Mtu pekee aliyeweza kuibadilisha na kuinua mafanikio ya sigara duniani
haswa sigara maarufu ya Marlboro, Eric Lawson (Pichani kulia) amefariki
dunia.
Mwanaume
aliyekuwa na mvuto, mcheza filamu ambaye alikuwa mpanda farasi maarufu
Southwest, aliyetoka Texas mpaka Colorado na kwenda Arizona nchini
Marekani, ambaye pia aliweza kuinua kampuni ya Phillip Morris Tobacco na
kulinda utamaduni wa kweli wa Kimarekani wa Cowboy, na kweli aliweza
kuvuta sigara za Marlboro mpaka paketi 3 kwa siku.
Lawson alikuwa
bado anavuta sigara mwaka 2006 alipogundulika kuwa na ugonjwa
usiotibika wa mapafu. Alifariki dunia kutokana na ugonjwa huo akiwa
nyumbani kwake San Luis Obispo tarehe 10 mwezi januari akiwa na miaka
72.
Kwa miaka 3, mwishoni mwa miaka ya 70 na mwanzoni wa miaka ya
80, Lawson alipata umaarufu mkubwa katika matangazo na kuwakilisha
utamaduni wa kimarekani.
Katika miaka kadhaa iliyopita Lawson
aliongelea sana na kwa ukali madhara ya uvutaji sigara, alifanya huduma
za kujitolea na kutoa matangazo kadhaa kwaajili ya taasisi ya saratani
ya Marekani ya American Cancer Society miaka ya 90, ikiwa ni miaka
michache kabla hajaacha kuvuta sigara.
“Alijitahidi kuongea na
watoto, kuwaambia wasianze kuvuta sigara”, alisema mkewe Susan Lawson
akiliambia shirika la AP akiongeza “alijua sigara
No comments:
Post a Comment