Malkia wa Mipasho Afrika Mashariki na Kati, Khadija Omary Kopa amevamiwa na vijana wahuni wakitaka kumfanyia fujo kwa madai ya kukatiza mitaani akiwa ameongozana na ‘mwaume aliyekuwa amevaa nguo za kike’.
Tukio
hilo lilijiri maeneo ya Kariakoo, Dar wiki iliyopita ambapo vijana hao
walianza kwa kuzomea wakitaka kumshika mwanaume huyo waliyedai alikuwa
amevaa nguo za jinsia ya kike.
Alichokifanya
Khadija ni kuingia kwenye gari na kumwambia dereva aondoke haraka
kukwepa kufanyiwa vurugu huku mwanaume huyo naye akiungana na malkia
huyo kuondoka eneo hilo.
Wakizungumza na GPL, vijana hao walidai kuwa Khadija alijiabisha kwa kuongozana na mwanaume huyo.
Khadija
aliiambia GPL kuwa alishangazwa na tukio hilo lililomkuta na kusema
kuwa mwanaume aliyeongozana naye ni mwimbaji mwenzake ambaye pia ni
shemeji yake.
Alifunguka: “Hivi kuwa mwimba taarabu wa kiume ndiyo ushoga jamani? Au kuvaa kaptura ya kitenge ni tatizo? Mbona alikuwa amevaa mavazi mazuri tu ya kiume?”
Khadija
alisema kuwa amewazoea mashabiki wake wa Kariakoo kwani huwa wakiwaona
mastaa huwa na tabia hiyo na ndiyo maana walianza uzushi huku wakisema
kuwa waimba taarabu wote ni wanawake, kitu ambacho si kweli.
No comments:
Post a Comment