Pages

Translate

Friday, 27 December 2013

JAIRO NA NYONI WAVULIWA UONGOZI NA SEREKALI

Serikali imewasafisha aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Blandina Nyoni na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo huku ikimpandisha cheo aliyekuwa Mganga Mkuu wa Serikali Deo Mtasiwa.

Nyoni alisimamishwa kazi pamoja na aliyekuwa Mganga Mkuu wa Serikali, Dk Deo Mtasiwa  na wote kwa pamoja walikuwa na tuhuma za kutumia vibaya madaraka yao wakiwa watumishi wa umma.

Jairo kwa upande wake alisimamishwa kazi kutokana na kuchangisha fedha kinyume cha sheria kwa lengo la kusaidia mchakato wa kupitisha bajeti ya wizara yake, katika mwaka wa fedha 2011/2012 na sasa ameondolewa kwenye utumishi wa umma, huku Bunge likiwa bado halijapata taarifa ya utekelezaji wa maazimio yanayomuhusu.

Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa Nyoni kwa sasa amerejea kwa mwajiri wake wa awali, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), akishikilia nafasi ya mmoja wa wakuu wa idara, huku Dk Mtasiwa akiwa ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa (Tamisemi).

Katibu Mkuu Kiongozi

 Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue amelithibitishia gazeti hili kuhusu watumishi hao na kwamba taratibu zimefuatwa.

“Mimi ninachojua ni kwamba Blandina alikuwa mwajiriwa wa TRA na mkataba wake ulikuwa haujaisha… Siyo kwamba alikuwa na mikataba miwili, kwenye utumishi wa umma huwa kuna utaratibu wa kuazima watumishi wa umma.

Ndiyo maana unaweza kukuta mwanajeshi anatolewa jeshini na kupelekwa uraiani au mtumishi kutoka idara moja kwenda nyingine. Kwa upande wetu sisi tulishamwondoa kwenye ukatibu mkuu na kule TRA hakuwa na tatizo,” alisema Balozi Sefue.

Kuhusu Dk Mtasiwa alisema: Uteuzi wa Dk Mtasiwa ulikuwa wazi na hata alipoapishwa mambo yote yalitangazwa hadharani.” Aliendelea kufafanua kuhusu Jairo akisema: “Jairo alishaondolewa kwenye ukatibu mkuu, siyo mtumishi tena wa umma.” Naye Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo alimtetea Nyoni akisema kuwa amerudi kwenye ajira yake ya awali.

“Siyo kwamba ameajiriwa TRA, amerudi tu kwenye ajira yake ya zamani, alikuwa akifanya kazi hapa akaazimwa na sasa amerudi,” alisema Kayombo na kuongeza: “Kwani amefanya kosa gani? Kuna mashtaka yoyote aliyofanya unaweza kuyathibitisha?”

Kauli hiyo iliungwa mkono na Mwenyekiti wa Bodi ya TRA, Bernard Mchomvu ambaye alisema Nyoni alishasafishwa na Serikali ndiyo maana wamempokea. “Yule aliazimwa tu na Serikali…Sasa kama Serikali imesham-clear sisi tutamkataaje?” alihoji na kuongeza:

“Kwa sababu sikumwomba huyo mtu, nimeambiwa kwamba huyo yuko safi mimi nifanyeje? Unajua watu wanafurahia wengine wakipata matatizo, hata kama mtu ameua, basi walete ushahidi. Hata unaposema nchi imejaa rushwa, ulete ushahidi… kama Serikali imeshamsafisha, ningemkataa ningekuwa mtu wa ajabu.”

Thursday, 12 December 2013

MSIGWA ASISITIZA KUWA BARAZA LA MAWAZIRI LIMEDUMAA

  
MBUNGE wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (CHADEMA), amesema asilimia 40 ya Baraza la Mawaziri limedumaa kwa sababu limeshindwa kutekeleza majukumu yake. Msigwa pia alikilaumu Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa kimeshakuwa chakavu kwa kushindwa kutoa matumaini kwa Watanzania. Alitoa kauli hiyo bungeni juzi wakati akichangia mjadala wa taarifa za Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa, Kamati ya Bunge ya Bajeti na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali. Alisema kila mwaka wabunge wamekuwa wakizungumza mambo yale yale na serikali imekuwa ikijibu vilevile wakati matatizo yale yale yameendelea kuwepo.

      “Bunge la mwaka juzi la Bajeti nilitoa takwimu za Wizara ya Afya, kwamba asilimia 42 ya watoto wanaozaliwa Tanzania wamedumaa, mtu anayedumaa hawezi kufikiri, hawezi kuhoji wala kudadisi, kwa kutumia takwimu hizi hizi Baraza la Mawaziri  ambao ni zaidi ya mawaziri 56, asilimia 40 wamedumaa na moja ya sababu ya kudumaa ni changamoto wanazozipata katika Bunge hili. “Kila mwaka tunazungumza yale yale, tunapata majibu yale, watu hawabadiliki maana yake kuna tatizo kwenye akili zao. “Matatizo ya wizi wa fedha lazima tuyapatie ufumbuzi, haiwezekani kila siku tuseme yale yale, matatizo yapo pale pale,” alisema. Mchungaji Msigwa alisema lazima kuwepo kwa nidhamu ya  matumizi ya fedha za serikali na kuitaka serikali kuzikumbusha halmashauri kwamba nchi inaongozwa kwa mfumo wa vyama vingi.
        “Katika jimbo langu magari ya halmashaiuri yanatumika katika shughuli za chama, mkurugenzi na meya wanalazimishwa  na madiwani kwenda uwanja wa ndege kumpokea Nape na Kinana, huu ni utovu wa nidhamu wa matumizi ya fedha za umma na haukubaliki. “Ukiona mbunge rafiki wa  mkurugenzi uje hapo kuna ‘deal’, ukiona meya rafiki wa mkurugenzi hapo kuna kitu. Mkurugenzi na mbunge wakiwa maaadui ujue  mkurugenzi huyo anasimamia vizuri matumizi ya fedha,” alisema. Msigwa alisema ni wakati muafaka wa Watanzania kuchagua chama mbadala kuongoza nchi badala ya kuendelea  kuichagua CCM. “Nashukuru sasa hadi Katibu Mkuu wenu wa chama kasema wazi kwamba baadhi ya mawaziri ni mzigo, kazi yao ni kufunga tai na kutembea mjini tu.

      “Mbeya aliwaomba radhi Watanzania, sasa mnaanza kuongea lugha yetu kwamba kuna mizigo, yaani hadi muambiane wenyewe ndo mnakubaliana… Hii Big Result Now mmewakaririsha watu kama kasuku, mnahadaa Watanzania wakati watu ni wale wale, wanafikiri vilevile, wanatenda vile vile eti Big Result Now. “Watanzania muda muafaka umefika, hiki chama chakavu kimechoka ni vizuri tulete chama mbadala, mabadiliko yamefanywa sana hasa katika Baraza la Mawaziri, lakini mambo bado yale yale,” alisema. Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (CHADEMA) alisema chanzo kikubwa cha ubadhirifu wa fedha katika halmashauri ni wakurugenzi na wenyeviti wa halmashauri au mameya huku akitoa mfano kwa Jiji la Mbeya. Mbunge wa Busega, Dk. Titus Kamani (CCM) aliitaka serikali kuchukua hatua za haraka kwa wale wote watakaobainika kuiba fedha za serikali. Dk. Kamani pia alimtetea Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwamba ni kiongozi muadilifu, na kwamba anashangaa siasa za Tanzania kiongozi muadilifu ndiye anayepigwa mawe.

SAUZI YAJAA...HAKUNA PA KUKANYAGA...NAMBA 3 YAWAMALIZA VIGOGO....SOMA ZAIDI HAPA


Wanajeshi wakiwa wameubeba mwili wa hayati Mandela kuelekea ofisi za serikali jijini Pretoria.

MAOMBOLEZO ya kifo cha aliyekuwa rais wa kwanza mweusi nchini Afrika Kusini, Nelson Mandela yanaendelea, kubwa kuliko ni nchi hiyo yenye kilomita za mraba 2,798 kufurika waombolezaji kutoka pande zote za dunia na hivyo, hakuna pa kukanyaga na hali hii ni mwanzo na mwisho!


Nelson Mandela.
Habari kutoka jijini Johannesburg nchini humo zinasema, msiba wa Mandela umebadilisha ghafla hali ya maisha ya raia wa nchi hiyo.

HOTELI HAZINA NAFASI
 
Hoteli nyingi, hasa katika Miji ya Pretoria na Johannesburg (alikofia Mandela), nyumba za kulala wageni, hoteli na sehemu nyingine zenye kuhifadhi watu zimejaa baada ya wateja kukodi kwa muda wote wa msiba hadi mazishi.


Wageni wanaoingia nchini humo kwa ratiba zao za kabla ya kifo wamekuwa wakipata tabu sehemu za kulala, wengine kugeuza wanakotoka.


Familia ya marehemu Mandela ikifuatilia ibada ya kumbukumbu.
 
Baadhi ya wenyeji waishio nchini humo wamewasiliana na ndugu zao wanaotaka kwenda, kusitisha safari ili kupisha shughuli za mazishi yatakayofanyika Desemba 15, mwaka huu.

BIDHAA BEI JUU
 
Licha ya kwamba kipato cha kawaida kwa wananchi wake ni cha chini, bei ya bidhaa, hasa vyakula imepanda na wafanyabiashara wengi wanaitumia fursa hiyo kujineemesha.


Rais wa Marekani, Barrack Obama akiwapungia maelfu ya wananchi waliohudhuria ibada ya kumkumbuka Mandela katika Uwanja wa FNB, Soweto, Afrika Kusini.
MIPAKA HAIPITIKI KAMA ZAMANI
 
Tofauti na hali ilivyokuwa kabla ya kifo cha Mandela ambapo wengi waliweza kuingia nchini humo bila kubanwa na ukaguzi wa kina, kwa sasa ulinzi umeimarishwa ambapo kila muingiaji anaulizwa maswali mengi, hasa yanayohusu usalama.


MAGAIDI WATUPIWA MACHO ZAIDI
Usalama nchini humo tangu kutokea kwa kifo cha Mandela umekuwa ukiwatupia macho zaidi magaidi wa kimataifa ambao wanaweza kutumia mwanya wa maombolezo kupenya na kusababisha maafa.


Baadhi ya waombolezaji.

GRACA MACHEL, WINNIE MANDELA HAKUNA BIFU
 
Juzi ndani ya Uwanja wa FNB uliopo Mtaa wa Soccer City nchini humo wakati wa zoezi la kumuaga marehemu Mandela, kivutio kikubwa kilikuwa kwa wanawake wawili waliowahi kuwa na uhusiano na kiongozi huyo.


Winnie Medekizela Mandela, aliyewahi kuwa mke wa Mandela mpaka kutoka kifungoni na Graca Machel aliyekuwa mke mpaka kifo cha Mandela, walitazamwa na waombolezaji wengi kufuatia historia zao kutokuwa na migongano.

Wawili hao, mara kadhaa wamewahi kupiga picha ya pamoja na mzee huyo wakiwa na nyuso za furaha huku wote wakiwa wamemkumbatia.

Viongozi mbalimbali akiwemo Rais Jakaya Kikwete (wa nne mstari wa pili kulia kutoka juu) na mkewe Mama Salma wakifuatilia ibada ya kumbukumbu ya Nelson Mandela.
OBAMA AHUTUBIA NDANI YA JUKWAA LENYE VIOO VYA KUKINGA RISASI
 
Akitoa hotuba yake kwa wananchi wa Sauzi na waombolezaji wengine duniani kote, Rais wa Marekani, Barack Obama alionekana ndani ya jukwaa lenye vioo visivyoweza kupitwa na risasi (bullet proof).


DUNIA YAANDIKA HISTORIA MPYA
 
Kuwepo kwa Rais wa Marekani, Barack Obama na Rais wa China, Xi-Jinping kunasemekana ni kuandikwa kwa historia mpya ya dunia kwani viongozi hao hawajawahi kukutana nje ya nchi zao.


Kingine kilichoonekana ni kuandikwa kwa historia mpya ya dunia ni tukio hilo kuwa la kwanza kukutanisha viongozi wazito wa duniani kwa wakati mmoja.

Inadaiwa hata wanaokwenda kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa hawakufikia uzito wa kwenye msiba wa Mandela.

Marais mbalimbali wakiambatana na ujumbe mzito kutoka katika nchi zao walihudhuria msiba huo, ukiachana na watu wengine maarufu na viongozi wa kawaida.


JINA LA KIKWETE LAWA LA KWANZA KWENYE ORODHA
 
Katika hali iliyoonesha mshikamano kati ya Afrika Kusini na Tanzania, jina la Rais Jakaya Kikwete lilikuwa la kwanza katika orodha ya marais waliokuwa kwenye mwaliko.


Jambo hilo limeongeza hamasa na uhusika wa moja kwa moja kwa Watanzania juu ya msiba huo kutokana na umoja, ushirikiano na kuaminiana kulikooneshwa na Sauzi.

Juzi, Jumatatu, Desemba 9, mwaka huu katika sherehe za Miaka 52 ya Uhuru, zilizofanyika kitaifa, Uwanja wa Uhuru, Dar, Rais Kikwete alizungumzia namna marehemu Mandela alivyoipenda Tanzania na uhusiano mwema wa nchi hizi mbili.
Hilo lilijidhihirisha baada ya Sauzi kumweka Rais Kikwete wa kwanza, akiwaongoza marais na viongozi wengine waliohudhuria msiba na shughuli za mazishi ya shujaa huyo.

NAMBA 3 YAWAMALIZA VIGOGO NCHINI HUMO
Pamoja na yote, namba 3 imeonekana kuweka historia ya kipekee nchini humo kwa kuhusika na vifo vya viongozi wake wakuu.


Mpigania haki mwingine mkongwe, Oliver Tambo aliyezaliwa Oktoba 27, 1917 naye alifariki mwaka 1993 (Aprili 24). Walter Sisulu, alikuwa mpigania uhuru sambamba na Tambo na Mandela, naye alifariki dunia mwaka 2003 (Mei 5, alizaliwa Mei 18, 1912).


Kifo cha Mandela kilichotokea Desemba 5, 2013 kinazidi kutia shaka katika orodha ya namba 3 kila baada ya miaka 10. 

Marehemu Nelson Mandela ambaye zoezi la kuuaga mwili wake linakamilika leo kwenye uwanja huo, atazikwa Jumapili ijayo.


 Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi - Amina.

WIVU WA MAPENZI WAMFANYA MICHELLE KUBADIRISHANA KITI NA MUMEWE OBAMA HUKO A. KUSINI



Inaonekana Rais Obama alikuwa na wakati mzuri sana katika Mandela's Memorial service mpaka pale mke wake Mitchelle Obama alipoingilia kati ka kuharibu kila kitu, unaweza ukawa Rais wa Dunia ila mke wako akisema badili siti tu,  Mtazame Michelle Obama yupo pembeni anafatilia kwa makini mno

Inaonekana hapo Mitchelle Obama aligeuka na kuangali kinachoendelea baina ya Obama na Huyu mwanamke

hapa Obama alikuwa Bize huku huyu mwanamke akionekana kuendelea kupiga story

Baada ya uvumilivu kumshinda Mitchelle Obama akaamua kubadilisha siti ili mumewe asisumbuliwe tena.
Mapenzi noma sana

Tuesday, 3 December 2013

DK SLAA ASITISHA ZIARA YAKE KUTOKANA NA HALI YA USALAMA KUTOKUWA SHWARI

 
MWANGWI wa uamuzi wa Kamati Kuu ya Chadema wa kumvua madaraka aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Kabwe Zitto na wenzake, mbali na kutikisa katika kanda sita kati ya kanda nane muhimu za chama hicho nchini, sasa umeanza kukubalika na Sekretarieti ya chama hicho Taifa. 


Jana Kurugenzi ya Habari ya Chadema, ilituma ratiba ya ziara za Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa, mikoani iliyoonesha amekubali ushauri wa kusogeza mbele ziara ya kutembelea majimbo nane ya Kigoma.



Awali Dk Slaa alitarajiwa kuanza ziara ya kuimarisha chama mkoani Kigoma kuanzia kesho lakini juzi Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Kigoma, Jafari Kasisiko, alisema baada ya kutafakari kwa kina na kwa kutumia hekima na busara, walipendekeza ziara hiyo isogezwe mbele.



Sababu za mapendekezo hayo kwa mujibu wa Kasisiko, ni kutoa nafasi kwa uongozi wa Mkoa, kwenda kuwaelimisha wanachama kutii uamuzi wa Kamati Kuu wa kumvua madaraka Zitto na wenzake, hata kama uamuzi huo umewaudhi, lakini lengo ni kudhibiti vitisho vya kuvuruga amani katika ziara hiyo vilivyokuwa vimetolewa. 



“Mkoa uliomba Taifa liahirishe na kusogeza mbele tarehe ya ziara hiyo muhimu kwa mkoa wetu, ili Mkoa kama ngazi ya chini ya Kanda na Taifa, uende katika majimbo hayo na kuwaelimisha wanachama na wapenzi wetu, kuhusu kuheshimu na kuwa na nidhamu na uamuzi utolewao na ngazi ya juu yetu, hata kama una maumivu. 



“Maoni ya wengi mkoani na kwa viongozi wa Chama ni kuudhiwa na uamuzi wa Kamati Kuu ambao ni dhahiri ulilenga kummaliza Zitto kisiasa. 


Mkoa ulitishika na vitisho baada ya kupokea taarifa kutoka kwa baadhi ya viongozi wa majimbo ya Mkoa, kuwa hali ya usalama si nzuri kwa ujio wa kiongozi wetu Dk Slaa… endapo hali haitokuwa salama Mungu aepushie mbali,” alisema Kasisiko katika taarifa yake. 



Dk Slaa ashaurika Pamoja na Chadema kusisitiza kuwa ziara hiyo itakuwepo, lakini taarifa ya jana ya Kurugenzi ya Habari ya Chadema, ilieleza kuwa badala ya kuanza ziara mkoani Kigoma kama ilivyokuwa awali, sasa ataanza ziara ya siku 20 kuanzia leo lakini mkoani Shinyanga. 



Bila kufafanua atakaa Shinyanga kwa siku ngapi, taarifa hiyo ilifafanua kwamba ziara hiyo itamfikisha Dk Slaa mpaka mkoani Kigoma, ingawa haikueleza lini atakwenda katika mkoa huo anakotoka Zitto na atakaa kwa siku ngapi.



“Siku ya Jumatano Desemba 4 mwaka huu (leo), Katibu Mkuu Dk Slaa atakuwa Wilaya ya Kahama, siku inayofuata Desemba 5, atakuwa Wilaya ya Kakonko, Jimbo la Buyungu na Desemba 6, atakuwa Jimbo la Muhambwe. Ratiba ya siku zinazofuata itaendelea kutolewa kwa vyombo vya habari,” ilieleza taarifa hiyo ya Kurugenzi ya Habari ya Chadema.



Mwenyekiti Singida
Wakati Dk Slaa akianza ziara za kuimarisha chama, vuguvugu la kupinga uamuzi wa kuvuliwa madaraka kwa Zitto, limeendelea kutikisa chama hicho katika kanda zake, ambapo jana katika Kanda ya Kati, Mwenyekiti wa Mkoa wa Singida, Wilfred Kitundu, alijiuzulu. 



Mwenyekiti huyo ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa tangu 1992, amechukua uamuzi huo kupinga Kamati Kuu kuwavua madaraka akina Zitto, hatua ambayo imeshachukuliwa katika kanda tano za chama hicho nchini. 



“Nimeona ni vema sasa niuthibitishie umma wa Tanzania kuwa kwenye Chadema unaruhusiwa kugombea vyeo na nafasi zote isipokuwa Uenyekiti wa Taifa, ndio maana Zitto tuliyemuunga mkono, leo hii anashambuliwa kwa dhamira yake safi ya kidemokrasia. 



“Tunampa onyo kali Katibu Mkuu Dk Slaa kuwa asithubutu kukanyaga Singida, ikiwa bado hajayafanyia kazi maelekezo yetu hapo juu. Kuzunguka kwake mikoani baada ya kumvua vyeo Zitto ni kwenda kuthibitisha kuwa amefanya makusudi mpango wake huo. 



“Nimejiuzulu Uenyekiti wa Mkoa wa Singida kuanzia leo (jana) tarehe 3.11.2013 na kuahidi kuwa nitapambana mpaka mwisho wa tone la damu ya uhai wangu, kuhakikisha demokrasia ya ndani ya chama hiki inaheshimiwa na kwamba Watanzania hawadanganywi tena,” alisema Kitundu katika taarifa yake ndefu kwa umma. 



Ofisi Arusha
Wakati katika Kanda ya Kati Kitundu akijiuzulu, ofisi za chama hicho za Wilaya ya Arusha, Mkoa na Kanda ya Kaskazini jana zilichomwa moto na watu wasiojulikana. 



Akizungumza na gazeti hili, Mwenyekiti wa Chadema ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Levolosi, Ephata Nanyaro, alikiri kuchomwa kwa ofisi hizo zilizoko katika jengo moja eneo la Ngarenaro jijini hapa. 



Nanyaro alisema ofisi hizo wana wasiwasi zilichomwa saa moja asubuhi kwa kuwa hali hiyo ilionekana saa mbili asubuhi baada ya ofisi hiyo kufunguliwa na kukuta moto ukiwaka katika baadhi ya maeneo. 



“Ofisi imechomwa moto eneo la juu lakini huenda mchomaji alikuja na kutupia moto juu ya paa. Hata hivyo hawajafanikiwa malengo yao maana ni paa tuu na mbao zilizoshika moto,” alisema Nanyaro.


Alisema ana wasiwasi kuwa tukio hilo lilitekelezwa na watu aliowaita wahujumu wa chama chao, ambao ni wale waliofukuzwa hivi karibuni na chama hicho wakiwatumia watu aliowaita kuwa ni wafuasi wao bila kufafanua zaidi. 



Hata hivyo, kiongozi aliyetimuliwa hivi karibuni, Ijumaa iliyopita ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Wilaya ya Monduli, Mchungaji Amani Mollel, ambaye alidaiwa kukiuka kanuni za chama hicho baada ya kuitisha kikao cha kumtetea Zitto.



“Kwa niaba ya Baraza la Uongozi la Mkoa wa Arusha, napenda kuujulisha umma wote kwa ujumla kuwa Mwenyekiti wa Wilaya ya Monduli, Mchungaji Amani Silanga Mollel, amekoma/amesimamishwa kuwa Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Monduli kuanzia tarehe 29 Novemba 2013 kutokana na tuhuma nzito za uvunjifu wa kanuni za maadili ya chama,” alisema Katibu wa Chadema, Mkoa wa Arusha, Amani Golugwa alipokuwa akitangaza uamuzi huo mwishoni mwa wiki iliyopita.



Kanda zingine
Kanda zingine zilizokwisha kutoa kauli za kupinga Kamati Kuu ni pamoja na Kanda ya Mashariki Dar es Salaam na Pwani, kupitia kwa Mwenyekiti wa Chadema wa Wilaya ya Temeke na mjumbe wa Baraza Kuu, Patrick Joseph, Kanda ya Kusini, Lindi ambako Mwenyekiti wa mkoa huo, Ally Chitanda, alijiuzulu wadhifa wake na kubakia na ujumbe Baraza Kuu Taifa. 



Kanda ya Ziwa Magharibi, Mwanza kulitolewa tamko na waliojiita umoja wa matawi 189 ya Chadema Mwanza, yakiongozwa na mwanachama Robert Gwanchele. Kwa sasa Chadema inajiendesha kupitia kanda 10. 



Kanda ya kwanza ni ya Mashariki Dar es Salaam, inayojumuisha mikoa ya Dar es Salaam na Pwani. Kanda ya pili ni Kusini, kwenye mikoa ya Lindi na Mtwara, ikifuatiwa na Kaskazini yenye mikoa ya Tanga, Manyara ,Kilimanjaro na Arusha. 



Pia ipo Kanda ya nne ya Kati inayojumuisha mikoa ya Morogoro, Dodoma na Singida; Kanda ya tano ya Nyanda za Juu Kusini, iliko mikoa ya Njombe, Iringa, Mbeya na Ruvuma. 



Kanda ya sita ya Magharibi inajumuisha mikoa ya Rukwa, Katavi, Tabora na Kigoma; Kanda ya saba ya Ziwa Mashariki yenye mikoa ya Shinyanga, Simiyu na Mara na Kanda ya nane ni Ziwa Magharibi, yenye mikoa ya Mwanza, Geita na Kagera. 



Pia zipo Kanda ya tisa ya Pemba, yenye mikoa ya Pemba Kusini na Pemba Kaskazini na Kanda ya kumi ya Unguja. HABARILEO

VIAZI LISHE MKOMBOZI WA UMASKINI JIJINI MWANZA

 Na Lydia Mapunda

Kama ilivyo kawaida ya misemo ya watafiti wengi wasemao mbegu bora ndio tija kwa kilimo bora.  Msemo huu umekuwa ukitimia katika vituo mbalimbali vya utafiti katika kilimo kwa kujizatiti katika tafiti za mbegu bora zenye  manufaa kwa wakulima nchini.

Mkoani Mwanza kituo cha Ukiriguru Agricultural Research Institute kimefanya utafiti na kuja na mbegu mpya ya viazi vitamu vilivyopewa jina la viazi lishe. Mbegu hizi za viazi lishe vililetwa mwaka 2002 kutoka nchini Uganda na shirika la International Potato Centre  na kufanyiwa utafiti na hatimaye sasa kanda ya ziwa wameanza kufaidi matunda yake.

Viazi vitamu ni kati ya mazao makuu ya mizizi yanayozalishwa kwa wingi  na kutumiwa kama  chakula.

Mara zote zao hilo linapewa nafasi kubwa kuzalishwa na wakulima kwa sababu linavumilia ukame na linahesabiwa kuwa ni moja kati ya mazao ya kinga ya njaa kama ilivyo kilimo cha mihogo.
 


Mikoa inayoongoza kwa uzalishaji wa viazi vitamu ni Mwanza, Shinyanga, Dodoma, Morogoro, Kagera, Arusha na Ruvuma japo kuwa viazi vitamu hivi hilimwa karibu katika kila mkoa hapa Tanzania

Katika Mkoa wa Mwanza viazi lishe vimeonekana kuwa mkombozi baada ya TAHEA (Tanzania Home Economics Association) kuingilia kati na kuwasaidia wakulima kutambua umuhimu wa viazi hivyo. Kwa kushirikiana na taasisi ya utafiti ya Ukiriguru UARI (Ukiriguru Agricultural Research Institute), TAHEA waliamua kutoa mafunzo kwa wakulima ili waweze kujikwamua kimaendeleo na kiuchumi kupitia mbegu mpya za viazi lishe ambazo ni matokeo ya utafiti wa mbegu bora za viazi hivyo uliofanywa na UARI.
Wanawake ndio waliokuwa wakwanza kupata mafunzo hayo baada ya kuonekana wao ndio wakulima wa zao hilo kutokana na zana ya kwamba halina faida kibiashara hivyo kulimwa kwa matumizi ya chakula pekee.
Baada ya utafiti kufanyika na kupatikana aina tano ikiwa ni Ejumla, Karoti Dar, karoti C, Kabode na Jewel za mbegu mpya ambazo zimetofutiana matumizi na ustahimilivu wake, ndipo TAHEA ikawafundisha wanawakea hao kilimo bora, uvunaji bora pamoja na usindikaji ili kupata manufaa zaidi ambayo hapo awali hayakuwepo.
 
Pichani, Unga viazi lishe baada ya kuwekwa kwenye paketi tayari kwa kwenda sokoni 

Ramadhani Bundala ambaye ni afisa kilimo wa TAHEA akifafanua kazi kubwa ambayo wameifanya katika mradi huu wa kuwafundisha wakulima wa viazi kujikwamua kimaisha alisema kuwa“ wanawake wamekuwa wakielemewa sana na kazi za kulea familia huku wakijibakiza nyuma kuwa wao huwa wanalima mazao kwa ajili ya chakula hivyo tukaona ni bora tuwaelekeza wanawake hawa kuwa wanaweza wakalima viazi kama zao la biashara. Tukawaweka katika vikundi na kuwapa mbegu mpya kisha kuwafundisha kuanzia kuandaa shamba mpaka usindikaji. Huwezi amini kwa sasa kilimo hiki cha viazi kimevamiwa na wanaume baada ya kuona mafanikio walioyapata kwenye vikundi hivi.”
Bundala alisema kuwa mbali na kuwa chanzo cha mapato viazi lishe pia vina faida kubwa ikiwamo kuboresha afya hasa za watoto chini ya miaka mitano. Pia viazi lishe vyenye vitamin za aina nyingi ikiwamo vitamin A, vinasaidia watu wenye matatizo ya macho, kuboresha afya za akina mama wajawazito na wanaonyonyesha na kuongeza kinga ya mwili hasa kwa watu wanaoishi na maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi.
Kwa upande wao wakulima, wanakikundi cha Imala buhabi cha jijini mwanza wametoa shukrani zao kwa TAHEA pamoja na Ukiriguru kwa kuwafikisha walipo kwani wanamabadiriko makubwa kimaisha tofauti na hapo awali.

Naye Bi Mwanaidi  mjumbe wa kikundi hicho alisema kuwa japo kuwa yeye ni mjane anayelea familia anauwezo wa kuwapeleka watoto wake shule na kujenga nyumba nzuri ya familia kutokana na viazi lishe anavyolima.
Wakieleza kwa upande wa changamoto wakulima hao walisema kuwa pamoja na mafanikio hayo pia wakulima wa zao hilo wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo ni pamoja na ukosefu wa soko la uhakika na  ukosefu wa usafiri kutoka shambani kwenda sokoni.

Wameiomba serikali kushirikiana mashirika na kampuni binafsi kuwahamasisha wakulima  kuongeza jitihada katika kilimo hicho na kuongeza idadi ya maofisa ugani ili wawaongezee uwezo wa kuzalisha na kutafuta masoko zaidi. Na ikiwezekana serikali iwasaidie wakulima hawa kuwatangazia kazi zao katika soko la nje ili kuwaendeleza wakulima.

kwa mantiki hiyo basi Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA),  pia wanapaswa kuwafikia wakulima ili waweze kukagua kazi za wakulima, kuwaelimishe kwa lengo la kuwawezesha kuzalisha kwa ubora zaidi ili kuwapa uelewa wakulima ni jinsi gani wanaweza kuandaa bidhaa zao ili waweze kufika mbali zaidi na kujikwamua kutoka katika wimbi la kilimo duni na kufika mbali zaidi kama ilivyo katika kilimo cha mazao mengine kama vile kahawa, korosho na mazao mengine ambayo yapo kwenye ramani ya kuipatia pesa za kigeni nchi yetu.

Nae Robert Kileo afisa habari wa Ukiriguru amesema kuwa Kutokana na umuhimu wa viazi lishe Kituo cha utafiti wa Kilimo Ukiriguru  kikishirikiana na TAHEA kwa pamoja wamebuni mpango wa  kuhamasisha wakulima na wananchi kwa ujumla ili wafahamu umuhimu wa zao hilo.



Kileo alisema kwakuwa Tanzania ipo katika kufanya mapindizi ya kijani na kilimo kwanza inatakiwa kila sekta katika serikali kuunga mkono jitihada za wakulima ili kufanya kazi yakilimo iwe ajira kwa watanzania wengi ambao kilio chao kikubwa sasa ni ukosefu wa ajira nchini. 

Wataalam kutoka katika vituo hivyo wanasema kuwa, mbali na kuwaelimisha kuhusu faida zake pia wakulima wanaelimishwa umuhimu wa usindikaji wa viazi lishe na uendelezaji wa masoko katika mikoa ya kanda ya ziwa

Hivyo  serikali inapaswa kuingilia kati katika kuhamasisha wananchi kulima zao hilo, kutafuta masoko kwa ajili ya wakulima ambao wamekwishaanzisha kilimo hicho na kuwataka wananchi ambao bado hawajajiunga wafanye hivyo kwa manufaa yao na taifa kwa ujumla.

Ushauri mwingine kwa serikali ni kuhimiza matumizi ya teknolojia katika kukibadilisha kilimo cha viazi lishe ili kiwe cha kisasa na cha tija pamoja na kumwezesha mkulima mdogo kumiliki ardhi  na kuanzisha vituo vya kumsaidia.

Baadhi ya bidhaa zitokanazo na vizi lishe 



Monday, 2 December 2013

RIPOTI YA CAG YAWATESA MAWAZIRI NA WABUNGE



Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Ludovick S.L. Utouh.
 

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linaanza mkutano wake wa 14 mjini Dodoma leo, huku kukiwa na homa ya matokeo ya mjadala wa Taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2011/12.
Taarifa hiyo inatarajiwa kujadiliwa katika mkutano huo sambamba na majibu ya awali ya Serikali kuhusu kasoro katika matumizi ya fedha za umma zilizobainishwa na CAG, huku Kamati za Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) na ile ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), zikitarajiwa kutoa taarifa ambazo zitakuwa mwongozo wa mjadala bungeni.
Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah alisema jana kuwa, kwa kawaida wabunge wanapaswa kujadili taarifa ya CAG kabla ya mkutano wa Bunge la Bajeti ambalo hufanyika Aprili, ili kuwawezesha kutoa maoni na maelekezo yanayopaswa kuzingatiwa katika mwaka wa fedha unaofuata. Kwa kuzingatia kalenda ya mikutano ya Bunge, mkutano wa 14 ulipaswa kufanyika Februari 2014, lakini kama Spika Anne Makinda alivyotangaza katika mkutano uliopita, unafanyika kuanzia leo ili kutoa fursa kwa Bunge Maalumu la Katiba ambalo litakaa kati ya Januari na Machi 2014.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi alisema jana kuwa tayari Serikali ilishawasilisha majibu ya awali kuhusu hoja za ukaguzi na kwamba baada ya taarifa za LAAC na PAC kutakuwa na majibu ya nyongeza kwa hoja mpya zitakazoibuliwa na kamati hizo. “Serikali tayari ilishatoa majibu ya awali sasa kwa sababu Kamati za PAC na LAAC zilikuwa zikikutana na watendaji wakuu wa Serikali ambao taasisi au wizara zao zilionekana kuwa na kasoro kwenye hesabu, tutawasikia watasema nini na hapo ndipo Serikali itatoa tena ya nyongeza,” alisema Lukuvi.
Tangu Rais Jakaya Kikwete aliporidhia taarifa ya CAG kuwasilishwa bungeni kisha kujadiliwa na wabunge, baadhi ya vigogo wa Serikali wakiwamo mawaziri na watendaji wakuu ambao wizara na idara wanazoziongoza zilibainika kuhusika na upotevu mkubwa wa fedha za umma waling’olewa katika nafasi zao. Katika mjadala wa mwaka jana, mawaziri sita na naibu mawaziri wawili walitimuliwa kazi, yakiwa ni matokeo ya mjadala mkali bungeni wa ripoti ya CAG ya 2010/2011. Mbali na vigogo hao, pia fagio hilo liliwakumba wakurugenzi wakuu Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na yule wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA).
Hali hiyo inatajwa kuwa moja ya sababu zilizoisukuma Serikali kupeleka bungeni marekebisho katika Sheria ya Ukaguzi wa Hesabu za Umma ya 2008, huku ikiongeza vifungu ambavyo vilitafsiriwa kuwa vinapunguza nguvu ya Bunge katika kushughulikia taarifa ya CAG. Kwa maana hiyo, Bunge linajadili kwa mara ya kwanza ripoti ya CAG tangu marekebisho ya sheria hiyo yanayozuia Bunge kujadili ripoti ya CAG kabla Serikali haijajibu hoja za ukaguzi, yapitishwe bungeni Februari mwaka huu.
Operesheni tokomeza
Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira inatarajiwa kuwasilisha taarifa kuhusu Operesheni Tokomeza Ujangili iliyoanza Oktoba 4 mwaka huu ikishirikisha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Polisi, Usalama wa Taifa na Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa) kabla ya kusitishwa na Serikali Novemba Mosi. Uamuzi wa kusitishwa kwake ulitangazwa bungeni na Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki kutokana na wabunge wengi kuilalamikia kwamba iliambatana na uporaji, utesaji watuhumiwa na uchomaji nyumba za watu wasiokuwa na hatia. Jana, Dk Kashililah alisema kamati hiyo inayoongozwa na Mbunge wa Kahama (CCM), James Lembeli ilikuwa katika hatua za mwisho kukamilisha taarifa yake kama ilivyoagizwa na Spika Makinda na kwamba: “Huenda wakapewa nafasi ya kuwasilisha taarifa yao kutokana na umuhimu wake.”
Jana, Lembeli alikiri kamati yake kuanza kazi rasmi na kwamba tayari imewahoji watu mbalimbali wakiwamo viongozi wa Serikali na vyombo vya ulinzi na usalama lakini akakataa kuwataja. “Ni kweli tulishaanza kazi na tulianzia Dar es Salaam na tumehoji watu mbalimbali na kesho (leo) tunaanza kwenda mikoani lakini naomba nisizungumze zaidi ya hapo… mambo mengine subirini taarifa bungeni,” alisema Lembeli. Kusitishwa kwa Operesheni Tokomeza Ujangili kulionekana kumgusa pia Rais Jakaya Kikwete ambaye wakati akilihutubia Bunge Novemba 7, mwaka huu alisisitiza kuwa operesheni hiyo ilikuwa sahihi kwa masilahi ya nchi.
Shughuli nyingine
Dk Kashililah alisema Mkutano huo wa 14 wa Bunge utapokea na kujadili taarifa za kamati 15 za Bunge zikiwa na maazimio, mapendekezo au maelekezo kwa Serikali. Alitaja shughuli nyingine kuwa ni miswada miwili ya Serikali; wa Sheria ya Kura ya Maoni ya 2013 na Sheria ya Takwimu na kusomwa kwa mara ya kwanza kwa Muswada Binafsi wa Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (Chadema) unaohusu kuundwa kwa Mfuko wa Maendeleo ya Vijana nchini. Maazimio matatu ambayo yanahusu ushirikiano wa majeshi katika nchi wanachama wa Afrika Mashariki, ushirikiano wa masuala ya fedha katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) na Azimio la Mabadiliko ya Chuo cha Tengeru.

UCHAWI NA WANAWAKE VYATAJWA KAMA NDIYO CHANZO CHA MAFANIKIO YA DIAMOND


 



MEBAINIKA kwamba msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania,Nassib Abdul Mohamed maarufu kwa jina la (Diamond Platnumz) anatumia nyota za wanawake katika kujipatia umaarufu, habari za ndani zinazomhusu msanii huyo zinadai kwamba amekuwa akitumia nyota za wasichana mbalimbali nchini kujipatia umaarufu.


Taarifa za ndani zilizonaswa na Papaprazi wetu kutoka kwa watu wake wakaribu zinadai kwamba msanii huyo ana amini katika ushirikina na kwamba anamganga wake wa kienyeji anayemtengezea nyota yake, kutokana na nyota za wasichana anao kuwa nao kimapenzi, ambapo anatumia nguo zao za ndani ,leso zao za kujifutia jacho pamoja na picha zao za kiganjani.

Taarifa zaidi zinaeleza kwamba baada ya Diamond kupeleka vitu hivyo kwa mganga wake, ambaye huviingiza katika luninga yake na kupiga ramri yenye nguvu ya kutambua nyota za msichana husika, baada ya hapo Diamond hudumu na msichana huyo mpaka atakapobaaini kwamba amekomba bahati zake zote kisha anatafuta sababu za kumuacha.

"Diamond hafai kabisa ni mshirikina ni mchawi, anaroga watu hususan wanawake,Diamond akikutaka kimapenzi ujue kwamba ukiachana naye lazima ufirisike ama uyumbe na kama ukiwa maarufu lazima umaarufu wako uporomoke, epu fanya utafiti kuanzia kwa wasicha wote aliowahi kutembea nao, tangu alipopata umaarufu mfano, alipokuwa na Wolper kila mtu anajua maisha ya Wopler pamoja na umaarufu wake ulivyokuwa,mtizame Wolper alivyo hivi sasa kama vile kachanganyikiwa"kilisema chanzo chetu na kuongeza:





Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya Tanzania Diamond Platnumz
"Mtizame Jokate wakati akiwa na Diamond maisha yake yalikuwaje, Jokate alikuwa na maisha ya juu lakini tangu alipoachana naye tu mambo yake yakaanza kuyumba, kuliko alivyokuwa awali, mtu mwingine ni Penny ambaye ni mtangazaji wa Luninga ya DTV, yule demu ukimwona hivi sasa huwezi kuamini, kwanza amechanganyikiwa kabisa, mtu mwingine ni Wema Sepetu kila siku ni majanga, inasemekana kwamba nyota ya Wema bado ina nguvu kwa Diamond kuliko wanakwake zake wote, lakini kwa masharti ya mganga wake ni kukaa na kila msichana kwa muda usiozidi miaka miwili ndiyo maana Wema bado anamuota Diamond hadi leo".
 

Hata hivyo Chanzo hicho kilidokeza kwamba, msanii huyo amegonga mwamba kwa Lulu kwa sababu Lulu hivi sasa anadaia kuwa na mtalaam mmoja mkali anayemtengenezea mambo yake, tangu alipo haribu nyota yake kutokana na kifo cha Kanumba na kwamba moja ya masharti yake kwa sasa ni kutokuwa na mahusiano ya kimapenzi na Diamond kwa sababu msanii huyo ndiye aliyempa mikosi tangu alipokuwa na Kanumba.

"Kama utakumbuka vizuri siku ya ugonvi wa Kanumba na Lulu kabla ya kifo kutokea Lulu alikuwa na ahadi ya kukutana na Diamond na akawa na mipango ya kutoroka usiku lakini kwa kuwa jamaa alishtukia mpango wake akawa anajaribu

MAKOSA 11 AMBAYO ZITTO KABWE ANATUHUMIWA NA CHADEMA




MASHITAKA 11 dhidi ya aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe, yamebainisha kuwa kosa kubwa la kiongozi huyo kijana, ni nia yake ya kutaka kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe.
Chanzo chetu cha habari kilichoona mashitaka hayo kabla ya kutumwa kwa washitakiwa, kimebainisha kuwa makosa saba kati ya makosa 11, yanahusu kugombea uenyekiti Taifa, au kumkashifu Mwenyekiti wa Taifa.
“Ukiona hayo mashitaka yenyewe ndugu yangu, yanajirudia rudia na kuzunguka katika kosa moja la nia ya kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa Taifa… angalia kosa la kwanza, kosa la tatu, tano, sita nane na tisa, ni kama vile kuwania uenyekiti ndio kosa kubwa.
“Hata hivyo kwa jinsi mgawanyiko ulivyo ndani ya chama sasa, nakuhakikishia hawa jamaa (Zitto, Dk Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba), watarudishwa katika nyadhifa zao na hakuna atakayeadhibiwa,” alisema mtoa taarifa wetu.
Alinukuu kauli ya Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Profesa Mwesiga Baregu aliyehoji kama makosa wanayotuhumiwa akina Zitto ni makubwa kiasi cha kuyeyusha mema aliyoyafanya katika chama. “Si umesikia akina Baregu wakizungumza? Kwa mashitaka yale nakuhakikishia kitakachofanyika ni kufunika kombe mwanaharamu apite,” alisema mtoa habari wetu.
Kosa la kwanza kwa Zitto, Dk Mkumbo na Mwigamba, wanadaiwa kuvunja Kanuni ya Chama inayokataza kukashifu chama, kiongozi au mwanachama yeyote. Katika maelezo ya kosa hilo, akina Zitto wanadaiwa kumkashifu Mwenyekiti wa Taifa, Mbowe, Katibu Mkuu, Dk Willibrod Slaa na Mjumbe wa Kamati Kuu, Godbless Lema.
Moja ya madai katika mashitaka hayo, ni kilichoandikwa katika Mkakati wa Mabadiliko 2013, kuwa Mbowe amekuwa akinunua vifaa vyote vya chama nje ya nchi kwa bei anayoijua mwenyewe na ambayo haihojiwi popote. Wanadaiwa pia wamemkashifu Dk Slaa kwa kudai ni mdhaifu kwa kumruhusu Mbowe kuingilia shughuli za kiutendaji.
Zitto na wenzake wanadaiwa katika kosa la pili, kutokuwa wawazi na wa kweli wakati wote na kushirikiana na vikundi vya majungu na udanganyifu kinyume na Kanuni za Uendeshaji kipengele cha 10.1 (VIII. 

Katika kosa la tatu, wanadaiwa kutoa tuhuma juu ya viongozi wenzao bila kupitia vikao halali na utaratibu wa ngazi zilizowekwa, kinyume na kanuni ya 10.1 (X).
Katika kosa la nne, akina Zitto wanadaiwa kujihusisha na vikundi vyenye misingi ya ukabila, udini au ukanda ambavyo vina makusudi ya kubaguana ndani ya chama, miongoni mwa jamii, kisiasa au kijamii. Katika kosa hilo wanadaiwa kwenda kinyume na kipengele cha 10.1 (IV), cha Kanuni za Uendeshaji wa Chama.
Akina Zitto katika kosa la tano, wanadaiwa kujihusisha na vitendo vya kuchonganisha na kuzua migogoro kwa viongozi wa chama au wanachama, kinyume na kifungu cha 10.1 (IX), cha Kanuni za Uendeshaji wa Chama.
Katika kosa la sita ambalo mtoa habari wetu alisema ndio kubwa, Zitto na wenzake wanadaiwakutekeleza mpango wa kusudio la kugombea uenyekiti wa Chama Taifa, bila kutangaza kusudio la kutangaza nafasi hiyo.
Hatua hiyo inadaiwa kuwa ni kinyume na kifungu 2.C cha Muongozo wa Kutangaza Kusudio la Kuwania Nafasi ya Uongozi wa Chama, Mabaraza na Serikali wa 2012.
Zitto na wenzake katika kosa la saba, wanadaiwa kutengeneza mitandao ya kuwania uongozi ndani ya chama kwa nia ya kujihakikishia ushindi kinyume na kanuni ya 2 (D), ya Muongozo wa Kuwania Uongozi. 
Katika kosa la nane, Zitto na wenzake wanadaiwa kuwachafua viongozi na wanachama wengine wenye kusudio/nia ya kutaka kugombea nafasi ya uenyekiti kinyume na kifungu 2 (E) cha Muongozo wa Kuwania Uongozi.
Katika kosa hilo, kumewekwa maelezo ya ziada kuwa kosa hilo linaunganishwa na kosa la kwanza ambalo washitakiwa wanadiwa kuwakashifu Mbowe, Dk Slaa na Lema.
Kosa la tisa, akina Zitto wanadaiwa kujihusisha na upinzani dhidi ya chama na makundi ya majungu ya kugonganisha viongozi na wanachama wakati wa uchaguzi wa chama, kinyume na kifungu cha 10.3 (IV), cha Kanuni za Uendeshaji.
Kosa la kumi linamhusu Zitto peke yake, ambapo anaidaiwa kukashifu chama na kiongozi wa chama nje ya Bunge kinyume na kifungu 2 C (B), kikisomwa pamoja na kifungu 3 B cha Kanuni za Mwenendo wa Maadili ya Wabunge.
Katika hilo Zitto kwa kushirikiana na baadhi ya viongozi wa chama yaani Dk Mkumbo na Mwigamba na mtu mwingine ambaye hajajulikana, wanadaiwa kusambaza waraka uitwao Mkakati wa Mabadiliko 2013.
Mkakati huo, unadaiwa kukashifu chama na/ au viongozi wake wakuu kama ilivyoelezwa katika kosa la kwanza, tatu, nne na nane.

Mwisho katika kosa la 11, Zitto na wenzake wanadaiwa kuchochea mgawanyiko ndani ya chama kinyume na kanuni ya 3 F ya Kanuni za Mwenendo wa Maadili ya Bunge.