MAHAKAMA ya Rufani leo inatarajia kutoa
uamuzi wa ama kulikubali au kulikataa ombi la marejeo lililowasilishwa
na mwanamuziki wa dansi nchini, Nguza Vicking ‘Babu Seya’ na mwanae,
Papi Kocha ‘Mtoto wa Mfalme’, ambao waliomba mahakama hiyo ifanyie
marejeo hukumu ya kifungo cha maisha iliyoitoa Februari 2010, kwa kuwa
ina dosari za kisheria na kuwaachia huru.
Kwa mujibu wa hati ya wito wa mahakama
iliyotolewa kwa mawakili wa pande zote mbili, mahakama imemtaka Babu
Seya na mwanae pamoja na mawakili wa pande zote kufika leo mahakamani
ili wapokee uamuzi wa maombi hayo.
Oktoba 30 mwaka huu, jopo la majaji
watatu wakiongozwa na Jaji Nataria Kimaro, Salum Massati na Mbarouk
Mbarouk, walisikiliza ombi hilo lililowasilishwa mahakamani hapo na
wakili wa waomba rufani, Mabere Marando.
Wakili Marando alidai kwa mujibu wa
kanuni ya 66 ya Mahakama ya Rufaa ya mwaka 2009 inatoa mamlaka kwa
Mahakama ya Rufaa kufanya mapitio ya hukumu inazozitoa, hivyo wateja
wake wamewasilisha ombi hilo kwa sababu wanaamini mahakama ilikosea
kisheria katika hukumu yake Februari 2010.
“Waheshimiwa majaji, kwa sababu jopo
lenu katika hukumu yake lilikiri wazi wazi kuwa Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu ilikosea kurekodi ushahidi wa watoto waliodai walitendewa
vibaya na waomba rufaa (Babu Seya na Papii) na sheria za nchi zinasema
endapo mahakama itabaini kuwa mahakama ya chini ilikiuka taratibu za
kurekodi ushahidi wa watoto wadogo, basi ushahidi ule wa watoto wadogo
uliotumika katika mahakama ya chini kuwatia hatiani washitakiwa unafutwa
na waomba rufaa au washitakiwa wanaachiwa.
“Nafahamu ni kazi ngumu kuwashawishi
nyie majaji kubadili uamuzi wenu mlioutoa katika hukumu ya Februari
2010, ambapo uliwatia hatiani wateja wangu, ila kwa utetezi huo wa
kisheria niliouainisha unaonyesha katika hukumu yenu mlikubaliana na
hoja yangu kuwa Mahakama ya Kisutu ilikosea kurekodi ushahidi wa watoto
wadogo, naamini mtatumia busara zenu na kufuata sheria na leo naiomba
mahakama iwaachie huru wateja wangu,” alidai Marando.
Mawakili wa upande wa mjibu maombi
(DPP), Angaza Mwipopo, Jackson Mlati, Imaculata Banzi na Joseph Pande,
waliomba mahakama itupilie mbali ombi hilo, kwa kuwa sababu zote
alizozitoa alizieleza wakati wa usikilizwaji wa rufaa na ziliamuliwa
katika hukumu iliyotolewa na mahakama hiyo Februari mwaka 2010.
Jackson alidai kama Marando anaona
hukumu ya mwaka 2010 ilikuwa na dosari, angeomba mahakama hiyo impangie
jopo la majaji watano wa kusikiliza ombi na si ombi lake kusikilizwa na
jopo la maji watatu wale wale waliotoa hukumu hiyo ambayo anadai ina
dosari.
Thursday, 21 November 2013
Wednesday, 20 November 2013
KAPUYA MAMBO SI SHWARI, HALI NI TETE.
Azidi kumtishia kifo binti anayedaiwa kumbaka
Fedha alizomtumia hadharani, amshambulia Sitta
KASHFA ya kumbaka na kutishia kumuua msichana wa miaka
16, inayomkabili Mbunge wa Urambo Magharibi, Profesa Juma Kapuya (CCM), imeibua
mambo mapya. Wakati serikali inakusudia kufungua mashtaka mawili ya
kubaka na kutishia kuua dhidi ya Profesa Kapuya, waziri huyo wa zamani bila
woga ameendelea kutuma ujumbe mfupi kupitia simu yake ya mkononi kwa binti huyo
na kusisitiza kuwa lazima amuue. Mbali na kutishia kumuua binti huyo na ndugu yake na
mtu mwingine yeyote atakayejitokeza kumsaidia, gazeti hili limenasa baadhi ya
mawasilino ya simu za ujumbe mfupi wa kuhamisha fedha kutoka kwa Profesa Kapuya
kwenda binti huyo ambaye juzi kupitia baadhi ya vyombo vya habari Kapuya
alikana kumfahamu na kwamba hajawahi kukutana naye.
Uchunguzi wetu umebaini kuwa mara baada ya taarifa ya
gazeti hili jana kuandika mwendelezo wa kashfa hiyo, huku likimkariri Waziri wa
Ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Samuel Sitta, akihoji ukimya
wa serikali katika kashfa hiyo, Profesa Kapuya alituma ujumbe mwingine wa
kutishia kumuua binti huyo. Ujumbe huo kutoka simu namba 0784993930 inayomilikiwa
na Kapuya kwenda kwa namba inayomilikiwa na binti huyo, unasomeka hivi: “Ni lazima nitakuua wewe na ndugu yako na atakaetaka
kuwasaidia, huyo Sita asijiingize kwenu, yaani nitakuua tena sijui leo
mtalala wapi! We unadhani nani atakayenifunga? Ndo nishakupa ukimwi, sasa
nakutaka uache mara moja kuongea na mtu, nitakuwinda popote tuone!” inasomeka
sehemu ya ujumbe huo unaodaiwa kutoka kwa Kapuya. Ujumbe huo wa vitisho vya kuuawa, unafanana na ule
uliokaririwa na gazeti hili ambao pia unadaiwa kutoka kwa Profesa Kapuya kwenda
kwa binti huyo anayedai kubakwa na Kapuya.
Sehemu ya ujumbe uliopita unasomeka: “Mkiuawa itakuwa
vizuri….itawapunguzia gharama za kuishi; usitake kugombana na serikali mtoto
mdogo kama wewe. “Sisi ndiyo wenye nchi yetu, mwenye hilo gazeti ni
Mbowe sasa mwambieni nyumba ya kuishi si mmemuingizia hela leo? Mnatumika tu
bure watu wanaingiza hela nyingi, ila mmenitibua lazima niwaue wiki hii
haitaisha; nitapiga kambi kote. Jana si walikuficha? Tuone kama utalindwa
milele; maana washatengeneza hela lazima mvae sanda tu hilo sio ombi ni
wajibu wenu. Mnajitia na nyie Mafia watoto siyo!!? “Watoto wetu wanauza unga nani anawakamata? Nani
atapingana nasi!?” Katika kuthibitisha kwamba Kapuya amekuwa na
mawasiliano na binti huyo na kwamba anamjua tofauti na anavyodai kuwa hamjui,
gazeti hili limenasa mawasiliano ya kutumiana fedha kutoka kwa Kapuya kwenda
kwa binti huyo.
Baadhi ya mawasiliano hayo ni pamoja na yale
yaliyofanyika Agosti 31 mwaka huu kupitia simu ya Kapuya ambapo alituma sh
300,000 kwenda kwa binti huyo kama sehemu ya makubaliano ya kutuma pesa kila
mwezi kwa ajili ya matunzo.
Mawasiliano hayo ni kama ifuatavyo:
R93NY448 Imethibitishwa
Umepokea Tsh505,000
kutoka kwa JUMA KAPUYA
Tarehe 21/6/13 saa 11:07 AM
Salio lako la M-PESA ni Tsh 505,000
U26UG365. Imethibitishwa Umepokea Tsh 300,000
kutoka kwa JUMA KAPUYA
Tarehe 31/8/13 saa 3:28 PM
Salio lako la M-PESA ni Tsh 300,000
V04EU470 Imethibitishwa Umepokea Tsh 400,000
kutoka kwa JUMA KAPUYA
Tarehe 24/9/13 saa 2:38 PM
Salio lako la M-PESA ni Tsh 400,040
Tayari serikali kupitia jeshi lake la polisi, limesema
linakusudia kufungua mashtaka mawili dhidi ya mbunge huyo. Mashtaka yanayotajwa kumkabili mbunge huyo ambaye
amepata kuwa waziri katika awamu tofauti za uongozi kuwa ni pamoja na ya
ubakaji na kutishia kuua. Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam,
Suleiman Kova, aliliambia gazeti hili juzi kuwa jeshi hilo halitakuwa na sababu
ya kumuacha mbunge huyo kuendelea kutamba mitaani huku akituma ujumbe wa
vitisho kwa binti wa miaka 16 anayedaiwa kumbaka. Wakati Kamanda Kova akisema hawatakuwa na ajizi na
tuhuma za kubaka na kutishia kuua zinazomkabili Profesa Kapuya, Ikulu ya Rais
Jakaya Kikwete imekerwa na kauli ya mbunge huyo wa Urambo Magharibi kuwa
serikali haiwezi kumfanya jambo lolote.
Pia CCM ambayo baadhi ya maafisa wake walijitahidi
kumtoa Kapuya kwenye kashfa hiyo, kimeamua kumtosa mbunge huyo aliyewahi kuongoza
Wizara ya Elimu na Ulinzi kwa nyakati tofauti baada ya kumtaka aache
kukihusisha chama na kashfa yake ya kubaka. Mbunge huyo anadaiwa kumbaka binti huyo kwenye
hoteli moja ya kitalii iliyoko jijini Dar es Salaam mwaka 2011, na kurudia tena
kitendo ndani ya ofisi yake katika Jengo la Biashara Complex lililoko
Mwananyamala Juni 3, 2012 alipoitwa kwenda kuchukua ada kwa mara ya pili. Kutokana na mfululizo wa habari hiyo ambayo imekuwa
ikichapishwa na gazeti hili, Profesa Kapuya kupitia kwa wakili wake Yasin
Memba, ametishia kuliburuza gazeti hili mahakamani endapo halitamwomba msamaha
ndani ya siku saba. Mbali na kutishia kulipeleka gazeti hili na baadhi ya mitandao
ya kijamii mahakamani pia Profesa Kapuya alikana kumfahamu binti anayedai
alibakwa huku akikanusha kumiliki simu namba 0784993930 ambayo imekuwa
ikitumiwa kuwasiliana naye ikiwemo kumtumia ujumbe mfupi wa maneno (sms) wa vitisho
MCHUNGAJI KANISA LA PENTEKOSTE HOLLINESS ADAIWA KUBAKA WANAFUNZI
Nyumba anayoishi Mchungaji Mwaikambo ikiwa imepigwa kufuri huku mwenyewe akiwa ''amelala mbele!! baada ya kufanya unyama wake |
MCHUNGAJI wa
kanisa la Pentekostal aliyefahamika kwa jina la Bryson Mwaikambo(55) anadaiwa
kuwabaka na kuwaambukiza ugonjwa wa zinaa wanafunzi wawili wa kike wanaosoma
katika shule ya msingi ya Maendeleo wa
kata ya Nsalala wilaya ya Mbeya vijiji mkoani Mbeya.
Wanafunzi
hao (majina yanahifadhiwa) wenye umri kati ya miaka 11 na 13 wanaosoma darasa
la nne na darasa la sita walifanyiwa unyama huo kuanzia mwaka 2012 ambapo
alianza kujenga mazoea na watoto hao wadogo kwa kuwapa peremende pamoja
na fedha.
Imeelezwa
kuwa mchungaji huyo ambaye anaendesha ibada katika kanisa hilo dogo lenye
waumini wachache lililopo kitongoji cha kanani kijiji cha ‘Tunduma Road’alikuwa
akiwavizia watoto hao kwa muda mrefu kila walipokuwa wanapita kuelekea shuleni.
Katika
jitihada zake za kuwanasa watoto hao wa kike alimdanganya mmoja wa wazazi wa
watoto aliyefahamika kwa jina la Bw.John Mussa(38) na kumuomba binti yake awe
anamsaidia kazi za nyumbani nyakati za jioni kutokana na kuwa mke wa mchungaji kuwepo safarini.
Kwa kuamini kuwa
mchungaji huyo alikuwa ni mtumishi wa Mungu, Bw. Mussa aliridhia mwanaye aende
kuishi na Mtumishi huyo wa Mungu bila kujua hatima ya kile ambacho kimemtokea
binti yake kwa sasa.
Kwa mujibu
wa maelezo kutoka kwa wazazi na walimu wa shule ya Msingi Maendeleo ni kwamba
mabinti hao walikuwa wakifanya ngono na mchungaji huyo kwa zamu na kwamba
walianza kujua tatizo hilo baada ya kutokea mgongano baina ya wasichana hao
wawili .
‘’Tumejua
tukio hili baada ya kutokea ugomvi baina yao wa kugombania maji na hivyo kuanza
kurushiana maneno, mmoja wa watoto hao alikuja ofisini kushitaki kuhusu ugomvi
wao ndipo mmoja akasema kuwa mwenzie anatembea na Mchungaji Mwaikambo’’alisema
Mwalimu mkuu msaidizi Bi. Lucy Kamongile.
Alifafanua
kuwa, baada ya tukio hilo walimu kwa pamoja walilazimika kuwauliza zaidi ndipo
walipoanza kujieleza kuwa wamekuwa wakilala na Mchungaji huyo kwa muda mrefu na
kwamba mwanzo alikuwa akiwapa peremende na baadaye akaanza kuwapa fedha.
Alisema kuwa
walilazimika kuitisha kikao cha dharura baina ya wazazi wa watoto hao na walimu
ambapo walieleza tukio zima la kuingiliwa kimwili na Mchungaji huyo tangu mwaka
jana.
‘’Nililazimika
kuwaita wazazi pamoja na wanafunzi tulikaa katika ofisi ya walimu, watoto
walieleza tukio zima mbele ya wazazi wao juu ya vitendo walivyokuwa wakifanyiwa
na Mchungaji huyo.
Alisema kuwa
mara baada ya kikao hicho cha wazazi waliwapeleka watoto hao katika kituo
kidogo cha Polisi kilichopo katika
mji mdogo wa Mbalizi ambako walipewa
Fomu ya Polisi Na. 3,(PF3) kwa ajili ya kuepelekwa hospitali ili wapatiwe
matibabu.
Mwalimu
Kamongile ambaye alikuwa na walimu wenzie katika ofisi ya Mwalimu mkuu wa shule
hiyo wakati akitoa taarifa hizi mbele ya Ripota Wetu kuwa
wanafunzi hao walipatiwa matibabu katika hospitali Teule ya Ifisi ambapo kwa
mujibu wa taarifa za mganga aliyewachunguza
watoto hao ni kwamba mbali na kufanyiwa ubakaji wote wawili walikuwa
wameambukizwa ugonjwa wa zinaa wa kaswende.
‘’Tukio hili
limetufedhehesha sana tulikuwa tunatafakari wapi tutaenda,tunaomba kilio chetu
kifike chama cha Waandishi wa Habari wanawake TAMWA kitoe taarifa hizi kwa
undani waone namna ambavyo jamii ya pembezoni inavyokosa msaada na haki za
kisheria,’’alisema Mwalimu Kamongile.
Mwalimu huyo
alisema kuwa wanatambua juhudi za chama cha waandishi wa habari wanawake TAMWA
ambazo wamekuwa wakizifanya hivyo wanaimani chama hicho kikisikia suala
kitalifanyia kazi kwa kina zaidi kuisaidia jamii ambayo aina mahali pa kusemea.
Kwa upande
wa watoto hao ambao walikuwa wakizungumza kwa kupokezana juu ya kadhia
iliyowakuta walisema kuwa Mchungaji huyo alianza kufanya nao vitendo vya ngono
tangu mwaka 2012 kwa kuwadanganya kwa fedha na peremende na baadaye wakazoea
kwenda kwa Mchungaji huyo mara kwa mara.
Mwanafunzi
anayesoma darasa la nne alisema kuwa alianza kutembea na Mchungaji huyo wakati
akimpitia mwenzie aliyekuwa akiishi nyumbani kwa mchungaji ambapo siku hiyo
alimuita chumbani kwake na kumlazimisha kulala kitandani ambapo alianza
kumuingiza vidole katika sehemu zake za siri.
“Siku ya
kwanza nililia sana wakati mwenzangu yupo pembeni akishuhudia mchungaji
akinifanya na ndipo mwenzangu alisema jikaze rafiki yangu”alisema Mtoto huyo.
Alisema kuwa
mara baada ya kumuingiza vidole alivua nguo zake na kumbaka huku akilia wakati
msichana mwenzie (alimtaja jina) akiwa amekaa pembeni ya kitanda akimweleza
kuwa aache kulia kwa kuwa baada ya kumaliza watapewa fedha za kutumia shuleni.
Binti huyo
aliendelea kusema kuwa alipata maumivu makali wakati Mchungaji huyo akitekeleza
ubakaji wake ambapo mara baada ya kumaliza` alimpa sh.500 na peremende na
baadaye alimwita mwenzie kitandani na kufanya naye ngono huku akishuhudia kwa
macho yake.
Alisema mara
baada ya kumaliza kufanya na mwenzie Mchungaji Mwaikambo aliwaonya wasiseme kwa
wazazi wao kisha akawapa fedha na kuwaonya wasiseme jambo hilo kwa mtu yoyote.
Akizungumza
sababu za kutosema kwa walimu au wazazi wake binti mwingine anayesoma darasa la
sita alisema kuwa Mchungaji huyo aliwatishia kuwachinja na kuwafukia kwenye
shimo iwapo atasikia wamesema tukio hilo kwa wazazi ama walimu wao.
Alisema kuwa
Mchungaji aliwaomba wazazi wake ili aende kuishi nyumbani kwake kumsaidia kazi
kutokana na mama Mchungaji ‘’Mke wa Mchungaji’’ kuwa safarini na kwamba katika
siku hizo ndipo Mchungaji huyo alipoanza kulala naye mahusiano taratibu.
Alisema kwa
siku za mwanzo alikuwa akimuingiza vidole katika sehemu zake za siri na baadaye
akaanza kumbaka ambapo alijisikia maumivu makali lakini alimbembeleza kwa kumpa
sh.1000 ambayo alikuwa akitumia shuleni kwa kununua chipsi.
‘’Alikuwa
akiniingiza vidole huku chini(akionyesha sehemu za siri) akanibaka, sikuweza
kumwambia baba niliogopa atanichinja..mwenzangu alipokuwa anakuja kunipitia
kwenda shuleni naye alianza kumuingiza vidole akambaka!!, alilia sana,
nikamwambia asilie atatupa hela,’’alisema.
Alisema kuwa
wamebakwa na Mchungaji huyo zaidi ya mara nne na kila alipokuwa akiwabaka
alikuwa anawapa hela za kutumia shuleni.
Kwa upande
wazazi wa watoto hao Bw.Suveli Harrison na Bw. John Mussa walikiri kuitwa
shuleni na kupata taarifa za kubakwa kwa watoto wao walipoitwa shuleni ambapo
watoto walijieleza walichokuwa wakifanyiwa na Mchungaji Mwaikambo mbele ya
walimu.
‘’Jambo hili
lilitushitua sana, machozi yalitulenga, hatukutegemea kusikia Mchungaji anaweza
kuwabaka watoto ambao ni sawa na wajukuu zake, tulienda polisi walitupa
karatasi tukaenda Hospitali ya Ifisi, watoto walikutwa na maambukizi ya ugonjwa
wa zinaa,’’alisema Bw. John Mussa.
Alisema kuwa
yeye aliridhia mwanaye kuishi na Mchungaji huyo baada ya kuombwa kutokana na
mchungaji huyo kuishi na mtoto mdogo wakati mkewe akiwa safarini.
Bw. Mussa
alisema kuwa hakujua kuwa kama kuna siku mwanaye atadhurika kwa kufanyiwa
kitendo cha unyanyasaji na ukatili wa kijinsia kama walivyofanyiwa watoto hao
na kwamba hata hivyo hadi sasa hakuna jitihada zozote za jeshi la polisi
zilizofanikisha kumnasa Mchungaji huyo.
Alisema kuwa
kwa sasa watoto hao wamekuwa wakitishiwa na Mchungaji kutokana na kufahamika
kuwa yeye aliwabaka na kwamba anaomba msaada wa kisheria kusimamia haki ili
sheria iifuatwe dhidi ya mtuhumiwa wa ubakaji.
Naye mzazi
mwingine Bw.Suvile Harrison alisema kuwa hakujua chochote juu ya vitendo
alivyofanyiwa mwanaye na Mchungaji huyo na
kwamba alifahamu tukio hilo baada ya kuitwa shuleni ambako walimu
waliwaita watoto wao na kueleza tukio zima walilokuwa wakifanyiwa na Mchungaji.
Alisema kuwa
hakubaini mabadiliko yoyote kwa mwanaye juu ya vitendo alivyofanyiwa na wala
hajawahi kuhisi lolote hadi hapo alipoitwa shuleni na walimu.
Baada ya
taarifa hizo waandishi wa habari wa gazeti hili walifunga safari hadi katika
nyumba ambayo inasadikiwa kuwa ndipo anapoishi Mchungaji huyo na kukuta mlango
ukiwa umefungwa lakini alijitokeza jamaa ambaye alijitambulisha kuwa ni mmiliki
wa nyumba hiyo Bw. Zacharia Gambi.
Bw.Gambi
alisema kuwa anamfahamu mpangaji wake kwa jina moja la Mchungaji Mwaikambo na
kwamba mbali ya kuwa ni Mchungaji wa Kanisa la Kipentekoste ni Balozi wa nyumba
kumi wa mtaa wa Kanani.
Bw.Gambi
alisema kuwa Mchungaji huyo hajaonekana muda mrefu na kwamba mkewe amekuwa na desturi
ya kuondoka alfajiri kuelekea shambani na kurudi usiku.
Kadhalika
imeelezwa na baadhi ya watu ambao hawakupenda kutajwa majina yao gazetini
kuwa kitendo cha Mchungaji huyo kuwabaka
mabinti wadogo kimetokana na imani za nguvu za giza kwamba kwa kufanya hivyo
kitamuongezea waumini katika kanisa lake dogo lililopo katika mtaa wa Kanani.
Mama mzazi
wa mmoja wa watoto waliobakwa aliyejitambulisha kwa jina la Jane John(35)
alisema kuwa awali yeye alikuwa ni mmoja wa waumini katika kanisa hilo lakini
baadaye walihamia kanisa jingine baada ya kuona mienendo ya mchungaji huyo
kutofanana na kazi ya huduma za kiroho.
Alisema
waumini wengi wamehama katika kanisa hilo wakiwemo watoto wake wakubwa wa kike
ambao walieleza waziwazi tabia ya ukware ya Mchungaji huyo ya kuwafuatilia
mabinti wadogo kwa ajili ya kufanya nao vitendo vya ngono.
Diwani wa
Kata ya Nsalala iliyopo Mbeya vijijini Bw.Mashauri Mbembela alipozungumza na
waandishi wa gazeti hili alisema kuwa anashangazwa tukio hilo kutoshughulikiwa
kwa kipindi chote huku taarifa zikiwa zimefikishwa kituo cha polisi.
Alisema kuwa
tukio hilo ni la unyanyasaji ambalo lilipaswa kushughulikiwa kwa nguvu zote na
kwamba kuna haja ya kuweka sheria ngumu itakayokomesha vitendo vya ubakaji kwa
watoto wa kike.
Bw.Mbembela
alisema kuwa ili kukomesha tabia za ubakaji, itungwe sheria ya kuwahasi
wabakaji badala ya kuwafunga jela miaka 30
ambako wanaenda kula chakula kinachotokana na kodi za wananchi.
‘’Wabakaji
wanafungwa jela, wakimaliza vifungo vyao hurejea uraiani ambako wanaweza
kuendeleza vitendo hivyo, njia pekee ya kukomesha ubakaji ni kuwahasi, wakirudi
uraiani wataendeleza kujenga Taifa,’’alisema Bw. Mbembela.
Ripota wetu alifanya jitihada za kutafuta namba za simu za mchungaji huyo ambaye mara
baada ya kupokea na kuulizwa juu ya tuhuma hizo alikanusha na kusema kuwa huu
ni uzushi na uongo uliolenga kumpaka matope ili kuchafua huduma zake anazotoa
kwa waumini .
Alidai kuwa
kanisa lake la Pentecostal Holiness lenye
jumla waumini nane linatoa huduma za uhakika kijijini hapo hivyo baadhi
ya wafuasi wa shetani wanalipiga vita ili lisiendelee kukua ili kuwafikia
wanakondoo wengi.
“Wananipakazia
tu unaweza kuingiwa na ibilisi na hivi ulivyonipigia nafikiria kuchukua maamuzi
magumu na mwili wangu hamtauona kamwe bora uliwe na ndege na wanyama wa porini niende jehanamu kuliko kuchafuliwa
huku”alisema Mchungaji huyo.
Alisema kuwa
tuhuma hizo zimeelekezwa kwake baada ya kumdai fedha mmoja wa wazazi wa watoto
hao ambaye alikuwa akifanya kibarua cha kujenga ofisi ya kata ambapo mama huyo
alimkopesha fedha sh.5000 na alipoanza kudai ndipo akaanza kuzushiwa tuhuma
hizo.
Hata hivyo
alisema Jumanne iliyopita alifuatwa na
askari mgambo sita wenye virungu ambao walitaka kumkamata lakini kwa nguvu za
yesu walishindwa na kuondoka zao.
“Mimi naishi
kwa nguvu za Yesu mtu yeyote mwenye nia mbaya na mimi hawezi kunipata nataka
niwe kama mfalme aliyejitoa mhanga nijiue mwili wangu usionekane
duniani”alisisitiza na kukata simu.
Kamanda wa
polisi mkoa wa Mbeya Bw.Diwani Athumani alisema kuwa amepata taarifa hizo za
ubakaji ambapo amemuagiza Ofisa Upelelezi wa Mkoa Bw.Mtatiro Nyamuhanga ambaye
atalifuatilia kwa karibu tukio hilo na kwamba hata hivyo mtuhumiwa bado
hajatiwa mbaroni.
MAREKANI YAITAJA TANZANIA KUWA KINARA WA BIASHARA YA KUSAFIRISHA BINADAMU...
Dar
es Salaam. Marekani imetoa ripoti inayozungumzia usafirishaji wa
binadamu ya mwaka 2013, huku ikiitaja Tanzania kuwa kinara wa kunyanyasa
wasichana, kuwatumikisha katika ngono na usafirishaji wa binadamu.
Tanzania
imetajwa kuwa ni miongoni mwa nchi 44 ambazo zinajaribu kupambana na
biashara hiyo, lakini hali inazidi kuwa mbaya zaidi
Ripoti hiyo iliyotolewa na idara ya
nchi hiyo inayohusika na diplomasia (US Department of State, Diplomacy
in Action), pia inaitaja Tanzania kuwa ni kitovu cha njia ya kusafirisha
wanawake, watoto na wanaume ambao hutumikishwa kwenye kazi za
mashambani na biashara ya ngono.
Ripoti hiyo iliyozinduliwa Julai mwaka
huu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Seneta John Kerry inaweka
bayana kwamba biashara ya usafirishaji wa binadamu hufanywa na baadhi ya
ndugu na marafiki ambao hutoa ahadi kwa wahusika kwamba wanakwenda
kuwasomesha au kuwatafutia ajira nzuri mijini.
“Unyonyaji
wa wasichana wadogo na utumikishaji majumbani ndilo tatizo
linaloongoza, ingawa kesi za watoto kusafirishwa kwa ajili ya biashara
ya ngono katika mpaka wa Tanzania na Kenya zinaongezeka. Pia, wasichana
wananyonywa kwenye maeneo ya utalii,” inasema sehemu ya ripoti hiyo.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, watoto
kutoka Burundi na Kenya, watu wazima kutoka Bangladesh, Nepal, Yemen na
India wanatumikishwa kufanya kazi kwenye sekta za kilimo, madini na
majumbani nchini Tanzania.
“Baadhi
ya raia kutoka nchi jirani huingia Tanzania kwa hiari yao, lakini
hulazimishwa kufanya kazi majumbani kabla ya kupelekwa kutumikishwa
kwenye biashara ya ngono Afrika Kusini, Ulaya na Mashariki ya Kati,” inaeleza.
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria,
Angela Kairuki alimtaka mwandishi kumtumia ripoti hiyo kwa njia ya
baruapepe ili aweze kuisoma na kuitolea maelezo.
Alipotafutwa siku ya pili, alisema kuwa
ameipokea na kuikabidhi ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka (DPP) ili
ifanyiwe kazi na baadaye kutoa majibu.
“Ripoti niliipata nikaikabidhi ofisi ya
DPP kwa kuwa wao ndio wanaoweza kuitolea maelezo baada ya kuisoma.
Maoni yangu lazima yawe ya kitaalamu siwezi kusema bila kupata taarifa
kutoka kwao,” alisema.
Lawama kwa Serikali
Ripoti hiyo inaitupia lawama Tanzania
kwa kutokuwa na sheria thabiti za kupambana na biashara haramu ya
kusafirisha binadamu, huku ikitolea mfano namna ilivyoshindwa kuwasaidia
raia wake waliokuwa wakinyanyaswa nje ya nchi.
“Kamati ya Serikali ya kupambana na
usafirishaji binadamu, haijachukua hatua za kutosha katika kutekeleza
mpango mkakati wa kupambana na vitendo hivyo,” inaeleza na kuongeza:
“Serikali
imeshindwa kutenga fedha kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa
usafirishaji wa binadamu kama ambavyo inaelekezwa kwenye sheria ya
kudhibiti biashara hiyo ya 2008.”
Taarifa hiyo inaitaka Tanzania kuongeza
nguvu katika kutekeleza sheria ya kudhibiti biashara ya kusafirisha
binadamu ya 2008 kwa kuwakamata na kuwashtaki wahusika wote, lakini
ikaikosoa kwa kusema inatoa adhabu ndogo kwa mtu anayebainika kufanya
makosa, ikiwa ni pamoja na kumhukumu kwenda jela miaka 10, kulipa faini
au vyote viwili kwa pamoja.
“Sheria hiyo haifanani na nyingine
kama za mtu anayepatikana na kosa la kubaka au kufanya kosa jingine la
jinai. Mamlaka imesema ina kesi nne inazozichunguza, saba zipo
mahakamani toka mwaka jana, zikiwepo mbili mpya,” inasema ripoti.
Pia, Serikali ya Tanzania imelaumiwa
kwa kushindwa kuripoti maendeleo ya uchunguzi wa maofisa wake
waliotuhumiwa kujihusisha na biashara ya usafirishaji binadamu.
LHRC na TGNP
Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki
za Binadamu (LHRC), Dk Hellen Kijo-Bisimba alisema tatizo la
usafirishaji wa binadamu pia linachangiwa na wasichana kuwa na tamaa ya
maisha mazuri, hivyo kukubali ahadi ambazo hupewa kwamba wanapelekwa
kusoma, wasifahamu wanarubuniwa.
“Wengi wanatamani kwenda ‘majuu’
wakidhani watapata elimu, lakini baadaye wanaingizwa kwenye vitendo
vinavyowafedhehesha na kuwafanya wakate tamaa kabisa,” alisema.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa
Jinsia Tanzania (TGNP), Usu Mallya alisema katika siku za karibuni
kumekuwa na ongezeko kubwa la vitendo vya unyanyasaji dhidi ya wasichana
waliochukuliwa vijijini kwenda mijini kufanya kazi.
Alisema pamoja na tatizo hilo
kuongezeka hapa nchini, hakuna tafiti za kutosha ambazo zimefanywa na
wadau mbalimbali kuonyesha madhara yaliyopatikana hadi sasa.
“Katika siku za usoni kumekuwa na
ongezeko kubwa la vitendo vya kunyimwa chakula, kupigwa na kufukuzwa
kazi huku wasichana wengine wakitumika kwenye biashara ya ngono,” alisema na kuongeza:
“Ripoti hii isiishie kwenye makabrasha bali ifanyiwe kazi ili jamii yote ijue kuwa hili ni tatizo.”
Ripoti hiyo inabainisha kuwa watu
47,000 pekee ndio walioweza kuokolewa mwaka jana kutoka kwenye mazingira
ya utumikishwaji kati ya milioni 27 waliopo katika hali hiyo duniani.
Friday, 15 November 2013
MBUNGE WA CCM( PROFESA JUMA KAPUYA )ATISHIA KUJIUA BAADA YA SIRI ZAKE ZA KUMBAKA MSICHANA NA KUMWAMBUKIZA UKIMWI KUVUJA....
MBUNGE wa Urambo Magharibi, Profesa Juma Kapuya (CCM), ameingia katika matata. Katika kujaribu kudhibiti mtoto wa shule ambaye anadai alibakwa naye na kuambukiwa virusi vya ukimwi, mbunge huyo ametoa vitisho vya kuua mtoto huyo na kujiua kama njia ya kuepuka dhahama inayoelekea kumkabili.
Siku moja baada
ya gazeti la Tanzania Daima kuripoti habari za mbunge mmoja (bila
kumtaja jina), jana asubuhi Profesa Kapuya ameibuka na kumtisha
mwanafunzi huyo mwenye miaka 16 anayesoma Shule ya Sekondari Turiani
iliyoko Magomeni jijini Dar es Salaam.
Baada ya kujua
kuwa mtoto huyo ndiye alitoa habari za masahibu hayo, ambayo mbunge
hakutaka yajulikane, alimpigia simu mtoto huyo, na baadaye kutuma meseji
kadhaa za vitisho.
Jana Tanzania Daima ilishuhudia baadhi ya meseji za simu zilizotumwa na Profesa Kapuya kwenda kwa mtoto huyo.
Alfajiri saa 11:21 kupitia simu yake ya mkononi yenye namba 0784993***, Profesa Kapuya alituma ujumbe ufuatao kwa mtoto huyo:“chagueni kunisubiri tuje tuongee au mnataka kufa?”
Baadaye saa 1:07 asubuhi, alituma ujumbe mwingine kutoka simu hiyo hiyo kwenda kwa mtoto huyo, ukisema: “Mkiuawa,
itakuwa nzuri, itawapunguzia gharama za kuishi. Usitake kugombana na
serikali, mtoto mdogo kama wewe. Sisi ndo wenye nchi yetu.
“Mwambieni
Mbowe mwenye hilo gazeti awape nyumba ya kuishi. Si mmemuingizia hela
leo? Mnatumika bure watu wanaingiza hela nyingi, mmenitibua lazima
niwauwe wiki hiii haitaisha, nitapanga kambi popote.
“Jana
si wamekuficha? Tuone kama utalindwa milele. Kazi ya kulindwa imeisha,
maana wameshatengeneza hela. Lazima mvae sanda. Hilo sio ombi, ni wajibu
wenu. Mnajitia mafia watoto sio? Watoto wetu wanauza unga, nani
anawakamata? Nani atapigana nasi?”
Hata hivyo,
baada ya kuhisi kuwa watoto hao wamedhamiria kumchukulia hatua, na
wamewasiliana na taasisi mbalimbali za kiraia na serikali zenye uwezo wa
kumtia adabu, mbunge huyo alimtumia mtoto huyo ujumbe wa kuonyesha
alikuwa anafikiria kunywa sumu..
Ujumbe huo uliotumwa kwa mtoto huyo saa 11:2 3 ulisema:“nimewakosea sana, acha nife mie nakunywa sumu nijiue, na nyie mje mnizike.”
Hasira za
Profesa Kapuya dhidi ya mtoto hao zilitokana na hatua ya mtoto huyo na
dada yake kufichua unyama wanaodai kutendewa na mbunge huyo, ambaye
amewahi kushika nyadhifa kadhaa za uwaziri katika Serikali ya Awamu ya
Nne.
Tangu alipogundua kuwa mtoto huyo alizungumza na gazeti hili juzi, saa 5:17 usiku wa kuamkia jana alituma ujumbe usemao: “Si mpo Bilz? Sasa tupo pamoja na nyie mpaka usiku.”
Baadaye saa 5:31 alituma ujumbe huu: “Hivi hamkubali kushindwa? Leo ulifuata nini ofisi ya CCM?”
Ujumbe huo
ulitokana na ukweli kwamba dada wa mtoto anayedaiwa kubakwa alifika
Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) juzi asubuhi kuonana na Katibu
Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana, ili kuomba chama kimsaidie
kumbana Profesa Kapuya, ambaye alikuwa ameanza kuwatisha yeye na mdogo
wake.
Hata hivyo, kwa mujibu wa mtoto huyo, Kinana alisema suala hilo si la chama bali la Profesa Kapuya binafsi.
Mtoto huyo
alikataa ushauri wa kupeleka shauri hilo mbele ya vyombo vya sheria,
akidai kuwa jitihada zake zimekuwa zinazimwa na mbunge huyo anayedai
serikali haiwezi kumfanya lolote.
Alisisitiza
kuwa hana imani na serikali, lakini akasema yupo tayari kuchukua hatua
kali dhidi ya Profesa Kapuya iwapo atasimamiwa na watetezi wa haki za
binadamu.
Baadhi ya
mashirika yanayotetea makundi kadhaa yakiwamo Kituo cha Sheria na Haki
za BInadamu (LHRC) na Mtandao wa Kijinsia Tanzania (TGNP) yalijitokeza
kumsaidia watoto hao, ambao ni yatima.
Mtoto huyo na
dada yake, wakizungumza na gazeti hili kwa hofu mafichoni, walisema kwa
sasa hawana imani tena kama kuna serikali nchini Tanzania kwa kuwa
wamedhalilishwa, wametembezwa hadi Bungeni na wabunge bila hatua
kuchukuliwa, licha ya kutoa taarifa katika kituo cha polisi Oysterbay
tangu mwaka jana.
Hata hivyo,
kabla ya tukio la watoto hao kuripoti, ofisi za gazeti hili juzi usiku
kulikuwa na watu waliokuja wakiwatafuta watoto hao, huku wakiwatisha kwa
simu na kuwatolea maneno ya kejeli, wakidai watawamwagia tindikali.
Mmoja wa watoto
hao, alidai kuwa miongoni mwa vijana waliokuwa wanawatisha juzi
walikuwa katika gari T170 BGY, Benz, Cream Metalic, ambayo inamilikiwa
na mbaya wao.
Jana
gazeti hili lilichapisha habari kuwa mwanafunzi huyo aliyesema kuwa
waziri huyo alimbaka kwenye hoteli moja ya kitalii iliyoko jijini Dar
es Salaam mwaka 2011, na kurudia tena kitendo hicho katika Jengo la
Biashara Complex lililoko Mwananyamala Juni 3, 2012 alipoitwa kwenda
kuchua ada kwa mara ya pili.
Akizungumza kwa uchungu, alisema mbunge huyo alifanya kitendo hicho kwenye Hoteli ya Giraffe, Jijini Dar es Salaam mwaka 2011.
Alisema kuwa
yeye alikuwa na urafiki na mwanafunzi mwenzake Zuhura Mwaking’inda.
Mwaking’inda amewahi kuwa Diwani wa Kata ya Sinza Jimbo la Ubungo,
Jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa
mwanafunzi huyo, rafiki yake (mtoto wa Mwaking’ida) alikuwa amepooza
hivyo alikuwa analazimika kumhudumia hali iliyowaunganisha hadi huyo
mtoto alipochukua jukumu la kumtambulisha kwa baba yake ambaye naye
alimtambulisha kwa Kapuya ili aweze kumsaidia fedha kwa jili ada.
Mwanafunzi huyo
alisema baada ya kutambulishwa aliitwa katika hoteli moja jijini Dar
ambapo baada ya kufika mapokezi wafanyakazi wa hoteli hiyo walimkataza
kuingia chumbani katika maana kwamba umri wake alikuwa mdogo (mwaka 2011
alikuwa na miaka 14), lakini Kapuya aliamrisha aje chumbani pamoja na
dereva na kumwingiza kwa nguvu.
Akiwa chumbani
alimlazimisha kulala naye kisha kumpa sh laki saba, badala ya sh elfu
sitini na saba kiasi ambacho kilikuwa ndio mahitaji halisi ya ada.
Mwanafunzi huyo
amesema baada ya muhula mmoja aliitwa tena na mbunge huyo katika Jengo
la Biashara Complex lililoko Mwananyamala tarehe 3 June 2012, ambapo pia
alimlazimisha kulala naye kwenye zulia la ofisi yake, kisha kumpa sh
350,000/.
Alisimulia
kwamba wakati anatoka kwa huzuni ofisini kwa mbunge huyo, mmoja wa
wahudumu wa hapo alimuuliza kwanini anatoka kwa huzuni, alimweleza kisa
hicho, na huyo mama aliangua kilio kwa kumwambia “mwanangu umekufa pole
tu, huyu baba ni muathirika wa ukimwi”.
Aliongeza kuwa
baada ya kuambiwa vile alilia na kufanya fujo hapo mapokezi hadi
alipokamatwa na walinzi wa kisha kupelekwa kituo cha polisi kufunguliwa
mashtaka, lakini akiwa polisi alipoeleza mkasa wote, Polisi walilazimika
kumwita Kapuya na wakawasuluhisha kwa makubaliano kwamba Kapuya atakuwa
anamlipia ada, na kumpa pesa za matumizi sh. laki tatu kila mwezi,
jambo ambalo amekuwa akilitekeleza kupitia simu yake ya mkononi
0755993***.
Kwa mujibu wa
mwanafunzi huyo, 24 Januari 2013, alifika mtu nyumbani kwao mtu mmoja
(jina tunalihifadhi) na kujitambulisha kuwa yeye ni jambazi na kuwa
alitumwa kwenda kuwaua kwa malipo ya sh. milioni 50, lakini alipokuta ni
watoto wadogo aliwasamehe, na kusema yeye ni jambazi sugu hawezi
kupoteza nguvu zake kuua vitoto.
Alienda akiwa
na bastola, maji kwenye chupa yanayodhaniwa kuwa ni tindikali na bomba
la sindano. Kwa mujibu wa mtoto huyo, jambazi huyo anasema kuwa tayari
alilipwa milioni 15 za awali.
Mtoto huyo
alisema jambazi huyo aliwambia kuwa yeye ni rafiki wa mtoto wa Kapuya na
wanamfahamu vizuri, lakini hataweza kuaua baada ya kubaini kuwa wao ni
yatima tu.
Hata hivyo
kufikia mwezi Februari mwaka huu, mtu asiyefahamika alienda nyumbani na
kutelekeza gari aina ya T.199 BGY Mercedes Benzi ya Blue wakati
wanafunzi hao wakiwa shuleni, kisha kuacha ufunguo kwa jirani yao kwa
maelekezo kuwa wakifika awapatie.
Na Kapuya
aliwapigia simu kuwaarifu kuwa amempa zawadi ya gari kwa ajili ya
matumizi ila yeye na dada yake wanaruhusiwa kuuza ili wapate pesa kwa
ajili ya mahitaji yake siku zilizosalia, kwani muda sio mrefu baada ya
uchguzi mkuu 2015, Kapuya atakuwa Waziri Mkuu, hivyo itakuwa ngumu yeye
kumtumia huyo binti pesa kama alivyoelekezwa na jeshi la polisi kituo
cha Oysterbay.
Baada ya
mwanafunzi huyo na dada yake ambaye ana umri wa miaka 20, kupewa gari
walishindwa kulitumia hivyo kutoa taarifa polisi kwani kwa kupokea gari
hilo ilikuwa ni kuwatelekeza kwani yeye hana hata hela ya kuweka mafuta
ya gari, hivyo walienda polisi ili kesi ipelekwe mahakamani kumshtaki
kapuya.
Polisi wa
Oysterbay walikubali kulipeleka tatizo hilo kwa Katibu wa Bunge, ambaye
alimwita mwanafunzi huyo na mdogo wake waende Dodoma kukutana na Kamati
ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ingawa walipofika Dodoma walikaa
na kamati ya hiyo kwa maelezo kuwa Kapuya hakuwepo hadi Bunge lilipoisha
walirejeshwa Dar es Salaam.
Mtoto huyo na
dada yake alitoka ofisi za CCM lakini akiwa anaelekea kituo cha basi
alithadharishwa na mwanafunzi mwingine kwa haraka kuwa akimbie kwa kuwa
atamwagiwa tindikali na watu waliokuwa wanamfuata nyuma, alikimbilia
katika mtaa wa Hoteli ya Star light kisha aliomba msaada baada ya
kupotea njia na hivyo alisaidiwa na mama mmoja kufikishwa chumba cha
habari cha Channel Ten.
Ni katika
chumba hicho ndio mwandishi wa habari hizi alienda na kuwakuta watu
wawili hao waliokuwa wanamhitaji binti huyo lakini walikatazwa
kumchukua.
Chanzo: Gazeti la Tanzania Daima
Chanzo: Gazeti la Tanzania Daima
MITIHANI KIDATO CHA NNE -2013 YAVUJISHWA
MTIHANI wa Taifa wa Kidato cha Nne, umeingia dosari baada ya walimu wawili akiwamo Mkuu wa Shule, kushikwa wakishiriki kutoa majibu kwa wanafunzi wao.
Tayari
Polisi mkoani Singida, inashikilia walimu hao wa Sekondari ya Nkinto
wilayani Mkalama kwa tuhuma ya kuvujisha mtihani huo unaoendelea
kufanyika nchini kote hivi sasa.
Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Singida, Geofrey Kamwela, alitaja watuhumiwa hao
kuwa ni Mkuu wa Shule, Monica Sebastian (30) na msimamizi wa mtihani
huo, Agaloslo Otieno (32).
Alisema
watuhumiwa hao walivujisha mtihani huo juzi kati ya saa 3 na 3:30
asubuhi katika shule hiyo iliyopo Kata ya Mwangeza Tarafa ya Kirumi.
Alidai
kuwa Mwalimu Agaloslo aliyekuwa akisimamia mtihani katika shule
nyingine ya Mwangeza, aliandika baadhi ya maswali ya Kiswahili na Uraia
kwenye simu yake ya mkononi na kumtumia Mkuu wa Shule yake ya Nkinto,
Monica aliyekuwa shuleni kwake.
Baada
ya Monica kupata maswali hayo, inadaiwa alitafuta majibu akiwa chooni
huku wanafunzi wakimfuata huko huko na kupewa majibu.
Kamanda
Kamwela alisema lengo lao lilikuwa kusaidia wanafunzi, wafanye vizuri
katika mtihani wao wa kidato cha nne mwaka huu. Alisema wanafunzi
waliishaambiwa wadanganye wanakwenda chooni, ili wakapewe majibu na Mkuu
wa Shule.
"Uchunguzi
wa awali unaonesha kuwa uvujishaji huo ulifanyika kwa nyakati tofauti
kati ya Monica na Mwalimu Agaloslo akiwa anasimamia mtihani huo katika
shule tofauti.
“Baada
ya Mkuu wa Shule kutumiwa maswali, alijificha chooni na watahiniwa kwa
nyakati tofauti waliomba ruhusa kwa wasimamizi kwenda kujisaidia na hapo
walimkuta Mkuu wa Shule na kuwapa maelekezo ya namna ya kujibu maswali
hayo," alisema Kamanda Kamwela.
Alisema
baada ya Polisi kupata taarifa ya siri kutoka kwa wasamaria, iliweka
mtego katika Sekondari ya Nkinto na kumkamata Mwalimu Monica huku simu
yake ikiwa na baadhi ya maswali ya mtihani.
-Habari Leo
-Habari Leo
TPA NA TRA AIBU KWAO
SIMU moja baada ya Waziri wa Maliasili
na Utalii Balozi Khamisi Kagasheki, kutangaza kwamba Mamlaka ya Mapato
nchini (TRA) inahusika katika ujangili, Waziri wa Uchukuzi Dk Harrison
Mwakyembe pia ameibuka leo na kutangaza kwamba TRA pamoja na Mamlaka ya
Bandari (TPA) kwa pamoja zinahusika katika biashara ya magendo nchini.
Balozi Kagasheki akiwa visiwani Zanzibar katika zoezi la kupakuwa shehena
kubwa ya pembe za Tembo ikiwa na vipande 1,021 na uzito wa kilo 2,915
ambayo haijawahi kukamatwa nchini, alisema kwamba TRA wanahusika katika
ujangili huo kwa sababu wao ndiyo wenye mamlaka ya kuhakikisha kwamba
mizigo yote haramu haipiti katika bandari hiyo.
"Katika hili siwezi kumumunya maneno,
lazima tu nisema ukweli hata kama wenzetu hawa watakasirika, lakini
ukweli ni kwamba hawana pa kukwepea kwani wanahusika kwa asilimia 100
katika ujangili huu, kwa sababu kama watu wasingekuwa na maslahi katika
hili kontena lisingekamatiwa hapa Zanzibar, hii ni ishara kwamba TRA
wanahusika na kusaidia kulipitisha hadi huku"alisema Balozi Kagasheki.
Balozi alisema kwamba, shehena
hiyo iliyokuwa tayari kusafirishwa kuelekea Philiphine ilikuwa katika
magunia 98 yaliyochanganywa na magunia mengine ambayo yalikuwa
yamefungwa pamoja na baadhi ya vitu vya baharini yalikuwa tayari
yameshawekwa ndani ya kontena la futi 40 tayari kwa kusafirishwa kwenda
Philiphne yakiwa katika hatua za mwisho za mamlaka husika za bandarini.
Katika hatua nyingine, Waziri wa
Uchukuzi Dk Mwakyembe akiwa jijini Tanga ametangaza vita rasmi na
wafanyabiashara wanaoingiza bidhaa za magendo kupitia Bandari bubu
Mkoani Tanga huku akidai kwamba maofisa wa vyombo vya Serikali waliopo
kwenye mtandao huo watakiona cha moto. Dk Mwakyembe aliwataka watambue
kuwa, kiama chao kimefika kwa sababu tayari Serikali inayo majina ya
wafanyabiashara na baadhi ya maofisa wa Polisi, Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) na Mamlaka ya Bandari (TPA) wanaotumika kufanikisha
upitishaji magendo.
Dk Mwakyembe ambaye aliwasili Tanga juzi
na kufanya ziara ya ghafla kutembelea bandari bubu zilizoko mkoani
hapa, alitangaza vita hiyo alipozungumza na maofisa wa TRA, Polisi, TPA
na wafanyabiashara. Alisema baada ya Serikali kudhibiti Bandari ya Dar
es Salaam, wafanyabiashara magwiji wa upitishaji bidhaa za magendo
wamehamishia nguvu zao Tanga. “Natangaza rasmi vita dhidi ya walio
katika mtandao huo, watambue hatuwezi kuruhusu Bandari ya Tanga, bandari
bubu na mpaka wa Horohoro kuwa gulio la walanguzi, wapitishaji dawa za
kulavya na wahamiaji haramu,” alisema.
MGANGA WA DIAMOND AFUNGUKA HADHARANI
Dk
Kamdege kutoka Tabora ambae inasemekana amekuwa kwenye ukaribu na
mwanamuziki Diamond pamoja na Pennieh hata kabla hawaanzisha mahusiano
yako.
Mganga huyo wa kienyeji ambae amekuwa maarufu sana tangu aanze huduma huyo kutokana na watu maarufu wengi kumfuata kwa ajili ya kutatuliwa mambo yao ikiwemo mafanikio kwenye biashara, kazi, muziki, sanaa, uongozi ngzi za juu pamoja na michezo.
Habari zaidi zilisema miezi kadhaa iliyopita mganga huyo aliwahi kujitoa kwenye vyombo vha habari akimsihi Pennie aende kwake akamtafutie dawa ili Diamond atulie kwani inamfahamu viuzri mwanamuziki huyo na anajua kitu ambacho angefanya.
Haikupta muda bila kufahamika kama Pennie alienda kwa Dk huyo au lakini hatimae Diamond alianza kurejea kwa Pennie na mambo yalimalizika kabisa kabla ya kuzuka kwa haya ya undugu na ndio maana watu wa karibu wamesema kuwa Dk huyu anahusika kwenye mahusiano hayo ya Diamond na Pennie kwa kuwa ni watu wake wa karibu sana.
Blog hii ilimtafuta DK huyo na alipatikana kupitia namba yake ya simu 0788-844490 na
alianza kusema" Mimi hao vijana nawafahamu sana lakini mimi ni Dk wa Watanzania wote sio Pennie na Wema tu hapana kazi zangu zinakubarika na watanzania wote na hata nje ya nchi kwani mimi nawatolea watu mikosi wanaotaka kuwa maarufu na wenye mafanikio pia nawanyooshea njia kwa hiyo naomba msiseme mimi ni Dk wa Pennie na Diamond hata viongozi wakubwa Serikalini nawapatia baraka zangu kisha wanaenda kufanikiwa huwa sipendi kujitangaza huko kwani mimi situmii uchawi kumpa mutu mfanikio hapana hapa ni miti shamba tu inafanyakazi yake" Alisema Kamdege
Aidha Mganga huyo anasemekana amekuwa akitumiwa sana na baadhi ya viongozi serikalini kwa ajili ya mafanikio kupata uongozi, kupandishwa vyeo kazini, kupewa dawa ya kumuona mbaya wako kwa macho tu huku mastaa wengi wa muziki, filamu, na biashara akiwa tegemeo lao...
Subscribe to:
Posts (Atom)