MBUNGE wa Urambo Magharibi, Profesa Juma Kapuya (CCM), ameingia katika matata. Katika kujaribu kudhibiti mtoto wa shule ambaye anadai alibakwa naye na kuambukiwa virusi vya ukimwi, mbunge huyo ametoa vitisho vya kuua mtoto huyo na kujiua kama njia ya kuepuka dhahama inayoelekea kumkabili.
Siku moja baada
ya gazeti la Tanzania Daima kuripoti habari za mbunge mmoja (bila
kumtaja jina), jana asubuhi Profesa Kapuya ameibuka na kumtisha
mwanafunzi huyo mwenye miaka 16 anayesoma Shule ya Sekondari Turiani
iliyoko Magomeni jijini Dar es Salaam.
Baada ya kujua
kuwa mtoto huyo ndiye alitoa habari za masahibu hayo, ambayo mbunge
hakutaka yajulikane, alimpigia simu mtoto huyo, na baadaye kutuma meseji
kadhaa za vitisho.
Jana Tanzania Daima ilishuhudia baadhi ya meseji za simu zilizotumwa na Profesa Kapuya kwenda kwa mtoto huyo.
Alfajiri saa 11:21 kupitia simu yake ya mkononi yenye namba 0784993***, Profesa Kapuya alituma ujumbe ufuatao kwa mtoto huyo:“chagueni kunisubiri tuje tuongee au mnataka kufa?”
Baadaye saa 1:07 asubuhi, alituma ujumbe mwingine kutoka simu hiyo hiyo kwenda kwa mtoto huyo, ukisema: “Mkiuawa,
itakuwa nzuri, itawapunguzia gharama za kuishi. Usitake kugombana na
serikali, mtoto mdogo kama wewe. Sisi ndo wenye nchi yetu.
“Mwambieni
Mbowe mwenye hilo gazeti awape nyumba ya kuishi. Si mmemuingizia hela
leo? Mnatumika bure watu wanaingiza hela nyingi, mmenitibua lazima
niwauwe wiki hiii haitaisha, nitapanga kambi popote.
“Jana
si wamekuficha? Tuone kama utalindwa milele. Kazi ya kulindwa imeisha,
maana wameshatengeneza hela. Lazima mvae sanda. Hilo sio ombi, ni wajibu
wenu. Mnajitia mafia watoto sio? Watoto wetu wanauza unga, nani
anawakamata? Nani atapigana nasi?”
Hata hivyo,
baada ya kuhisi kuwa watoto hao wamedhamiria kumchukulia hatua, na
wamewasiliana na taasisi mbalimbali za kiraia na serikali zenye uwezo wa
kumtia adabu, mbunge huyo alimtumia mtoto huyo ujumbe wa kuonyesha
alikuwa anafikiria kunywa sumu..
Ujumbe huo uliotumwa kwa mtoto huyo saa 11:2 3 ulisema:“nimewakosea sana, acha nife mie nakunywa sumu nijiue, na nyie mje mnizike.”
Hasira za
Profesa Kapuya dhidi ya mtoto hao zilitokana na hatua ya mtoto huyo na
dada yake kufichua unyama wanaodai kutendewa na mbunge huyo, ambaye
amewahi kushika nyadhifa kadhaa za uwaziri katika Serikali ya Awamu ya
Nne.
Tangu alipogundua kuwa mtoto huyo alizungumza na gazeti hili juzi, saa 5:17 usiku wa kuamkia jana alituma ujumbe usemao: “Si mpo Bilz? Sasa tupo pamoja na nyie mpaka usiku.”
Baadaye saa 5:31 alituma ujumbe huu: “Hivi hamkubali kushindwa? Leo ulifuata nini ofisi ya CCM?”
Ujumbe huo
ulitokana na ukweli kwamba dada wa mtoto anayedaiwa kubakwa alifika
Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) juzi asubuhi kuonana na Katibu
Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana, ili kuomba chama kimsaidie
kumbana Profesa Kapuya, ambaye alikuwa ameanza kuwatisha yeye na mdogo
wake.
Hata hivyo, kwa mujibu wa mtoto huyo, Kinana alisema suala hilo si la chama bali la Profesa Kapuya binafsi.
Mtoto huyo
alikataa ushauri wa kupeleka shauri hilo mbele ya vyombo vya sheria,
akidai kuwa jitihada zake zimekuwa zinazimwa na mbunge huyo anayedai
serikali haiwezi kumfanya lolote.
Alisisitiza
kuwa hana imani na serikali, lakini akasema yupo tayari kuchukua hatua
kali dhidi ya Profesa Kapuya iwapo atasimamiwa na watetezi wa haki za
binadamu.
Baadhi ya
mashirika yanayotetea makundi kadhaa yakiwamo Kituo cha Sheria na Haki
za BInadamu (LHRC) na Mtandao wa Kijinsia Tanzania (TGNP) yalijitokeza
kumsaidia watoto hao, ambao ni yatima.
Mtoto huyo na
dada yake, wakizungumza na gazeti hili kwa hofu mafichoni, walisema kwa
sasa hawana imani tena kama kuna serikali nchini Tanzania kwa kuwa
wamedhalilishwa, wametembezwa hadi Bungeni na wabunge bila hatua
kuchukuliwa, licha ya kutoa taarifa katika kituo cha polisi Oysterbay
tangu mwaka jana.
Hata hivyo,
kabla ya tukio la watoto hao kuripoti, ofisi za gazeti hili juzi usiku
kulikuwa na watu waliokuja wakiwatafuta watoto hao, huku wakiwatisha kwa
simu na kuwatolea maneno ya kejeli, wakidai watawamwagia tindikali.
Mmoja wa watoto
hao, alidai kuwa miongoni mwa vijana waliokuwa wanawatisha juzi
walikuwa katika gari T170 BGY, Benz, Cream Metalic, ambayo inamilikiwa
na mbaya wao.
Jana
gazeti hili lilichapisha habari kuwa mwanafunzi huyo aliyesema kuwa
waziri huyo alimbaka kwenye hoteli moja ya kitalii iliyoko jijini Dar
es Salaam mwaka 2011, na kurudia tena kitendo hicho katika Jengo la
Biashara Complex lililoko Mwananyamala Juni 3, 2012 alipoitwa kwenda
kuchua ada kwa mara ya pili.
Akizungumza kwa uchungu, alisema mbunge huyo alifanya kitendo hicho kwenye Hoteli ya Giraffe, Jijini Dar es Salaam mwaka 2011.
Alisema kuwa
yeye alikuwa na urafiki na mwanafunzi mwenzake Zuhura Mwaking’inda.
Mwaking’inda amewahi kuwa Diwani wa Kata ya Sinza Jimbo la Ubungo,
Jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa
mwanafunzi huyo, rafiki yake (mtoto wa Mwaking’ida) alikuwa amepooza
hivyo alikuwa analazimika kumhudumia hali iliyowaunganisha hadi huyo
mtoto alipochukua jukumu la kumtambulisha kwa baba yake ambaye naye
alimtambulisha kwa Kapuya ili aweze kumsaidia fedha kwa jili ada.
Mwanafunzi huyo
alisema baada ya kutambulishwa aliitwa katika hoteli moja jijini Dar
ambapo baada ya kufika mapokezi wafanyakazi wa hoteli hiyo walimkataza
kuingia chumbani katika maana kwamba umri wake alikuwa mdogo (mwaka 2011
alikuwa na miaka 14), lakini Kapuya aliamrisha aje chumbani pamoja na
dereva na kumwingiza kwa nguvu.
Akiwa chumbani
alimlazimisha kulala naye kisha kumpa sh laki saba, badala ya sh elfu
sitini na saba kiasi ambacho kilikuwa ndio mahitaji halisi ya ada.
Mwanafunzi huyo
amesema baada ya muhula mmoja aliitwa tena na mbunge huyo katika Jengo
la Biashara Complex lililoko Mwananyamala tarehe 3 June 2012, ambapo pia
alimlazimisha kulala naye kwenye zulia la ofisi yake, kisha kumpa sh
350,000/.
Alisimulia
kwamba wakati anatoka kwa huzuni ofisini kwa mbunge huyo, mmoja wa
wahudumu wa hapo alimuuliza kwanini anatoka kwa huzuni, alimweleza kisa
hicho, na huyo mama aliangua kilio kwa kumwambia “mwanangu umekufa pole
tu, huyu baba ni muathirika wa ukimwi”.
Aliongeza kuwa
baada ya kuambiwa vile alilia na kufanya fujo hapo mapokezi hadi
alipokamatwa na walinzi wa kisha kupelekwa kituo cha polisi kufunguliwa
mashtaka, lakini akiwa polisi alipoeleza mkasa wote, Polisi walilazimika
kumwita Kapuya na wakawasuluhisha kwa makubaliano kwamba Kapuya atakuwa
anamlipia ada, na kumpa pesa za matumizi sh. laki tatu kila mwezi,
jambo ambalo amekuwa akilitekeleza kupitia simu yake ya mkononi
0755993***.
Kwa mujibu wa
mwanafunzi huyo, 24 Januari 2013, alifika mtu nyumbani kwao mtu mmoja
(jina tunalihifadhi) na kujitambulisha kuwa yeye ni jambazi na kuwa
alitumwa kwenda kuwaua kwa malipo ya sh. milioni 50, lakini alipokuta ni
watoto wadogo aliwasamehe, na kusema yeye ni jambazi sugu hawezi
kupoteza nguvu zake kuua vitoto.
Alienda akiwa
na bastola, maji kwenye chupa yanayodhaniwa kuwa ni tindikali na bomba
la sindano. Kwa mujibu wa mtoto huyo, jambazi huyo anasema kuwa tayari
alilipwa milioni 15 za awali.
Mtoto huyo
alisema jambazi huyo aliwambia kuwa yeye ni rafiki wa mtoto wa Kapuya na
wanamfahamu vizuri, lakini hataweza kuaua baada ya kubaini kuwa wao ni
yatima tu.
Hata hivyo
kufikia mwezi Februari mwaka huu, mtu asiyefahamika alienda nyumbani na
kutelekeza gari aina ya T.199 BGY Mercedes Benzi ya Blue wakati
wanafunzi hao wakiwa shuleni, kisha kuacha ufunguo kwa jirani yao kwa
maelekezo kuwa wakifika awapatie.
Na Kapuya
aliwapigia simu kuwaarifu kuwa amempa zawadi ya gari kwa ajili ya
matumizi ila yeye na dada yake wanaruhusiwa kuuza ili wapate pesa kwa
ajili ya mahitaji yake siku zilizosalia, kwani muda sio mrefu baada ya
uchguzi mkuu 2015, Kapuya atakuwa Waziri Mkuu, hivyo itakuwa ngumu yeye
kumtumia huyo binti pesa kama alivyoelekezwa na jeshi la polisi kituo
cha Oysterbay.
Baada ya
mwanafunzi huyo na dada yake ambaye ana umri wa miaka 20, kupewa gari
walishindwa kulitumia hivyo kutoa taarifa polisi kwani kwa kupokea gari
hilo ilikuwa ni kuwatelekeza kwani yeye hana hata hela ya kuweka mafuta
ya gari, hivyo walienda polisi ili kesi ipelekwe mahakamani kumshtaki
kapuya.
Polisi wa
Oysterbay walikubali kulipeleka tatizo hilo kwa Katibu wa Bunge, ambaye
alimwita mwanafunzi huyo na mdogo wake waende Dodoma kukutana na Kamati
ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ingawa walipofika Dodoma walikaa
na kamati ya hiyo kwa maelezo kuwa Kapuya hakuwepo hadi Bunge lilipoisha
walirejeshwa Dar es Salaam.
Mtoto huyo na
dada yake alitoka ofisi za CCM lakini akiwa anaelekea kituo cha basi
alithadharishwa na mwanafunzi mwingine kwa haraka kuwa akimbie kwa kuwa
atamwagiwa tindikali na watu waliokuwa wanamfuata nyuma, alikimbilia
katika mtaa wa Hoteli ya Star light kisha aliomba msaada baada ya
kupotea njia na hivyo alisaidiwa na mama mmoja kufikishwa chumba cha
habari cha Channel Ten.
Ni katika
chumba hicho ndio mwandishi wa habari hizi alienda na kuwakuta watu
wawili hao waliokuwa wanamhitaji binti huyo lakini walikatazwa
kumchukua.
Chanzo: Gazeti la Tanzania Daima
Chanzo: Gazeti la Tanzania Daima
No comments:
Post a Comment