MASHITAKA 11 dhidi ya aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe, yamebainisha kuwa kosa kubwa la kiongozi huyo kijana, ni nia yake ya kutaka kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe.
Chanzo
chetu cha habari kilichoona mashitaka hayo kabla ya kutumwa kwa
washitakiwa, kimebainisha kuwa makosa saba kati ya makosa 11, yanahusu
kugombea uenyekiti Taifa, au kumkashifu Mwenyekiti wa Taifa.
“Ukiona
hayo mashitaka yenyewe ndugu yangu, yanajirudia rudia na kuzunguka
katika kosa moja la nia ya kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa Taifa…
angalia kosa la kwanza, kosa la tatu, tano, sita nane na tisa, ni kama
vile kuwania uenyekiti ndio kosa kubwa.
“Hata
hivyo kwa jinsi mgawanyiko ulivyo ndani ya chama sasa, nakuhakikishia
hawa jamaa (Zitto, Dk Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba), watarudishwa
katika nyadhifa zao na hakuna atakayeadhibiwa,” alisema mtoa taarifa
wetu.
Alinukuu
kauli ya Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Profesa Mwesiga Baregu
aliyehoji kama makosa wanayotuhumiwa akina Zitto ni makubwa kiasi cha
kuyeyusha mema aliyoyafanya katika chama. “Si umesikia akina Baregu
wakizungumza? Kwa mashitaka yale nakuhakikishia kitakachofanyika ni
kufunika kombe mwanaharamu apite,” alisema mtoa habari wetu.
Kosa la kwanza kwa Zitto, Dk
Mkumbo na Mwigamba, wanadaiwa kuvunja Kanuni ya Chama inayokataza
kukashifu chama, kiongozi au mwanachama yeyote. Katika maelezo ya kosa
hilo, akina Zitto wanadaiwa kumkashifu Mwenyekiti wa Taifa, Mbowe,
Katibu Mkuu, Dk Willibrod Slaa na Mjumbe wa Kamati Kuu, Godbless Lema.
Moja
ya madai katika mashitaka hayo, ni kilichoandikwa katika Mkakati wa
Mabadiliko 2013, kuwa Mbowe amekuwa akinunua vifaa vyote vya chama nje
ya nchi kwa bei anayoijua mwenyewe na ambayo haihojiwi popote. Wanadaiwa
pia wamemkashifu Dk Slaa kwa kudai ni mdhaifu kwa kumruhusu Mbowe
kuingilia shughuli za kiutendaji.
Zitto na wenzake wanadaiwa katika kosa la pili,
kutokuwa wawazi na wa kweli wakati wote na kushirikiana na vikundi vya
majungu na udanganyifu kinyume na Kanuni za Uendeshaji kipengele cha
10.1 (VIII.
Katika kosa la tatu, wanadaiwa kutoa tuhuma juu ya viongozi wenzao bila kupitia vikao halali na utaratibu wa ngazi zilizowekwa, kinyume na kanuni ya 10.1 (X).
Katika kosa la tatu, wanadaiwa kutoa tuhuma juu ya viongozi wenzao bila kupitia vikao halali na utaratibu wa ngazi zilizowekwa, kinyume na kanuni ya 10.1 (X).
Katika kosa la nne,
akina Zitto wanadaiwa kujihusisha na vikundi vyenye misingi ya ukabila,
udini au ukanda ambavyo vina makusudi ya kubaguana ndani ya chama,
miongoni mwa jamii, kisiasa au kijamii. Katika kosa hilo wanadaiwa
kwenda kinyume na kipengele cha 10.1 (IV), cha Kanuni za Uendeshaji wa
Chama.
Akina Zitto katika kosa la tano,
wanadaiwa kujihusisha na vitendo vya kuchonganisha na kuzua migogoro
kwa viongozi wa chama au wanachama, kinyume na kifungu cha 10.1 (IX),
cha Kanuni za Uendeshaji wa Chama.
Katika kosa la sita ambalo mtoa habari wetu alisema ndio kubwa, Zitto na wenzake wanadaiwakutekeleza mpango wa kusudio la kugombea uenyekiti wa Chama Taifa, bila kutangaza kusudio la kutangaza nafasi hiyo.
Hatua
hiyo inadaiwa kuwa ni kinyume na kifungu 2.C cha Muongozo wa Kutangaza
Kusudio la Kuwania Nafasi ya Uongozi wa Chama, Mabaraza na Serikali wa
2012.
Zitto na wenzake katika kosa la saba,
wanadaiwa kutengeneza mitandao ya kuwania uongozi ndani ya chama kwa
nia ya kujihakikishia ushindi kinyume na kanuni ya 2 (D), ya Muongozo wa
Kuwania Uongozi.
Katika kosa la nane,
Zitto na wenzake wanadaiwa kuwachafua viongozi na wanachama wengine
wenye kusudio/nia ya kutaka kugombea nafasi ya uenyekiti kinyume na
kifungu 2 (E) cha Muongozo wa Kuwania Uongozi.
Katika
kosa hilo, kumewekwa maelezo ya ziada kuwa kosa hilo linaunganishwa na
kosa la kwanza ambalo washitakiwa wanadiwa kuwakashifu Mbowe, Dk Slaa na
Lema.
Kosa la tisa,
akina Zitto wanadaiwa kujihusisha na upinzani dhidi ya chama na makundi
ya majungu ya kugonganisha viongozi na wanachama wakati wa uchaguzi wa
chama, kinyume na kifungu cha 10.3 (IV), cha Kanuni za Uendeshaji.
Kosa la kumi linamhusu Zitto peke yake,
ambapo anaidaiwa kukashifu chama na kiongozi wa chama nje ya Bunge
kinyume na kifungu 2 C (B), kikisomwa pamoja na kifungu 3 B cha Kanuni
za Mwenendo wa Maadili ya Wabunge.
Katika
hilo Zitto kwa kushirikiana na baadhi ya viongozi wa chama yaani Dk
Mkumbo na Mwigamba na mtu mwingine ambaye hajajulikana, wanadaiwa
kusambaza waraka uitwao Mkakati wa Mabadiliko 2013.
Mwisho katika kosa la 11, Zitto na wenzake wanadaiwa kuchochea mgawanyiko ndani ya chama kinyume na kanuni ya 3 F ya Kanuni za Mwenendo wa Maadili ya Bunge.
No comments:
Post a Comment