kumhadaa mama wa mtoto aitwae Salma Frank (29), mkazi wa Kawe Mji Mpya kwa kumuomba ambebee huku wote wakiwa abiria wa daladala, wakitokea Hospitali ya Mwananyamala.

Kova alisema walipofika kituo cha daladala Mwenge, mtuhumiwa aliteremka upesi na kutoweka na mtoto, wakati mwenye mtoto akikusanya vitu vingine alivyokuwa navyo.

“Chapanga alitenda kosa hilo kwa kushirikiana na Halima Alabi (46), mkazi wa Boko Maliasili ambaye naye alikamatwa Januari 4 mwaka huu,” alisema.

Alisema watuhumiwa wote baada ya kutenda kosa hilo, waliondoka kwenda Sumbawanga mkoani Rukwa, ambapo Chapanga alimdanganya mumewe kuwa yeye ni mjamzito na angependa kwenda kujifungulia nyumbani kwao Sumbawanga.

“Upelelezi wa tukio hilo ulifanikisha kumkamata mume wa Chapanga aitwaye Daniael Mwaikambo (38), mkazi wa Bunju B, ambaye pia ni mfanyakazi wa Uhamiaji Makao Makuu Dar es Salaam na kwenda naye Sumbawanga, ambapo walimkuta mtuhumiwa na kumkamata” alisema.

Inasemekana kwamba tangu Chapanga na Mwaikambo wafunge ndoa mwaka 2010 hadi sasa, wanandoa hao hawajabahatika kupata mtoto.

Aidha, Kova alisema mwaka 2012 Chapanga alifanyiwa upasuaji wa uvimbe tumboni na daktari alimwambia hatoweza kushika mimba tena, jambo ambalo mwanamke huyo hakumueleza ukweli mume wake wala ndugu yake yeyote hadi alipopanga njama na hatimaye kufanikiwa kumuiba mtoto huyo.

Alisema upelelezi wa shauri hilo unaendelea kwa kufuatilia uchunguzi wa vinasaba (DNA) vya mama mzazi, mtuhumiwa na mtoto aliyeibwa. Pia alisema mtoto huyo amekabidhiwa kwa mama yake mzazi. HABARILEO

MWENDOKASI NDIO HAYA HAPA




Mmoja ya basi la mwendo kasi likikatiza mtaa wa Lumumba ikiwa sehemu ya majaribio ya mabasi hayo ambayo yanaaminika yataondoa kabisa tatizo la usafiri katika jiji la Dar.

MZEE AFUMWAFUMWA GESTI NA MWANAFUNZI

 

Ile tabia ya wazee ya kupenda dogodogo imemtokea puani mzee aliyetajwa kwa jina moja la mzee Omari.Mzee huyo alinaswa laivu akiwa gesti na denti wa shule moja ya sekondari jijini Dar (jina la denti na shule vinahifadhiwa kimaadili).  Tukio hilo la aibu lilijiri juzikati kwenye gesti moja iliyopo maeneo ya Kawe, Dar na kusababisha timbwili zito.

 
Chanzo  cha  mzee  huyo  kufumaniwa  kinatokana  na  mzazi  wa   mwanafunzi   huyo  kuanza  kufuatilia  kwa  ukarubu  mwenendo  wa  binti  yake. Akiongea  na  mwandishi  wetu, Mzazi huyo alidai  kuwa  amekuwa akifuma mawasiliano ya kwenye simu ya mkononi ya mwanaye na mwanaume huyo ambaye alikuwa hamfahamu.
 
Mama huyo alisema kuwa kutokana na maendeleo ya mwanaye kuzidi kudorora shuleni, aliamua kumfuatilia kwa karibu kwa kuwa hakutaka apotee.
Mama huyo alitiririka kuwa, siku ya tukio, alimsikia mwanaye huyo akiwekeana miadi kwenye simu na mwanaume huyo ndipo akaamua kumuwekea mtego.
 
Alisema wakati mwanaye huyo akilonga kwenye simu, yeye alibana sehemu na kuyasikia yote ambayo alikuwa akiyaongea na kwamba walipanga kukutana baa.
 
“Nilichokifanya nilimpigia simu mjomba wake na kumweleza kila kitu, nikamwelekeza namna ya kumfuatilia. Alichukua bodaboda na kuanza kumfuatilia. Mimi na timu yangu tulifuata nyuma,” alisema mama huyo kwa uchungu.

Alisema mzee huyo alikubaliana na mwanaye wakutane kwenye baa hiyo ambapo ndani yake kuna nyumba ya kulala wageni

Baada ya mpango wa mtego kukamilika ndipo mama huyo akawaita wanahabari.Kabla ya kuchukua hatua yoyote, wanahabari hao walishauriana kutoa taarifa kituo cha polisi, jambo ambalo lilifanyika na kupatiwa msaada wa kiusalama.

Walipofika kwenye baa hiyo mama mtu alipigwa na butwaa kumuona mtu aliyekuwa akiwasiliana na mwanaye ni mzee sawa na babu yake.

Huku wakifuatiliwa kwa karibu, mzee huyo na denti walipiga madikodiko na vinywaji ndipo wakatimba kwenye gesti hiyo.

Kilichofanyika ni kwamba polisi na mama wa denti walizama gesti hiyo na kuomba kumsaka mwanafunzi huyo, jambo ambalo halikupingwa.

Baada ya kuzama ndani ndipo mtego ukafyatuka ambapo mzee Omari alibambwa katika moja ya vyumba vya gesti hiyo huku akiwa amejifunga taulo tu.
 Mzee huyo alipatwa na taharuki kubwa asijue la kufanya kufuatia timbwili zito alilozua mama wa denti huyo.

Mara baada ya mzee huyo kunaswa, aliomba chondechonde kukaa na familia ya mwanafunzi huyo ili kuyamaliza yasifike mbali.

Hata hivyo, baada ya maombi ya muda mrefu walikubaliana kuandikishiana ambapo mzee huyo alitakiwa kulipa faini. 
  
“Sisi hatuna maneno mengi, hatutaki kesi ila atulipe fidia ya kumsababishia mtoto wetu asiwe na mahudhurio mazuri shuleni kutokana na ulaghai wake,” alisema mzazi huyo.

Habari zilieleza kuwa mzee huyo alishindwa kulipa mara moja badala yake aliingia mitini kwa kigezo kuwa anakwenda kutafuta faini hiyo.
CREDIT :GPL

CHADEMA WAIVAMIA MOROGORO KWA MBWEMBWE, AFANDE SELE ATAMBULISHWA RASMI

 Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akimtambulisha mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya, Afande Sele, wakati wa mkutano wa Operesheni M4C Pamoja Dama, uliofanyika katika Kata ya Tungi mjini Mororgoro .
 Mwenyekiti wa Chama ch Demokrasia na Mendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akiwahutubia maelfu ya wakazi wa mji wa Mtibwa katika mkutano wa Operesheni M4C pamoja Daima.


Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya, Afande Sele akiwahutubia wananchi wa Kata ya Tungi mjini Morogoro, katika mkutano wa hadhara wa Operesheni M4C Pamoj Daima.
 Mbunge wa Kawe, Halima Mdee akiwahutubia maelfu ya wakazi wa mji wa Mtibwa, katika mkutano wa Operesheni M4C Pamoja Daima.
 Sehemu ya maelfu ya wakazi wa mji wa Ifakara, wakitawanyika baada ya mkutano wa Operesheni M4C Pamoja Daima, ambao ulihutubiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe jana.
 
 Baadhi ya wa mji wa Ifakara wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe mbalimbali, wakati wa mkutano wa Operesheni M4C Pamoja Daima, ambao ulihutubiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe jana.
 Mwenyekiti wa Chama cha Demokreasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee wakiondoka baada ya kuhutubia mkutano wa Operesheni M4C Pamoja Daima, uliofanyika mjini Ifakara.
 .Maelefu ya wakazi wa mkji wa Ifakara, wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa Operesheni M4C Pamoja Daima, ambao ulihutubiwa na Mweneyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)

ZITO AJA NA UKWELI MWINGINE

Mbunge wa Kigoma Kasikazini ZittoZuberi Kabwe leo kaanika ukweli na kuonesha uwazi wa maslahi wanayopata viongozi wetu. Ikiwa wananchi kipato chao ni kidogo sana huku watumishi wakipokea mishahara ambayo haikidhi na cha kushangaza wale waliopewa dhamana ya kuwawakilisha bungeni hawaoneshi nia ya kupigania kuongezwa mishahara ya watumishi walau ikaribie kama yao. Je tutafika na je ndio Tanzania tunayoitaka?

Katika ukurasa wake wa FACEBOOK, Mwanademokrasia huyo kaandika hivi: "Posho za kukaa (sitting allowances) kwa mwaka ni tshs 36m kila mbunge. Kwa miaka 5 ni tshs 182m! We lost the battle. Will we gratuity one?"

NOTE TAKE: kama ndio hivyo basi mwaka 2015 vijana wote watagombea ubunge maana hakuna watu wenye nia ya dhati ya kuwatetea wananchi, vijana wanamaliza vyuo hakuna ajira wala kutengenezewa mbinu ya ajira. Kumbuka mbunge ni mtumishi na ni wajibu wake kuwatumikia wananchi.

habari kamili ingia hapa:https://www.facebook.com/zkabwe

Tuesday 28 January 2014

KONGAMANO LA KILIMO LIWE NA MANUFAA KWA WAKULIMA

  
 :Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea kitabu cha Mandela toka kwa Mkurugenzi wa Programu wa Spintelligent ya Afrika Kusini Bi. Amore Swart baada ya kufungua rasmi kongamano la Kilimo Afrika Mashariki katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo Januari 28, 2014.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo toka kwa Bi Meab Mdimi wa Kampuni ya Kilimo ya TECHNOSERVE  baada ya kufungua rasmi kongamano la Kilimo Afrika Mashariki katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo Januari 28, 2014.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo katika banda la Mpango wa Kuendeleza Sekta ya Kilimo Kusini mwa Ukanda wa Afrika (SAGCOT)    baada ya kufungua rasmi kongamano la Kilimo Afrika Mashariki katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo Januari 28, 2014.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati wa kufungua rasmi kongamano la Kilimo Afrika Mashariki katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo Januari 28, 2014. 

KONGAMANO LA KILIMO LIWE NA MANUFAA KWA WAKULIMA

  
 :Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea kitabu cha Mandela toka kwa Mkurugenzi wa Programu wa Spintelligent ya Afrika Kusini Bi. Amore Swart baada ya kufungua rasmi kongamano la Kilimo Afrika Mashariki katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo Januari 28, 2014.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo toka kwa Bi Meab Mdimi wa Kampuni ya Kilimo ya TECHNOSERVE  baada ya kufungua rasmi kongamano la Kilimo Afrika Mashariki katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo Januari 28, 2014.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo katika banda la Mpango wa Kuendeleza Sekta ya Kilimo Kusini mwa Ukanda wa Afrika (SAGCOT)    baada ya kufungua rasmi kongamano la Kilimo Afrika Mashariki katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo Januari 28, 2014.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati wa kufungua rasmi kongamano la Kilimo Afrika Mashariki katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo Januari 28, 2014. 

OKOA MAISHA YA MTOTO HUYU UBARIKIWE: JIONEE MWENYEWE

LAZIMA utokwe machozi! Grace John mkazi wa Mzumbe, Mvomero mkoani Morogoro yupo kwenye wakati mgumu kutokana


na maradhi ya ajabu yanayomsumbua mwanaye Honolina Christian Mkude (11).

Honolina Christian Mkude (11) anayesumbuliwa na ugonjwa wa kuota nyama.

Honolina anasumbuliwa na ugonjwa wa kuota nyama sehemu za mwili wake zinazofanana na pembe za mnyama, ugonjwa ambao unamtesa tangu kuzaliwa kwake.MATUKIO NA VIJANA
ILIKUWAJE?
Akisimulia kisa kizima, mama mzazi wa Honolina, Bi. Grace, anasema tangu amemzaa mwanaye huyo ni mitihani baada ya mitihani.

Wasamaria wema wakimpatia misaada mama Honolina.

Mazungumzo hayo yalifanyika hivi karibuni katika kituo cha mabasi ya mikoani, Msamvu, mjini hapa wakati mama huyo na mwanaye wakihangaikia kuchangisha fedha za usafiri wa kwenda Moshi kutafuta tiba zaidi katika Hospitali ya Kilimanjaro Christian Medical Centre (KCMC).
“Ndugu mwandishi, kwa kweli sijui hatima ya mwanangu. Nilimzaa akiwa ameota nywele sehemu zote za mwili wake, hadi usoni. Mimi na mume wangu tulishangaa, lakini tuliendelea na matibabu katika hospitali mbalimbali maana baadaye alianza kupatwa na uvimbe.


Mtoto Honolina akipata kinywaji.

MTIHANI MWINGINE
“Jamani ndugu yangu... Mungu ana mitihani yake. Mume wangu (Christian Mkude) ambaye ndiye alikuwa tegemeo pekee kwetu, alifariki mwaka 2007 kwa ajali ya gari, wakati akisaka fedha za  matibabu ya mwanetu.
“Kifo chake, kwangu kimekuwa pigo mujalabu. Sina pa kukimbilia na hivi juzi tu tulikuwa tumelazwa Hospitali ya Mkoa (Morogoro) na hapo tumepewa barua ya kwenda KCMC kwa matibabu zaidi.

Mama Honolina akipokea msaada kutoka kwa msamaria.

“Hivi unavyoniona nachangisha fedha ili nipate angalau nauli za kutufikisha kwanza hospitalini.  Nimechanganyikiwa kabisa,” alisema Bi. Grace kwa majonzi na kuongeza:
“Wakati tatizo la mwanangu linaanza sikutegemea kama siku moja angekuja kuwa hivi. Zilianza kuota nywele mwili mzima, baadaye vidonda vikaanza kumtoka na sasa hali imebadilika na kuota nyama hizi kubwa kama mapembe kama unavyoona.”

Mtoto Honolina (kulia) alipoanza kuugua.

SAUTI YA BI. GRACE KUTOKA MOSHI
Misaada ya fedha kidogo alizopata kwa wasamaria wema waliomuona Msamvu, ulimsaidia mama huyo kusafiri hadi Moshi na kufika katika Hospitali ya KCMC.
Akizungumza kwa njia ya simu kutoka Moshi, Bi. Grace alisema: “Nawashukuru waliniosaidia, tumefika salama na mwanangu hapa KCMC, ndiyo tumeanza taratibu za matibabu.”
BADO ANAHITAJI MSAADA
“Madaktari wametupa moyo, wamesema watajaribu kumsaidia mwanangu. Watamtoa hizo nyama ila kwa sababu kutabaki na mashimo lazima wapandikize nyama nyingine.
“Tumeshakubaliana kuwa mimi ndiye nitakayekatwa sehemu ya nyama kutoka kwenye makalio yangu kwa ajili ya kumsaidia mwanangu,” alisema Bi. Grace, kilio kikisikika kwenye simu.

Wananchi wakimtazama Honolina kwa huruma.

Akaongeza: “Wameshachukua nyama za mwanangu na kwenda kupima na baadaye watachukua zangu ili kuona kama zinaendana, upasuaji ufanyike. Gharama kwa ajili ya matibabu hayo wamesema ni shilingi 400,000 na mimi sina uwezo.
“Watanzania wenzangu, naombeni mnisaidie ili niweze kuondokana na hili tatizo. Mimi ni mjane na sina kazi ya kueleweka, napigania uhai wa mwanangu. Naombeni msaada wenu,” alisema.
SHIRIKI BARAKA
Kumsaidia mhitaji wa kweli huongeza baraka katika kipato, vitabu vitakatifu vinaeleza wazi. Ndugu wasomaji wetu wapenzi, kwa yeyote atakayeguswa na mateso ya familia hii, anaweza kumsaidia chochote mama huyo kupitia simu zake namba 0719 749542(Tigopesa) na 0762 425973 (M - pesa).

MZEE WA UPAKO AUKANA UFREEMASON

ULE uvumi kwamba baadhi ya wachungaji na maaskofu wa makanisa ya kiroho  nchini wanajihusisha na imani ya Freemason unazidi kushika kasi huku awamu hii ‘rungu’ likimwangukia Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC) la Ubungo jijini Dar, Lusekelo Mzee wa Upako’ na kutikisika, 

 MINONG’ONO ILIVYOANZA
Madai ya mtumishi huyo kujihusisha na imani ya Freemason yalianza kuenea kwa kasi mithili ya moto nyikani huku baadhi ya watu, wakiwemo watumishi wa makanisa ya Kikristo, wakionesha shaka juu ya uponyaji wa mtumishi huyo kufuatia miujiza ya ajabu ambayo amekuwa akiionesha kwa watu wenye uhitaji wa kiimani.
 
MATENDO YA SHAKA
Baadhi ya matendo ambayo yamekuwa yakiwatia shaka baadhi ya watu ni pamoja na kitendo cha mchungaji huyo kuwaombea watu wakiwa hawana kitu kabisa lakini baada ya miezi michache hurudi kanisani hapo wakiwa na magari ya kifahari na wakionesha kila dalili ya ukwasi (utajiri).
“Eti unakuta mtu amekwenda kuombewa akiwa hana kitu kabisa (fukara) lakini bada ya miezi michache anarudi akiwa na gari la kifahari, kweli?
 “Tena anaonesha kila dalili ya ukwasi, huenda ni kweli kuna nguvu za ziada zaidi ya ile ya kiroho,” walisema baadhi ya waumini wa makanisa mbalimbali ya Kikristo walipozungumza na gazeti hili hivi karibuni.  

ALAMA NA VIASHIRIA  TATA
Wakifafanua kwa kina zaidi juu ya wasiwasi wao kwa Mzee wa Upako na miujiza yake, waumini hao walitolea mfano wa baadhi ya dalili na viashiria tata vinavyoshukiwa kuwa ni moja ya utambulisho wa Taasisi ya Freemason.
 Wakitaja baadhi ya alama hizo, waumini hao walisema mara nyingi mtumishi huyo akiwa madhabahuni amekuwa akitumia kitambaa kikubwa.
“Kila akiwa  jukwaani au madhabahuni hutumia kitambaa kikubwa kujifutia na kuwagusia anaowaombea hali ambayo huwafanya kuanguka na kupiga kelele hovyo,” walisema.
 Mbali na kitambaa, pia walisema Mzee wa Upako amekuwa akionekana na pete zenye picha za ajabu akiwa anahubiri au kutenda miujiza. 

MADAI ZAIDI
Baadhi ya waumini hao walisema viashiria vingine ni kitendo cha mchungaji huyo kutotaja neno Mbinguni katika mahubiri yake zaidi ya kusema, ‘Mungu wangu awabariki sana’.
 “Mapete yake yana  mapicha ya ajabu sana, yale maalama ya Freemason yapo, pia huwa hawezi kusema Mungu wa Mbinguni, badala yake husema ‘Mungu wangu awatangulie’ au ‘kwa uwezo wa Mungu ninaye mwabudujambo ambalo hututia shaka sana,” walisema Wakristo hao.  

WAUMINI WAMBANA
Katika kufuatilia kwa kina sakata hilo, habari zikadai kuwa baada ya mambo kupamba moto waumini wa kanisa lake walianza kumbana mtumishi wao huyo kuhusu uvumi huo huku baadhi yao wakianza kutimkia kwingine.
 “Ni kweli zahama hiyo iliwahi kutokea, lakini mambo yalikaa sawa baada ya Lusekelo kutufafanulia zaidi juu ya madai hayo,” alisema mmoja wa waumini wa kanisa hilo kwa sharti la kutotajwa jina lake gazetini.  

LUSEKELO KIZIMBANI
Baada ya  kupata taarifa hizo nzito, hivi karibuni  waliamua ‘kukanyaga  lami’ hadi kanisani kwa mchungaji huyo, Ubungo -Kibangu  ambapo licha ya kukumbana na vikwazo mbalimbali walibahatika kukutana naye na kumbana kwa maswali juu ya tuhuma hizo ambapo kwa ‘jasho jembamba’ aliweza kueleza kwa kina:
 “Hizo tuhuma zilianza kusikika zamani sana, watu walianza kunituhumu kwenye matumizi ya bendera ya taifa kanisani, nikatoa, wakahamia kwenye kitambaa.
“Jamani natumia muda mwingi sana kusimama madhabahuni. Sasa nikitumia kitambaa (hendkachifu) cha shilingi mia tano itawezekana kweli, natumia kitaulo kidogo kujifutia jasho, sasa inaonekana nongwa.
 “Baadaye wakahamia kwenye pete! Mimi ni mtu smart sana (msafi) nimezaliwa mjini (born town) sasa kuvaa pete ni sehemu ya maisha ya mjini sioni tabu, lakini baada ya manenomaneno nilivua na sasa sina,” alisema Mzee wa Upako. 

 KUHUSU WAUMINI KUTIMKA
“Ni kweli, baadhi waliniuliza nikawajibu, wengine wakaamua kutimka. Unajua mimi nimeanza kumtumikia Mungu kwa miaka thelathini sasa, muumini kuhama kanisa na kwenda kwingine sishangai.
“Lakini wajue kwamba hapa kwangu ni moto mkubwa, super charge, cartapillar, siteteleki, nitazidi kuwaombea na kuwaponya wenye taabu na magonjwa,” aliongeza.
  

KUHUSU FREEMASON?
“Sijawahi kufikiria hata siku moja kuwa Freemason, kwanza sifahamu hata wanavyopatikana, nimeanza kumtumikia Mungu nikiwa kijana mdogo, mimi si muumini wa dini wala imani yoyote ya kishetani.
 “Shetani mwenyewe ananiogopa, sasa hao wanaosema kuwa huwa sisemi Mungu wa Mbinguni, nashangaa, ni lazima kuweka neno Mbinguni? Jamani hao Freemason siwajui, wala siwazuii watu kuniita hivyo, naendelea kulihuburi Neno la Mungu aliye hai,” alisema Lusekelo na kufunga ‘faili’ la mazungumzo na waandishi wetu.

MARLBORO AFARIKI DUNIA

Mtu pekee aliyeweza kuibadilisha na kuinua mafanikio ya sigara duniani haswa sigara maarufu ya Marlboro, Eric Lawson (Pichani kulia) amefariki dunia.

Mwanaume aliyekuwa na mvuto, mcheza filamu ambaye alikuwa mpanda farasi maarufu Southwest, aliyetoka Texas mpaka Colorado na kwenda Arizona nchini Marekani, ambaye pia aliweza kuinua kampuni ya Phillip Morris Tobacco na kulinda utamaduni wa kweli wa Kimarekani wa Cowboy, na kweli aliweza kuvuta sigara za Marlboro mpaka paketi 3 kwa siku.

Lawson alikuwa bado anavuta sigara mwaka 2006 alipogundulika kuwa na ugonjwa usiotibika wa mapafu. Alifariki dunia kutokana na ugonjwa huo akiwa nyumbani kwake San Luis Obispo tarehe 10 mwezi januari akiwa na miaka 72.

Kwa miaka 3, mwishoni mwa miaka ya 70 na mwanzoni wa miaka ya 80, Lawson alipata umaarufu mkubwa katika matangazo na kuwakilisha utamaduni wa kimarekani.

Katika miaka kadhaa iliyopita Lawson aliongelea sana na kwa ukali madhara ya uvutaji sigara, alifanya huduma za kujitolea na kutoa matangazo kadhaa kwaajili ya taasisi ya saratani ya Marekani ya American Cancer Society miaka ya 90, ikiwa ni miaka michache kabla hajaacha kuvuta sigara.

“Alijitahidi kuongea na watoto, kuwaambia wasianze kuvuta sigara”, alisema mkewe Susan Lawson akiliambia shirika la AP akiongeza “alijua sigara

BIFU LA ZITTO LINAENDELEA, SAFARI HII KASFA YA MAPENZI



 

KUNDI la watu ambao inadaiwa kwamba wamekula yamini ya kumchafua Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe kwa namna yoyote ile, wamemuonjesha machungu Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Catherine Magige. Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Catherine Magige.

  Zitto, baada ya msululu wa tuhuma ambazo nyingi zilibainika kupikwa makusudi ili kuichafua taswira yake mbele ya jamii, sasa hivi anahusishwa kutoka kimapenzi na Magige, ikidaiwa kuwa walisafiri pamoja kwenda Dubai kwa ajili ya kufanya mambo yasiyofaa. 


Hata hivyo, uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa tuhuma hiyo ya Zitto na Magige ni nyingine kati ya zile zilizopikwa, kwani ukweli wake ni wa kufikirika. 

Imebainika kuwa safari ya Dubai ambayo inasemwa kuwa Zitto na Magige walisafiri, inapotoshwa kwa sababu ukweli ni kwamba wabunge hao walisafiri pamoja na timu nzima ya Kamati ya Hesabu za Serikali Bungeni (PAC) kwa shughuli za kikazi na hakukuwa na suala la mapenzi kati yao. 

Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe. Mbunge wa Ludewa (CCM), Deo Filikunjombe, aliye makamu mwenyekiti wa PAC, akiizungumzia skendo hiyo ya Zitto na Magige alisema: “Nimeona ujumbe ambao unasambazwa kuhusu Zitto na Catherine (Magige), ni uongo mkubwa, hakuna kitu kama hicho. “Nimeona wanazungumzia zaidi tiketi, ni kweli tulisafiri kamati nzima kwenda Dubai. Wajumbe wote wa PAC tulikwenda Dubai baadaye Uingereza. 

Zitto ndiye hakwenda Uingereza, yeye aliishia Dubai na kurudi nchini. “Katika hili namsikitikia zaidi Magige kwa sababu anaingizwa kwenye vita ambayo haijui, siyo mzoefu wa kashfa hizi za kuzushiwa, Zitto angalau naweza kusema amezoea. 

Nitasimama kokote kumtetea Catherine na hata Zitto. Hili limeandaliwa makusudi kumchafua Zitto na hii ni vita ndani ya Chadema wao kwa wao.” Mjumbe wa PAC, Esther Matiko, ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) Mkoa wa Mara, alisema: 
 
“Hilo suala ni la uongo kabisa, walioanzisha hiyo tuhuma pengine wanataka kumchafua Catherine. Tulifikia hoteli moja na chumba changu na kile cha Catherine, vilikuwa karibukaribu, hakuna kitu kama hicho kinachosemwa. 

“ Catherine alisafiri na mwanaye wa kike anayesoma kidato cha kwanza, na alikuwa akilala naye chumba kimoja, sasa hayo mambo yangewezekanaje? Hizi ni siasa tu. 

Kwanza Catherine hii siyo safari yake ya kwanza, kila tunaposafiri kwenda nje, huwa analala chumba kimoja na dada Lucy (Owenya, Mbunge wa Viti Maalum Chadema). “Kitendo cha kupendelea kulala chumba kimoja na dada Lucy maana yake hapendi hayo mambo, tena ni kuonesha anaogopa manenomaneno kama haya. 

Safari zote huwa analala na dada Lucy, kasoro hiyo tu ndiyo alilala na mwanaye wa kike. Zaidi ya hayo, namsemea Zitto, yeye ni mwenyekiti wetu, amekuwa akitaka tuwe na maadili ndiyo maana hajawahi kuwa na uhusiano na mjumbe yeyote.” Zitto hakupatikana kuzungumzia tuhuma hiyo lakini Catherine alipopatikana alisema kuwa hana maneno kwa sababu anajua kinachosemwa ni uongo, akaongeza
“Wanatishia wana video, waiweke wazi kama ni kweli. Hizi siasa za kuchafuana kwa vitu vya uongo hazifai hata kidogo, haziisaidii nchi.” 

Monday 27 January 2014

AFUMWA NA MCHUMBA AKIJIUZA

OPARESHENI Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers si mchezo! Safari hii imenasa tukio la mchumba wa mtu aliyetajwa kwa jina moja la Jose kuuza mwili.
Za mwizi 40: Mchumba wa mtu baada ya kunaswa na OFM akijiuza licha ya kuaga kuwa anakwenda kwa bibi yake.
Tukio hilo lilijiri eneo maarufu la Baa ya Kaumba iliyopo katikati ya mji kwenye Mtaa wa Makongoro, mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo OFM na polisi walikuwa kwenye oparesheni za kufichua uovu wa biashara haramu ya ngono.

OFM NOMA: Mchumba wa mtu na wenzake wakiwa mikononi mwa OFM na Polisi.
Kwa mujibu wa mchumba huyo katika mahojiano na OFM, aliaga kwao Kilosa kuwa anakwenda Morogoro mjini kumuuguza bibi yake ambaye ni mgonjwa.
Tofauti na matarajio ya familia yake, mrembo huyo alikwenda kukita kambi maeneo hayo akijihusisha na biashara hiyo haramu eti kwa madai ya kusaka fedha ya kununulia sare za harusi yake ambayo inatarajiwa kufanyika Februari 15, mwaka huu.

Mshangao: Mchumba wa mtu akishangaa baada ya kubambwa na OFM.
Jumatano iliyopita, OFM ilipokea simu kutoka kwa dada mmoja ambaye alieleza kuwa kuna ‘shori’ ambaye ni mchumba wa mtu anajiuza katika viunga vya Kaumba.
Dada huyo aliendelea kueleza kuwa yeye ni mmoja wa wajumbe katika kikao cha harusi ya dada huyo huku akiwa ameshachangia shilingi elfu 50 lakini alishangaa kumuona maeneo hayo hatarishi.

Twendeni: Mchumba wa mtu akiongoza wenzake wanaoshuka kutoka kwenye difenda kuelekea kituoni.
“Niamini mimi, tunakaa naye Mji Mpya (Morogoro). Hata fedha za advance ya ukumbi, vinywaji, MC na muziki tumeshalipa na harusi yake inatarajiwa kufanyika Februari 15, mwaka huu.
Baada ya kunyetishiwa habari hizo, kikosi kazi cha OFM kiliingia mzigoni kwa kushirikiana na dada huyo ambaye alivalishwa ‘beji’ yao na kufanikisha kunaswa kwa mchumba huyo.


Chini ya ulinzi: Mchumba wa mtu na wenzake wakiwa chini ya ulinzi kituoni.
OFM ikishirikiana na polisi wanaojua kujituma kwenye majukumu yao walimtia mbaroni dada huyo akiwa katika pilikapilika zake za kunasa wanaume huku mmoja wa vijana wa OFM akijifanya mteja na kupatana naye bei ya kuingia chumbani kwa ‘shoti taimu’.
Baada ya kunaswa, mwanadada huyo alikiri mbele ya OFM kuwa ni bibi harusi mtarajiwa.
“Jamani… jamani ni kweli mimi ni mchumba wa mtu, shetani ameniponza nisameheni,” alisema.

Hata hivyo, kilio chake kiligeuka cha samaki kwani hakikusikika, yeye na wenzake walionaswa walipelekwa moja kwa moja katika kituo kikuu cha polisi ili kupisha sheria ichukue mkondo wake