ULE
uvumi kwamba baadhi ya wachungaji na maaskofu wa makanisa ya kiroho
nchini wanajihusisha na imani ya Freemason unazidi kushika kasi huku
awamu hii ‘rungu’ likimwangukia Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC) la
Ubungo jijini Dar, Lusekelo Mzee wa Upako’ na kutikisika,
MINONG’ONO ILIVYOANZA
Madai ya mtumishi huyo kujihusisha na imani ya Freemason yalianza kuenea kwa kasi mithili ya moto nyikani
huku baadhi ya watu, wakiwemo watumishi wa makanisa ya Kikristo,
wakionesha shaka juu ya uponyaji wa mtumishi huyo kufuatia miujiza ya
ajabu ambayo amekuwa akiionesha kwa watu wenye uhitaji wa kiimani.
MATENDO YA SHAKA
Baadhi
ya matendo ambayo yamekuwa yakiwatia shaka baadhi ya watu ni pamoja na
kitendo cha mchungaji huyo kuwaombea watu wakiwa hawana kitu kabisa
lakini baada ya miezi michache hurudi kanisani hapo wakiwa na magari ya
kifahari na wakionesha kila dalili ya ukwasi (utajiri).
“Eti unakuta mtu amekwenda kuombewa akiwa hana kitu kabisa (fukara) lakini bada ya miezi michache anarudi akiwa na gari la kifahari, kweli? “Tena
anaonesha kila dalili ya ukwasi, huenda ni kweli kuna nguvu za ziada
zaidi ya ile ya kiroho,” walisema baadhi ya waumini wa makanisa
mbalimbali ya Kikristo walipozungumza na gazeti hili hivi karibuni.
ALAMA NA VIASHIRIA TATA
Wakifafanua
kwa kina zaidi juu ya wasiwasi wao kwa Mzee wa Upako na miujiza yake,
waumini hao walitolea mfano wa baadhi ya dalili na viashiria tata
vinavyoshukiwa kuwa ni moja ya utambulisho wa Taasisi ya Freemason. Wakitaja baadhi ya alama hizo, waumini hao walisema mara nyingi mtumishi huyo akiwa madhabahuni amekuwa akitumia kitambaa kikubwa.
“Kila
akiwa jukwaani au madhabahuni hutumia kitambaa kikubwa kujifutia na
kuwagusia anaowaombea hali ambayo huwafanya kuanguka na kupiga kelele
hovyo,” walisema. Mbali
na kitambaa, pia walisema Mzee wa Upako amekuwa akionekana na pete
zenye picha za ajabu akiwa anahubiri au kutenda miujiza.
MADAI ZAIDI
Baadhi
ya waumini hao walisema viashiria vingine ni kitendo cha mchungaji huyo
kutotaja neno Mbinguni katika mahubiri yake zaidi ya kusema, ‘Mungu
wangu awabariki sana’. “Mapete
yake yana mapicha ya ajabu sana, yale maalama ya Freemason yapo, pia
huwa hawezi kusema Mungu wa Mbinguni, badala yake husema ‘Mungu wangu
awatangulie’ au ‘kwa uwezo wa Mungu ninaye mwabudu’jambo ambalo hututia shaka sana,” walisema Wakristo hao.
WAUMINI WAMBANA
Katika kufuatilia kwa kina sakata hilo, habari zikadai kuwa baada ya mambo kupamba moto waumini wa kanisa lake walianza kumbana mtumishi wao huyo kuhusu uvumi huo huku baadhi yao wakianza kutimkia kwingine. “Ni kweli zahama hiyo iliwahi kutokea, lakini mambo yalikaa sawa baada ya Lusekelo kutufafanulia zaidi juu ya madai hayo,” alisema mmoja wa waumini wa
kanisa hilo kwa sharti la kutotajwa jina lake gazetini.
LUSEKELO KIZIMBANI
Baada
ya kupata taarifa hizo nzito, hivi karibuni waliamua
‘kukanyaga lami’ hadi kanisani kwa mchungaji huyo, Ubungo -Kibangu
ambapo licha ya kukumbana na vikwazo mbalimbali walibahatika kukutana
naye na kumbana kwa maswali juu ya tuhuma hizo ambapo kwa ‘jasho
jembamba’ aliweza kueleza kwa kina: “Hizo
tuhuma zilianza kusikika zamani sana, watu walianza kunituhumu kwenye
matumizi ya bendera ya taifa kanisani, nikatoa, wakahamia kwenye
kitambaa.
“Jamani natumia muda mwingi sana kusimama madhabahuni. Sasa
nikitumia kitambaa (hendkachifu) cha shilingi mia tano itawezekana
kweli, natumia kitaulo kidogo kujifutia jasho, sasa inaonekana nongwa. “Baadaye
wakahamia kwenye pete! Mimi ni mtu smart sana (msafi) nimezaliwa mjini
(born town) sasa kuvaa pete ni sehemu ya maisha ya mjini sioni tabu,
lakini baada ya manenomaneno nilivua na sasa sina,” alisema Mzee wa
Upako.
KUHUSU WAUMINI KUTIMKA
“Ni
kweli, baadhi waliniuliza nikawajibu, wengine wakaamua kutimka. Unajua
mimi nimeanza kumtumikia Mungu kwa miaka thelathini sasa, muumini kuhama
kanisa na kwenda kwingine sishangai.
“Lakini wajue kwamba hapa
kwangu ni moto mkubwa, super charge, cartapillar, siteteleki, nitazidi
kuwaombea na kuwaponya wenye taabu na magonjwa,” aliongeza.
KUHUSU FREEMASON?
“Sijawahi
kufikiria hata siku moja kuwa Freemason, kwanza sifahamu hata
wanavyopatikana, nimeanza kumtumikia Mungu nikiwa kijana mdogo, mimi si
muumini wa dini wala imani yoyote ya kishetani. “Shetani
mwenyewe ananiogopa, sasa hao wanaosema kuwa huwa sisemi Mungu wa
Mbinguni, nashangaa, ni lazima kuweka neno Mbinguni? Jamani hao
Freemason siwajui, wala siwazuii watu kuniita hivyo, naendelea
kulihuburi Neno la Mungu aliye hai,” alisema Lusekelo na kufunga ‘faili’
la mazungumzo na waandishi wetu.
No comments:
Post a Comment