LAZIMA utokwe machozi! Grace John mkazi wa Mzumbe, Mvomero mkoani Morogoro yupo kwenye wakati mgumu kutokana |
Honolina Christian Mkude (11) anayesumbuliwa na ugonjwa wa kuota nyama.
Honolina
anasumbuliwa na ugonjwa wa kuota nyama sehemu za mwili wake
zinazofanana na pembe za mnyama, ugonjwa ambao unamtesa tangu kuzaliwa
kwake.MATUKIO NA VIJANA
ILIKUWAJE?
Akisimulia kisa kizima, mama mzazi wa Honolina, Bi. Grace, anasema tangu amemzaa mwanaye huyo ni mitihani baada ya mitihani.
Mazungumzo
hayo yalifanyika hivi karibuni katika kituo cha mabasi ya mikoani,
Msamvu, mjini hapa wakati mama huyo na mwanaye wakihangaikia kuchangisha
fedha za usafiri wa kwenda Moshi kutafuta tiba zaidi katika Hospitali
ya Kilimanjaro Christian Medical Centre (KCMC).
“Ndugu
mwandishi, kwa kweli sijui hatima ya mwanangu. Nilimzaa akiwa ameota
nywele sehemu zote za mwili wake, hadi usoni. Mimi na mume wangu
tulishangaa, lakini tuliendelea na matibabu katika hospitali mbalimbali
maana baadaye alianza kupatwa na uvimbe.
Mtoto Honolina akipata kinywaji.
MTIHANI MWINGINE
“Jamani
ndugu yangu... Mungu ana mitihani yake. Mume wangu (Christian Mkude)
ambaye ndiye alikuwa tegemeo pekee kwetu, alifariki mwaka 2007 kwa ajali
ya gari, wakati akisaka fedha za matibabu ya mwanetu.
“Kifo chake, kwangu kimekuwa pigo mujalabu. Sina pa kukimbilia na
hivi juzi tu tulikuwa tumelazwa Hospitali ya Mkoa (Morogoro) na hapo
tumepewa barua ya kwenda KCMC kwa matibabu zaidi.
“Hivi
unavyoniona nachangisha fedha ili nipate angalau nauli za kutufikisha
kwanza hospitalini. Nimechanganyikiwa kabisa,” alisema Bi. Grace kwa
majonzi na kuongeza:
“Wakati
tatizo la mwanangu linaanza sikutegemea kama siku moja angekuja kuwa
hivi. Zilianza kuota nywele mwili mzima, baadaye vidonda vikaanza
kumtoka na sasa hali imebadilika na kuota nyama hizi kubwa kama mapembe
kama unavyoona.”
SAUTI YA BI. GRACE KUTOKA MOSHI
Misaada
ya fedha kidogo alizopata kwa wasamaria wema waliomuona Msamvu,
ulimsaidia mama huyo kusafiri hadi Moshi na kufika katika Hospitali ya
KCMC.
Akizungumza kwa njia ya simu kutoka Moshi, Bi. Grace alisema:
“Nawashukuru waliniosaidia, tumefika salama na mwanangu hapa KCMC, ndiyo
tumeanza taratibu za matibabu.”
BADO ANAHITAJI MSAADA
“Madaktari wametupa moyo, wamesema watajaribu kumsaidia mwanangu.
Watamtoa hizo nyama ila kwa sababu kutabaki na mashimo lazima
wapandikize nyama nyingine.
“Tumeshakubaliana kuwa mimi ndiye nitakayekatwa sehemu ya nyama
kutoka kwenye makalio yangu kwa ajili ya kumsaidia mwanangu,” alisema
Bi. Grace, kilio kikisikika kwenye simu.
Akaongeza:
“Wameshachukua nyama za mwanangu na kwenda kupima na baadaye watachukua
zangu ili kuona kama zinaendana, upasuaji ufanyike. Gharama kwa ajili
ya matibabu hayo wamesema ni shilingi 400,000 na mimi sina uwezo.
“Watanzania
wenzangu, naombeni mnisaidie ili niweze kuondokana na hili tatizo. Mimi
ni mjane na sina kazi ya kueleweka, napigania uhai wa mwanangu.
Naombeni msaada wenu,” alisema.
Kumsaidia mhitaji wa kweli huongeza baraka katika kipato, vitabu
vitakatifu vinaeleza wazi. Ndugu wasomaji wetu wapenzi, kwa yeyote
atakayeguswa na mateso ya familia hii, anaweza kumsaidia chochote mama
huyo kupitia simu zake namba 0719 749542(Tigopesa) na 0762 425973 (M - pesa).
No comments:
Post a Comment