Nyumba anayoishi Mchungaji Mwaikambo ikiwa imepigwa kufuri huku mwenyewe akiwa ''amelala mbele!! baada ya kufanya unyama wake |
MCHUNGAJI wa
kanisa la Pentekostal aliyefahamika kwa jina la Bryson Mwaikambo(55) anadaiwa
kuwabaka na kuwaambukiza ugonjwa wa zinaa wanafunzi wawili wa kike wanaosoma
katika shule ya msingi ya Maendeleo wa
kata ya Nsalala wilaya ya Mbeya vijiji mkoani Mbeya.
Wanafunzi
hao (majina yanahifadhiwa) wenye umri kati ya miaka 11 na 13 wanaosoma darasa
la nne na darasa la sita walifanyiwa unyama huo kuanzia mwaka 2012 ambapo
alianza kujenga mazoea na watoto hao wadogo kwa kuwapa peremende pamoja
na fedha.
Imeelezwa
kuwa mchungaji huyo ambaye anaendesha ibada katika kanisa hilo dogo lenye
waumini wachache lililopo kitongoji cha kanani kijiji cha ‘Tunduma Road’alikuwa
akiwavizia watoto hao kwa muda mrefu kila walipokuwa wanapita kuelekea shuleni.
Katika
jitihada zake za kuwanasa watoto hao wa kike alimdanganya mmoja wa wazazi wa
watoto aliyefahamika kwa jina la Bw.John Mussa(38) na kumuomba binti yake awe
anamsaidia kazi za nyumbani nyakati za jioni kutokana na kuwa mke wa mchungaji kuwepo safarini.
Kwa kuamini kuwa
mchungaji huyo alikuwa ni mtumishi wa Mungu, Bw. Mussa aliridhia mwanaye aende
kuishi na Mtumishi huyo wa Mungu bila kujua hatima ya kile ambacho kimemtokea
binti yake kwa sasa.
Kwa mujibu
wa maelezo kutoka kwa wazazi na walimu wa shule ya Msingi Maendeleo ni kwamba
mabinti hao walikuwa wakifanya ngono na mchungaji huyo kwa zamu na kwamba
walianza kujua tatizo hilo baada ya kutokea mgongano baina ya wasichana hao
wawili .
‘’Tumejua
tukio hili baada ya kutokea ugomvi baina yao wa kugombania maji na hivyo kuanza
kurushiana maneno, mmoja wa watoto hao alikuja ofisini kushitaki kuhusu ugomvi
wao ndipo mmoja akasema kuwa mwenzie anatembea na Mchungaji Mwaikambo’’alisema
Mwalimu mkuu msaidizi Bi. Lucy Kamongile.
Alifafanua
kuwa, baada ya tukio hilo walimu kwa pamoja walilazimika kuwauliza zaidi ndipo
walipoanza kujieleza kuwa wamekuwa wakilala na Mchungaji huyo kwa muda mrefu na
kwamba mwanzo alikuwa akiwapa peremende na baadaye akaanza kuwapa fedha.
Alisema kuwa
walilazimika kuitisha kikao cha dharura baina ya wazazi wa watoto hao na walimu
ambapo walieleza tukio zima la kuingiliwa kimwili na Mchungaji huyo tangu mwaka
jana.
‘’Nililazimika
kuwaita wazazi pamoja na wanafunzi tulikaa katika ofisi ya walimu, watoto
walieleza tukio zima mbele ya wazazi wao juu ya vitendo walivyokuwa wakifanyiwa
na Mchungaji huyo.
Alisema kuwa
mara baada ya kikao hicho cha wazazi waliwapeleka watoto hao katika kituo
kidogo cha Polisi kilichopo katika
mji mdogo wa Mbalizi ambako walipewa
Fomu ya Polisi Na. 3,(PF3) kwa ajili ya kuepelekwa hospitali ili wapatiwe
matibabu.
Mwalimu
Kamongile ambaye alikuwa na walimu wenzie katika ofisi ya Mwalimu mkuu wa shule
hiyo wakati akitoa taarifa hizi mbele ya Ripota Wetu kuwa
wanafunzi hao walipatiwa matibabu katika hospitali Teule ya Ifisi ambapo kwa
mujibu wa taarifa za mganga aliyewachunguza
watoto hao ni kwamba mbali na kufanyiwa ubakaji wote wawili walikuwa
wameambukizwa ugonjwa wa zinaa wa kaswende.
‘’Tukio hili
limetufedhehesha sana tulikuwa tunatafakari wapi tutaenda,tunaomba kilio chetu
kifike chama cha Waandishi wa Habari wanawake TAMWA kitoe taarifa hizi kwa
undani waone namna ambavyo jamii ya pembezoni inavyokosa msaada na haki za
kisheria,’’alisema Mwalimu Kamongile.
Mwalimu huyo
alisema kuwa wanatambua juhudi za chama cha waandishi wa habari wanawake TAMWA
ambazo wamekuwa wakizifanya hivyo wanaimani chama hicho kikisikia suala
kitalifanyia kazi kwa kina zaidi kuisaidia jamii ambayo aina mahali pa kusemea.
Kwa upande
wa watoto hao ambao walikuwa wakizungumza kwa kupokezana juu ya kadhia
iliyowakuta walisema kuwa Mchungaji huyo alianza kufanya nao vitendo vya ngono
tangu mwaka 2012 kwa kuwadanganya kwa fedha na peremende na baadaye wakazoea
kwenda kwa Mchungaji huyo mara kwa mara.
Mwanafunzi
anayesoma darasa la nne alisema kuwa alianza kutembea na Mchungaji huyo wakati
akimpitia mwenzie aliyekuwa akiishi nyumbani kwa mchungaji ambapo siku hiyo
alimuita chumbani kwake na kumlazimisha kulala kitandani ambapo alianza
kumuingiza vidole katika sehemu zake za siri.
“Siku ya
kwanza nililia sana wakati mwenzangu yupo pembeni akishuhudia mchungaji
akinifanya na ndipo mwenzangu alisema jikaze rafiki yangu”alisema Mtoto huyo.
Alisema kuwa
mara baada ya kumuingiza vidole alivua nguo zake na kumbaka huku akilia wakati
msichana mwenzie (alimtaja jina) akiwa amekaa pembeni ya kitanda akimweleza
kuwa aache kulia kwa kuwa baada ya kumaliza watapewa fedha za kutumia shuleni.
Binti huyo
aliendelea kusema kuwa alipata maumivu makali wakati Mchungaji huyo akitekeleza
ubakaji wake ambapo mara baada ya kumaliza` alimpa sh.500 na peremende na
baadaye alimwita mwenzie kitandani na kufanya naye ngono huku akishuhudia kwa
macho yake.
Alisema mara
baada ya kumaliza kufanya na mwenzie Mchungaji Mwaikambo aliwaonya wasiseme kwa
wazazi wao kisha akawapa fedha na kuwaonya wasiseme jambo hilo kwa mtu yoyote.
Akizungumza
sababu za kutosema kwa walimu au wazazi wake binti mwingine anayesoma darasa la
sita alisema kuwa Mchungaji huyo aliwatishia kuwachinja na kuwafukia kwenye
shimo iwapo atasikia wamesema tukio hilo kwa wazazi ama walimu wao.
Alisema kuwa
Mchungaji aliwaomba wazazi wake ili aende kuishi nyumbani kwake kumsaidia kazi
kutokana na mama Mchungaji ‘’Mke wa Mchungaji’’ kuwa safarini na kwamba katika
siku hizo ndipo Mchungaji huyo alipoanza kulala naye mahusiano taratibu.
Alisema kwa
siku za mwanzo alikuwa akimuingiza vidole katika sehemu zake za siri na baadaye
akaanza kumbaka ambapo alijisikia maumivu makali lakini alimbembeleza kwa kumpa
sh.1000 ambayo alikuwa akitumia shuleni kwa kununua chipsi.
‘’Alikuwa
akiniingiza vidole huku chini(akionyesha sehemu za siri) akanibaka, sikuweza
kumwambia baba niliogopa atanichinja..mwenzangu alipokuwa anakuja kunipitia
kwenda shuleni naye alianza kumuingiza vidole akambaka!!, alilia sana,
nikamwambia asilie atatupa hela,’’alisema.
Alisema kuwa
wamebakwa na Mchungaji huyo zaidi ya mara nne na kila alipokuwa akiwabaka
alikuwa anawapa hela za kutumia shuleni.
Kwa upande
wazazi wa watoto hao Bw.Suveli Harrison na Bw. John Mussa walikiri kuitwa
shuleni na kupata taarifa za kubakwa kwa watoto wao walipoitwa shuleni ambapo
watoto walijieleza walichokuwa wakifanyiwa na Mchungaji Mwaikambo mbele ya
walimu.
‘’Jambo hili
lilitushitua sana, machozi yalitulenga, hatukutegemea kusikia Mchungaji anaweza
kuwabaka watoto ambao ni sawa na wajukuu zake, tulienda polisi walitupa
karatasi tukaenda Hospitali ya Ifisi, watoto walikutwa na maambukizi ya ugonjwa
wa zinaa,’’alisema Bw. John Mussa.
Alisema kuwa
yeye aliridhia mwanaye kuishi na Mchungaji huyo baada ya kuombwa kutokana na
mchungaji huyo kuishi na mtoto mdogo wakati mkewe akiwa safarini.
Bw. Mussa
alisema kuwa hakujua kuwa kama kuna siku mwanaye atadhurika kwa kufanyiwa
kitendo cha unyanyasaji na ukatili wa kijinsia kama walivyofanyiwa watoto hao
na kwamba hata hivyo hadi sasa hakuna jitihada zozote za jeshi la polisi
zilizofanikisha kumnasa Mchungaji huyo.
Alisema kuwa
kwa sasa watoto hao wamekuwa wakitishiwa na Mchungaji kutokana na kufahamika
kuwa yeye aliwabaka na kwamba anaomba msaada wa kisheria kusimamia haki ili
sheria iifuatwe dhidi ya mtuhumiwa wa ubakaji.
Naye mzazi
mwingine Bw.Suvile Harrison alisema kuwa hakujua chochote juu ya vitendo
alivyofanyiwa mwanaye na Mchungaji huyo na
kwamba alifahamu tukio hilo baada ya kuitwa shuleni ambako walimu
waliwaita watoto wao na kueleza tukio zima walilokuwa wakifanyiwa na Mchungaji.
Alisema kuwa
hakubaini mabadiliko yoyote kwa mwanaye juu ya vitendo alivyofanyiwa na wala
hajawahi kuhisi lolote hadi hapo alipoitwa shuleni na walimu.
Baada ya
taarifa hizo waandishi wa habari wa gazeti hili walifunga safari hadi katika
nyumba ambayo inasadikiwa kuwa ndipo anapoishi Mchungaji huyo na kukuta mlango
ukiwa umefungwa lakini alijitokeza jamaa ambaye alijitambulisha kuwa ni mmiliki
wa nyumba hiyo Bw. Zacharia Gambi.
Bw.Gambi
alisema kuwa anamfahamu mpangaji wake kwa jina moja la Mchungaji Mwaikambo na
kwamba mbali ya kuwa ni Mchungaji wa Kanisa la Kipentekoste ni Balozi wa nyumba
kumi wa mtaa wa Kanani.
Bw.Gambi
alisema kuwa Mchungaji huyo hajaonekana muda mrefu na kwamba mkewe amekuwa na desturi
ya kuondoka alfajiri kuelekea shambani na kurudi usiku.
Kadhalika
imeelezwa na baadhi ya watu ambao hawakupenda kutajwa majina yao gazetini
kuwa kitendo cha Mchungaji huyo kuwabaka
mabinti wadogo kimetokana na imani za nguvu za giza kwamba kwa kufanya hivyo
kitamuongezea waumini katika kanisa lake dogo lililopo katika mtaa wa Kanani.
Mama mzazi
wa mmoja wa watoto waliobakwa aliyejitambulisha kwa jina la Jane John(35)
alisema kuwa awali yeye alikuwa ni mmoja wa waumini katika kanisa hilo lakini
baadaye walihamia kanisa jingine baada ya kuona mienendo ya mchungaji huyo
kutofanana na kazi ya huduma za kiroho.
Alisema
waumini wengi wamehama katika kanisa hilo wakiwemo watoto wake wakubwa wa kike
ambao walieleza waziwazi tabia ya ukware ya Mchungaji huyo ya kuwafuatilia
mabinti wadogo kwa ajili ya kufanya nao vitendo vya ngono.
Diwani wa
Kata ya Nsalala iliyopo Mbeya vijijini Bw.Mashauri Mbembela alipozungumza na
waandishi wa gazeti hili alisema kuwa anashangazwa tukio hilo kutoshughulikiwa
kwa kipindi chote huku taarifa zikiwa zimefikishwa kituo cha polisi.
Alisema kuwa
tukio hilo ni la unyanyasaji ambalo lilipaswa kushughulikiwa kwa nguvu zote na
kwamba kuna haja ya kuweka sheria ngumu itakayokomesha vitendo vya ubakaji kwa
watoto wa kike.
Bw.Mbembela
alisema kuwa ili kukomesha tabia za ubakaji, itungwe sheria ya kuwahasi
wabakaji badala ya kuwafunga jela miaka 30
ambako wanaenda kula chakula kinachotokana na kodi za wananchi.
‘’Wabakaji
wanafungwa jela, wakimaliza vifungo vyao hurejea uraiani ambako wanaweza
kuendeleza vitendo hivyo, njia pekee ya kukomesha ubakaji ni kuwahasi, wakirudi
uraiani wataendeleza kujenga Taifa,’’alisema Bw. Mbembela.
Ripota wetu alifanya jitihada za kutafuta namba za simu za mchungaji huyo ambaye mara
baada ya kupokea na kuulizwa juu ya tuhuma hizo alikanusha na kusema kuwa huu
ni uzushi na uongo uliolenga kumpaka matope ili kuchafua huduma zake anazotoa
kwa waumini .
Alidai kuwa
kanisa lake la Pentecostal Holiness lenye
jumla waumini nane linatoa huduma za uhakika kijijini hapo hivyo baadhi
ya wafuasi wa shetani wanalipiga vita ili lisiendelee kukua ili kuwafikia
wanakondoo wengi.
“Wananipakazia
tu unaweza kuingiwa na ibilisi na hivi ulivyonipigia nafikiria kuchukua maamuzi
magumu na mwili wangu hamtauona kamwe bora uliwe na ndege na wanyama wa porini niende jehanamu kuliko kuchafuliwa
huku”alisema Mchungaji huyo.
Alisema kuwa
tuhuma hizo zimeelekezwa kwake baada ya kumdai fedha mmoja wa wazazi wa watoto
hao ambaye alikuwa akifanya kibarua cha kujenga ofisi ya kata ambapo mama huyo
alimkopesha fedha sh.5000 na alipoanza kudai ndipo akaanza kuzushiwa tuhuma
hizo.
Hata hivyo
alisema Jumanne iliyopita alifuatwa na
askari mgambo sita wenye virungu ambao walitaka kumkamata lakini kwa nguvu za
yesu walishindwa na kuondoka zao.
“Mimi naishi
kwa nguvu za Yesu mtu yeyote mwenye nia mbaya na mimi hawezi kunipata nataka
niwe kama mfalme aliyejitoa mhanga nijiue mwili wangu usionekane
duniani”alisisitiza na kukata simu.
Kamanda wa
polisi mkoa wa Mbeya Bw.Diwani Athumani alisema kuwa amepata taarifa hizo za
ubakaji ambapo amemuagiza Ofisa Upelelezi wa Mkoa Bw.Mtatiro Nyamuhanga ambaye
atalifuatilia kwa karibu tukio hilo na kwamba hata hivyo mtuhumiwa bado
hajatiwa mbaroni.
No comments:
Post a Comment