Pages

Translate

Wednesday 30 October 2013

MTOTO WA MIAKA 8 ALAZIMISHWA KUWA HAUSIGELI,MWAJIRI WAKE AMCHANJA NA KISU.





UKATILI! Katika hali ya kusikitisha, mtoto mwenye umri wa miaka 8 aliyejitambulisha kwa jina la Loveness na mwenzake aitwaye Anna, wanadaiwa kulazimishwa kufanya kazi za ndani huku wakipata vipigo vikali kutoka kwa waajiri wao. 
Loveness alikuwa akifanyishwa kazi Ubungo-Maziwa na Anna alikuwa Kimara jijini Dar.
Watoto hao wameeleza kazi nzito wanazofanyishwa katika mazingira magumu wakiwa na umri mdogo, wanaohitaji kwenda shule.
“Mama (mwajiri wake) alikuwa akinipiga na wakati mwingine kunichanja na kisu,” alisema Loveness.

Majirani ambao hawakupendezwa na matukio hayo, waliitonya Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers ili kufuatilia suala hilo.
Jirani mmoja ambaye hakutaka kutajwa gazetini, alidai kwamba alikuwa akiumizwa na mwajiri wa Anna ambaye alikuwa akimpa vipigo vikali mtoto huyo ambaye alikuwa akimlea mtoto wa mama huyo kila siku.
“Hakuna kitu kilichokuwa kikituumiza majirani kama mtoto Anna ambaye alikuwa akipata vipigo vikali kila siku iendayo kwa Mungu kutoka kwa mwajiri wake, heri arudi kwao,” alisema.

Mtangazaji wa kipindi cha Wanawake Live kinachotetea haki za watoto na wanawake kupitia EATV, Joyce Kiria alitinga nyumbani kwa waajiri hao na kumkamata mmoja wao kisha  kumpeleka katika Kituo cha Polisi cha Kimara, Dar kwa ajili ya kujibu mashitaka ya kukaa na mtoto mdogo kama mfanyakazi.
Hata hivyo, mtangazaji huyo aliamua kuwachukua watoto hao na kwenda kuishi nao nyumbani kwake Changanyikeni, Dar, kwa ajili ya kufanya utaratibu wa kuwasafirisha vijijini kwao ambapo Loveness anatokea Morogoro na Anna ametokea Singida.
Joyce amekuwa akifanya mawasiliano na familia za watoto hao ili kuwarejesha kwao huku Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Sophia Simba na Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka wakiombwa kuangalia suala hilo la unyanyasaji kwa watoto kwa umakini mkubwa.

DIAMOND APANDA NA JENEZA JUKWAANI

Diamond akipozi na madansa wake siku alipoingia na jeneza katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, Dar.
Diamond ambaye wimbo wake mpya wa ‘Number One’ upo katika chati ya juu katika muziki huo, usiku wa kuamkia Jumapili iliyopita aliingia na jeneza hilo katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, Dar na kusababisha maswali mengi tata kutoka kwa mashabiki waliojazana kwenye onesho la Serengeti Fiesta 2013. 
ILIKUWA SAPRAIZI
Mapaparazi  waliokuwa wamejaa katika viwanja hivyo wakihakikisha wananasa matukio muhimu hasa yale ‘exclusive’, walipenyezewa mapema kuhusu Diamond kuingia na jeneza.
 Mtoa habari alisema Diamond aliingiza jeneza viwanjani humo kwa lengo la kupanda nalo jukwaani wakati akiimba wimbo wake uitwao Nikifa Kesho ambao mashabiki wake wengi wanasema amejichulia kifo.
 Kwa sharti la kutoandikwa jina lake , mtoa habari huyo ambaye ni mtu wa karibu na Diamond alisema:
“Diamond amekuja na jeneza, limefichwa kule nyuma wanakobadilishia nguo wasanii, atapanda nalo jukwaani. Anataka kuwafanyia sapraizi mashabiki wake.”
 SAPRAIZI YAKWAMA
Hata hivyo, baada ya matatizo ya kiufundi yaliyojitokeza, Diamond hakuweza kupanda jukwaani Jumamosi usiku huo na badala yake akatakiwa kupanda kesho yake Jumapili ambapo pia hakulitumia jeneza hilo kama mawazo yake ya awali yalivyokuwa.
Mapaparazi wetu walisaka sehemu lilipohifadhiwa jeneza hilo na kufanikiwa ambapo pia walikuta baadhi ya watu wakilishangaa na kuulizana maswali. 
MASWALI TATA
Nurdin Ali, mkazi wa Mbagala, Dar aliyeliona jeneza la Diamond alisema:
“Mimi namkubali sana huyu bwana mdogo lakini sasa mambo ya majeneza jukwaani ya nini tena?
 “Sikubaliani na hili suala. Hata wimbo wake wa Nikifa Kesho sioni kama una mantiki. Ni kama tu anajitabiria kifo. Anapita mlemle alimopita marehemu Kanumba, maana naye aliimba wimbo akielezea itakavyokuwa siku akifa, ikawa kweli.
“Lakini Diamond amekwenda mbele zaidi kwa kuamua kuja na jeneza kabisa stejini. Sijui amenunua au amekodisha, ila sikubaliani naye hata kidogo.” 
MATUMIZI YA JENEZA
Mwingine aliyekataa kuandikwa jina lake  alisema:
“Halafu kama lengo lake lilikuwa kuonesha uhalisia wa kifo katika wimbo wake, kwa nini asingekuja na jeneza la imani yake? Angalia, jeneza lina msalaba ambao unakubalika katika imani ya Kikristo, kwa nini asije na jeneza la Kiislamu au sanduku ambalo halina msalaba?”
 Akaongeza: Au inawezekana huyu jamaa anataka kubadili dini ili aoane na Penny (Penniel Mungilwa) ambaye ni Mkristo kwa sababu huku ni kukana imani yake kimyakimya.” 


 
ALIWAHI KUTANGAZA KUJENGA MSIKITI
Shabiki mwingine alikwenda mbali zaidi na kusema kama Diamond ni muumini mzuri wa Kiislamu tena mwenye lengo la kujenga msikiti kama alivyowahi kutangaza siku za nyuma, anatakiwa kutofungamana kabisa na ishara zinazoonesha anaunga mkono imani nyingine.
 “Anapaswa kuwa makini na mambo yake na awe na washauri wazuri, vinginevyo atakuwa anafanya mambo yanayoibua maswali mengi kwa jamii inayomwamini,” alisema shabiki huyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Jennifer. 
HUYU YUPO TOFAUTI
Shabiki aliyejitambulisha kwa jina la Hamadi Hajj (34) mkazi wa Kijitonyama, Dar alisema:
“Hakuna uhusiano wowote kati ya hili jeneza na mambo ya kubadilisha dini au kuiunga mkono. Kikubwa ni lengo alilotaka litimie. 
“Ukiachana na hilo, mambo mengine yako wazi jamani. Upatikanaji wa majeneza ya Kikristo ni rahisi zaidi tofauti na ya Kiislamu. Wabongo wanapenda sana kukuza mambo,”  alisema Hajj. 
Siku hiyohiyo, usiku huohuo, mapaparazi wetu walimbana Diamond kuhusu kutinga Leaders na jeneza ambapo alijitetea hivi:
“Ni swaga tu zile.”
Alipobanwa zaidi na kuulizwa ni swaga gani zinazochanganywa na vitu vinavyoashiria huzuni na imani ambayo si yake, alisema:
“Nilitaka kuwafurahisha mashabiki wangu na kuwapa uhalisia wa ule wimbo wangu wa Nikifa Kesho, sikuwa na nia ya kukashifu imani ya mtu.” 
FIESTA PART II
Baada ya shoo yake kushindikana na kuhamishiwa siku iliyofuata (Jumapili), timu yetu ilitinga viwanjani hapo ili kujua kama Diamond angepanda na jeneza hilo kama alivyotarajia lakini jeneza halikuwepo eneo lilipohifadhiwa awali.
Diamond alipofuatwa na kuulizwa kama mpango wake bado uko palepale, alijibu:
 “Lile jeneza nilipanga kupanda nalo jukwaani wakati nikiwa naimba wimbo wangu wa Nikifa Kesho lakini kwa bahati mbaya sikuweza kupanda kuimba kutokana na matatizo ya kiufundi, leo (Jumapili) nisingeweza kupanda nalo kwa kuwa muda tuliopewa ni mfupi sana,” alisema Diamond.
 Alipobanwa kuhusu kutumia jeneza la Kikristo na kuhusishwa na fununu za kubadili dini, alisema hana mpango huo kabisa.
“Naomba nieleweke, mimi sikuwa na nia tofauti zaidi ya kuwakilisha kilichopo katika wimbo wangu. Lengo lilikuwa kuonesha uhalisia tu wa kibao changu cha Nikifa Kesho, siyo zaidi ya hivyo,” alisema.
 Inasemekana kwamba Diamond aliamua kubadilisha uamuzi wake wa kupanda na jeneza jukwaani siku hiyo baada ya kunyetishwa na watu wanaomtakia mema kuwa asingeonesha picha nzuri kwa jamii, hasa kwa vile jeneza hilo lilikuwa na msalaba juu ya mfuniko.
 katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, Dar



WANANCHI WAONDOKA NA MIFUKO YOTE YA MBOLEA BAADA YA GARI GALI LILILOBEBA SHEHENA HIYO KUPATA AJALI



 Gari lenye namba T319BCU upande wa nyuma na Kichwa namba T885 CBS  aina ya Roli likiwa limepinduka
 Mbolea ikiwa imemwagika
 Gari lenye namba T319BCU upande wa nyuma na Kichwa namba T885 CBS  aina ya Roli upande wa mbele baada ya kupata ajali
 Wakazi Mbalimbali wakiwa wanashuhudia ajali hiyo
 Hii ndio Mbolea ambayo wananchi wameondoka  nayo yote
 Hili ni eneo Jirani na ajali ilipo tokea
Mabaki ya Mbolea hiyo.

Picha zote na Mbeya yetu

BABA YAKE DIAMOND AFURAHISHWA NA UAMUZI WA DIAMOND KURUDIANA NA WEMA.....ADAI KUWA PENNY HANA NYOTA YA KUWA NA MWANAYE..!!


Akizungumza na mwanahabari wetu juzikati, Baba Diamond alisema alifurahishwa mno na hatua ya mwanaye kurudiana na Wema kwani ndiye mwanamke anayejielewa na ana nyota kali tofauti na warembo wengine aliowahi kuwa nao.
 Wema ni mwanamke mwenye nyota kali sana na anapendwa na wengi. Siyo kama hao akina sijui Penny (Penniel Mungilwa).
 Hana majivuno hata mimi nilisema mwanzoni walipoachana kuwa Diamond alipoteza bahati lakini sasa naamini atafika mbali zaidi kwani kama siyo kuachana kwao, Diamond angekuwa mbali,” alisema.

 

Wema na Diamond.
 Hata hivyo, alimtaka Diamond kutulia na Wema kwani ndiye mwanamke sahihi kwake na aepuke kutangatanga kwani atashindwa kufanya mambo ya maana yatakayomuwezesha kuwa juu zaidi ya hapo alipo kwa sasa.
Baba mzazi wa Diamond, Abdul Jumaa

 Hivi karibuni Diamond alithibitisha kurudiana na Wema wakiwa China lakini alipotua Bongo akaendelea na uhusiano wake na Penny hivyo kuwaacha mashabiki wake njiapanda.



----GPL

KAPTAIN KOMBA AJITOA MHANGA NA KUSEMA "LOWASSA NDIO RAIS 2015"

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Kapteni Mstaafu, John Komba amevunja ukimya na kutamka wazi kuwa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, ndiye chaguo lake na atakuwa Rais ajaye uchaguzi wa 2015.

Komba anakuwa mtu wa pili kumtaja Lowassa hadharani kuwa anafaa kwa rais 2015.

Itakumbukwa Mbunge wa Viti Maalumu, Beatrice Shelukindo (CCM) naye alivunja ukimya baada ya kutangaza kumuunga mkono Lowassa kumrithi Rais Kikwete.

Shelukindo alitoa kauli hiyo wakati akiwasalimia wakazi wa Monduli baada ya kukaribishwa kuchangia ujenzi wa Hosteli ya KKKT, kwenye sherehe za kukaribisha Mwaka Mpya zilizofanyika nyumbani kwa Lowassa na kuhudhuriwa na makada kadhaa wa CCM.

Akizungumza na Mwananchi katika mahojiano maalumu jana, Komba ambaye ni Kiongozi wa Kundi la Uhamasishaji cha CCM Tanzania One Theatre (TOT Plus), alisema mtazamo wake kwa mtu anayefaa kumrithi Rais Jakaya Kikwete ni Lowassa.

Komba aliyeingia kwenye siasa kutokana na msukumo wa mama yake aliyekuwa msaidizi wa Bibi Titi Mohamed, alisema anazo sababu kuu tano za kumkubali Lowassa kuwa Rais na atasimama popote kumtetea.

“Nakuambia Lowassa ndiye anafaa kuwa Rais... unafikiri kuna mwingine. Nina sababu zangu tatu,” alisema Komba na kuhoji:

“Wewe unakwenda kwenye harambee, nani leo hii anaweza kusaidia kuchangia kwa fedha nyingi na zote hizo ni kwa maendeleo yanayokusudiwa kama siyo Lowassa?”

alisema Komba ambaye ni mahiri katika kuinadi CCM, katika kampeni mbalimbali za udiwani, ubunge na urais.Juu ya kuwa atakuwa katika wakati mgumu endapo anayempigia debe hatokuwa, Komba alisema: “Mimi sikwambii ni nani, lakini wapo Mawaziri waliomkana, lakini leo hii wapo kwenye Serikali hii hii ya Rais Kikwete.

“Mimi nasema Lowassa, na kama akipita sawa nitaburudiiika kwelikweli, lakini kama akiteuliwa mwingine, mimi nitakuwa naye...nitamwimbia hadi mwisho. Kazi yangu si unaijua, nitampigia debe kwa kuwa si mtu wa mtu mmoja, ni uteuzi wa wanaCCM ule si wa Komba.” alisema.

Mbali na kumnadi Lowassa, Komba alisifu uimara wa chama chake kuwa kinaimarika siku hadi siku na ndicho kinachotoa viongozi wa kweli na hata wananchi wanakikubali.


Akizungumzia suala la rushwa ndani ya CCM, Komba ambaye pia ni Mbunge wa Mbinga, alisema kama chama kuna watu wa aina nyingi, kuna wasafi, kuna wachafu lakini wote wako kwenye mstari mmoja.

Alisema kuwa vita ya rushwa ndani ya CCM itamalizika endapo kila kiongozi atasimamia kwenye haki na maadili ya uongozi na pia kutambua wajibu wake ndani ya chama.Komba alijipigia upatu kuwa ameleta maendeleo katika jimbo lake kwani jimbo linatazamika ikilinganisha na miaka ya nyuma kuwa wananchi walikuwa wakiishi maisha ya tabu na kimaskini ilhali wana 

MGANGA AKUTWA NA KIGANJA CHA BINADAMU AKIMUUZIA MTEJA WAKE KWA MILIONI 100 HUKO MWANZA..


Mtu mmoja jijini Mwanza anadaiwa kukamatwa na kiganja cha mtu akiwa anajiandaa kumuuzia mteja kwa sh million 100.

Washukiwa walikamatwa  jana  karibia na uwanja wa ndege wa Mwanza  wakifanya  biashara  hiyo  haramu.... 
 Baada  ya  upekuzi  wa  kina, mteja  alikuwa  ana  milioni  100  na mganga alikutwa  na   kiganja cha  binadamu  ambacho kilikuwa  kibichi kikitoa damu.
Kiganja  hicho  kilikuwa  kimevishwa  tunguri  na nywele za binadamu.

BABA ATUMIA PANGA NA RUNGU KUMWADHIBU MWANAYE KWA KOSA LA KUKATAA KWENDA SHULE


Victoria Mukama (10) baada ya matibabu


Mwalimu wa zamu wa Shule ya Msingi Airport, Damali Obadia alisema tukio hilo la ajabu lilitokea  majira ya saa mbili na nusu asubuhi ambapo akiwa ofisini alimuona mzazi huyo akiwa na mtoto huku akiendelea kumpiga wakielekea ofisini.

Mama mzazi wa binti huyo Teodora Paulo alisema yeye na mume wake hawakuwepo nyumbani ambapo baada ya kurejea kutoka Msibani majira ya asubuhi walimkuta binti yao hajaenda shule na walivyomuuliza sababu ya kutoenda shule alijibu alikuwa havioni viatu vyake.

majirani wa mtuhumiwa huyo walidai kuwa tabia ya Mwanaume huyo kufanya unyanyasaji inafichwa na mkewe ambaye anaonekana kuwa muoga wa kupigwa na mumewe na kuongeza kuwa anatabia ya kuandika makosa anayotendewa na mkewe.


 Victoria Mukama (10) baada ya matibabu 



KATIKA hali isiyokuwa ya Kawaida, Baba mmoja aliyejulikana kwa jina la Oscar Mukama  mkazi wa Isengo Airport Jijini Mbeya amemjeruhi vibaya binti yake Victoria Mukama (10) kwa kumpiga sehemu mbali mbali za mwili wake akitumia vifaa vyake vya ulinzi likiwemo Lungu.

Kwa mujibu wa Mwalimu wa zamu wa Shule ya Msingi Airport, Damali Obadia alisema tukio hilo la ajabu lilitokea  majira ya saa mbili na nusu asubuhi ambapo akiwa ofisini alimuona mzazi huyo akiwa na mtoto huku akiendelea kumpiga wakielekea ofisini.

Alisema mzazi huyo baada ya kufika walimu walimpokea na kumuuliza kwa nini anampiga kiasi hicho mtoto wake alijibu mtoto ni wa kwake mwenyewe na alizaa kwa manufaa yake hivyo haoni sababu ya kuulizwa kuhusu kipigo kwa mwanaye.

Aliongeza kuwa baada ya walimu kumweleza kuwa kitendo alichokifanya ni cha kinyama na hakipaswi kutendeka Mzazi huyo alitoa kisu na kuwatishia walimu ikiwa ni pamoja na kutoa matusi makali dhidi yao ambapo walimu walifanikiwa kumtuliza na kumuomba amwache mtoto ili walimu wamwadhibu.

Alisema baada ya mzee huyo kuondoka na kumwacha mtoto walimpigia simu mama wa mtoto ambaye baada ya kufika shule alizimia kutokana na hali aliyomkuta nayo mtoto wake ambapo Walimu walitoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Mtaa kasha kwenda Polisi kuchukua Fomu namba tatu (PF3) kwa ajili ya matibabu.

Mama mzazi wa binti huyo Teodora Paulo alisema yeye na mume wake hawakuwepo nyumbani ambapo baada ya kurejea kutoka Msibani majira ya asubuhi walimkuta binti yao hajaenda shule na walivyomuuliza sababu ya kutoenda shule alijibu alikuwa havioni viatu vyake.

Alisema baada ya kumsaidia kutafuta na kutofanikiwa kuviona baba yake ambaye nayeb alikuwa amejiandaa kwa ajili ya kwenda kazini kwake anakofanya kazi ya Ulinzi alimwamuru mwanaye kuvaa sare za shule na kwenda naye hivyo hivyo kwa kile alichodai anampeleka shule.

Alisema alishikwa na butwaa hadi kupoteza fahamu baada ya kumkuta mtoto amejeruhiwa huku akiwa amepigiwa simu na mumewe kwamba aende shule kumchukua mtoto wake lakini hakujua kama amepigwa kiasi cha kumjeruhi mtoto sehemu mbali mbali za mwili wake.

Akizungumzia kisa cha kupigwa kwake baada ya kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya katika Chumba cha dharula, Victoria Mukama (10) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la nne katika Shule ya Msingi Airport alisema wakiwa njiani kuelekea shuleni alishangaa akianza kupigwa bila kuelezwa sababu ni nini.

Alisema alianza kupigwa tangu wanatoka nyumbani hadi wanafika shule iliyoumbali wa Mita 250 kutoka Nyumbani hadi Shuleni akitumia Virungu na fimbo huku akiwa ameshika kisu mkononi kwa ajili ya kuwatishia wanataka kumuokoa.

Kutokana na tukio hilo Jeshi la Polisi linaendelea kumtafuta Mtuhumiwa huyo wa unyanyasaji wa watoto baada ya kufunguliwa kwa jarada lenye namba MB/IR/9563/2013 katika kituo cha kati cha Polisi Mbeya.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Pambogo Esia Edward ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Shule hiyo alisema kitendo kilichofanywa na mtuhumiwa huyo hitendo hakipaswi kufumbiwa macho hivyo ni lazima sheria ichukue mkondo wake kwa kuhakikisha vitendo hivyo vinakomeshwa ndani ya jamii.

Aliongeza kuwa hajawahi kusikia mtuhumiwa huyo kama amewahi kujihusisha na ukatili wa namna hiyo na kuongeza kuwa huwa anatoa ushirikiano vizuri katika ngazi ya mtaa na kuhudhuria vikao mbali mbali vinavyoitishwa pamoja na kuchangia mada.

Nao majirani wa mtuhumiwa huyo walidai kuwa tabia ya Mwanaume huyo kufanya unyanyasaji inafichwa na mkewe ambaye anaonekana kuwa muoga wa kupigwa na mumewe na kuongeza kuwa anatabia ya kuandika makosa anayotendewa na mkewe.

Walisema awali amewahi kuoa mke na kuzaa nae watoto watatu lakini mkewe huyo alikimbia baada ya kuona tabia ya unyanyasaji imezidi kutoka kwa Mwanaume huyo aliyetajwa kuwa ni jamii ya watu wa Mosoma Mkoani Mara ambako tabia kandamizi dhidi ya wanawake na watoto bado zinafanyika.

CREDIT: MBEYA YETU

MTOTO WA LUKUVI AJERUHIWA KWA UJANGILI

MTOTO wa kaka wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera, Uratibu na Bunge, Willium Lukuvi, aitwaye Tomm Malenga, ambaye ni katibu wake, amejeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili wake baada ya kukamatwa kwa tuhuma za kuhusishwa na ujangili.
Habari zilizopatikana mjini hapa, juzi Jumapili, Oktoba 27, mwaka huu, zinasema akiwa ofisini kwake siku hiyo, Tomm alifuatwa na maofisa wa Wanyama Pori kwa kile kilichotajwa kuwa anahusika na ujangili.
“Walifika na kumkamata kisha wakaanza kumpiga, tena palepale ofisini kwa Lukuvi. Amevunjika vidole vya mguu na mkono wake mmoja hauko sawa baada ya kipigo hicho,” alisema mtoa habari wetu.
Tomm hakupatikana ili kuzungumzia sakata hilo lakini waziri Lukuvi alifafanua baada ya kuzungumza na mwandishi wetu ambapo alisema kilichofanyika anakijua na kwamba ni njama za wabaya wake.
“Sikiliza bwana, licha ya Tomm kuwa msaidizi wangu wa jimboni ni mtoto wa marehemu kaka yangu. Wanasema eti ametajwa kwenye ujangili; sasa kutajwa tu, unawezaje kwenda kumchukua mtu ofisini kwake, tena kwa kumpiga? Huo siyo utawala wa kisheria,” alisema waziri Lukuvi.
Alisema, mtu aliyemtaja Tomm ni Gedi ambaye alikuwa wa kwanza kukamatwa kwa ujangili na akasema amekuwa akishirikiana na mwanaye.
“Ukweli ni kwamba huyo Gedi ana usongo na mimi, kwani huwa ananipinga tangu mwaka 1995. Aliwahi kugombea udiwani, tukagundua kuwa ni Msomali, tukamfuta. Nadhani anatumia mwaya huo kunichafu mimi na familia yangu,” alisema Lukuvi.

Friday 25 October 2013

CHANGUDOA AMUUMBUA MUME WA MTU HADHARANI



OKTOBA 19, 2013 ilikuwa  ya aibu kwa mmiliki wa gari aina ya Noah kufuatia kuangushiwa varangati na kahaba ambaye jina lake halikupatikana mara moja baada ya mmiliki huyo ambaye ni mume wa mtu kula naye uroda kisha kutaka kumfanyia kitu mbaya.
Tukio hilo lililojaza watu kibao, lilitokea usiku wa saa 5:19 Jumapili iliyopita ambapo kikosi cha Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ kikiwa katika ‘patroo’ ya kunasa matukio ya usiku.
Ilikuwa wakati OFM wakipita eneo hilo, walikuta umati ukiwa umelizunguka gari hilo huku kahaba huyo akianika ya ‘chumbani zaidi’.



Alisema: (huku ameshika jiwe) nakwambia sikubali, huwezi kunifanyia hivi. Wewe umelala na mimi kwenye gari kule halafu unakuja hapa unanitenda hivi? Jaribu kuondoa gari uone nitakavyovunja vioo.
OFM: Kwani dada ilikuwaje?
Kahaba: (huku akilia) Huyu baba amelala na mimi kule (hakutaja jina) tena ndani ya gari lake, si angalieni muone kile kiti cha upande wa abiria kilivyolala. Tumemaliza, tumekuja wote kufika hapa akanisukumia nje, nikaangukia nje na kuumia mkono. Ndiyo nikaokota jiwe ili nivunje vioo vya gari lake.

Mume wa mtu: Sasa wewe unapiga kelele za nini? Elfu kumi yako si nimekupa? Unataka nini tena, au lengo lako kunivunjia heshima?
Kahaba: Umenipa ndiyo, nataka hela ya kwenda kujitibia huu mkono ulioniumiza, nataka matibabu tu mimi.

Kahaba huyo alionesha sehemu ya mkono inayovuja damu. Aliumia baada ya kuanguka kwa kusukumwa na mwanaume huyo.
Mwanaume huyo alitaka kuondoka kwa kuwasha gari, lakini OFM wakamzuia wakimtaka asubiri polisi kwa vile msichana huyo aliumia kiganja cha mkono wa kushoto.

Mume wa mtu: (huku akimnong’oneza sikioni OFM) jamani sikieni, tumalizane kiume. Unajua mimi nina mke na watoto, sasa kusubiri polisi hamuoni kama nitaumbuka mwenzenu?
OFM: Hamna, hatuzungumzii biashara yenu mliioifanya ndani ya gari, hapa tunasimamia majeraha ya mkono uliyomsababishia.
Mashuhuda mbalimbali nao waliunga mkono OFM kwamba, mwanaume huyo asiondoke mpaka polisi wafike kushughulikia tatizo lao.
Ndipo mwanaume huyo bila kujua anaoongea nao ni OFM, alisema:

“Sawa, tusubiri polisi lakini no media (akimaanisha amekubali kusubiri polisi lakini kusiwepo wanahabari).
OFM: Ndiyo, no media, lakini polisi wanakuja sasa hivi.
Ndani ya dakika saba, mwanaume huyo alishangaa akipigwa picha na paparazi mmoja wa OFM aliyeliwahi tukio akitokea Sinza-Makaburini, Dar alikokuwa akifanya kazi nyingine za OFM.

Alipoona mwanga wa kamera ukimmulika mara kadhaa, mwanaume huyo aliingia ndani ya gari na kuondoka kwa kasi huku wananchi wakimzomea.
Cha ajabu, kahaba huyo naye alipoona mwanga wa kamera alianza kuondoka huku akisema haogopi kupigwa picha.

DANGURO LA MADENTI LAFUMULIWA

Na Waandishi Wetu
Vijana wa Kamishina wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP Suleiman Kova kwa kushirikiana na Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers wamefanikiwa kulifumua danguro linalodaiwa kufuga madenti wa vyuo mbalimbali jijini Dar.
Madenti hao walikamatwa mwanzoni mwa wiki hii kwenye danguro hilo lililopo ndani ya baa maarufu iliyopo maeneo ya Buguruni-Sokoni, Dar.

KERO
Awali kikosi kazi cha OFM kilipokea malalamiko kutoka kwa wazazi waishio maeneo hayo wakilalamikia ufuska wa kutisha unaofanyika kwenye danguro hilo.
Mzazi:Halooo…nazungumza na OFM?
OFM: Ndiyo…tukusaidie nini?

Mzazi: Mna habari?
OFM: Tunazo nyingi lakini ukitupatia ya kwako tutaifanyia kazi ipasavyo.
Mzazi: Tunawaamini OFM mnatisha kama njaa. Sisi ni wazazi wa hapa Buguruni-Sokoni. Kuna danguro hapa kwa kweli yanayofanyika ni aibu tupu. Tunaomba mje mjionee wenyewe mfanye kazi yenu.
OFM: Nini hasa kinafanyika?

Mzazi: Yaani vitendo vya ngono vinafanyika na sasa hivi hata kwa nje wapo watu wanafanya biashara haramu ya ngono hivyo watoto wetu wanashuhudia vitu vya ajabu na kondomu zimezagaa kila kona.
OFM: Sawa, tuachie tufanye kazi yetu.

Mzazi: Oke, lakini naomba chondechonde msinitaje wala kuonesha namba yangu kwa sababu hii ni biashara ya watu nitamwagiwa tindikali bure!
OFM: Tunaheshimu vyanzo vyetu hatuwezi kukutaja popote kwani siyo maadili ya kazi yetu.

OFM KAZINI
Kabla ya kuwataarifu polisi juu ya kero hiyo kwa wakazi wa eneo hilo, vijana wa OFM waliingia kazini ili kujikusanyia ushahidi ambapo walipofika walishuhudia vitendo hivyo vikifanyika mchana kweupe bila kujali kama kuna serikali.
Baadhi ya makachero wa OFM walijifanya wauzaji na wengine wanunuaji ambapo walijikusanyia data za kutosha huku wakiwarekodi wahusika (madenti wanaojiuza na wanaume wanaowanunua) kwa kutumia vifaa vya kazi bila wao kushtuka.

BEI
Kuhusu bei, wapo wa bei chee kuanzia buku mbili hadi tano na wa bei mbaya ambao siyo wengi, wao wakianzia dau la elfu kumi na kuendelea.
Mmoja wa vijana hao wa OFM alifanikiwa kuingia ndani baada ya kukubaliana bei na mmoja wa wauzaji ambapo alipofika na kujionea mazingira halisi aliahirisha kwa kigezo kuwa alikuwa amepokea simu ya dharura.

USHUHUDA MBAYA
Hata hivyo, alichokishuhudia ndani, anasimulia: “Nilishuhudia watu wakiwa kwenye ‘pea’ wakijiachia kwa ngono na suala la kondom ilikuwa ni uamuzi wa mtu.
“Kondom zilizotumika zilikuwa zimezagaa kila kona yaani nilihisi mwili kunisisimka na kuwaza sana juu ya janga la Ukimwi. Kwa hali ile tumekwisha.”

TAARIFA POLISI
Ili kufanikisha zoezi la kulifumua danguro hilo, OFM iliwasiliana na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi na kumweleza mchezo mzima wa uchafu unaofanyika eneo hilo.

Bila kusita, kamanda huyo aliteua vijana wake kutoka Kituo Cha Buguruni ambao walitekeleza kwa kiwango cha oparesheni hiyo maalum.
Walipofika eneo la tukio, polisi hao waliwakamata wahusika wote akiwemo mmiliki wa biashara hiyo.

DENTI IFM
Wakati watuhumiwa hao wakihenyeshwa na polisi, mmoja wa madenti hao anayesoma Chuo cha IFM, Peter Davis alisema kwa upande wake aliamua kuweka makazi yake ndani ya chumba kimoja cha danguro hilo.

Katika utetezi wake, denti huyo alidai kuwa aliamua kuishi hapo kwa kuwa mazingira hayo ni mazuri kwake kwa ajili ya kujisomea.
Mwingine aliyenaswa ndani ya kiwanja hicho cha maasi ni denti aliyejitambulisha kwa jina la Mwanahamisi (hakutaja chuo) ambaye alidai kuwa tangu siku hiyo atauacha uchangudoa na kuapa kuwa akiachiwa huru ataenda kusoma kwa bidii.

Denti mwingine aliyekamatwa katika msala huo alijitambulisha kwa jina moja la Angel ambaye alidai kuwa anasoma chuo kimoja kilichopo Kariakoo, Dar na wengine hawakutaja majina zaidi ya kukiri kuwa ni wanafunzi.

MUUZA KONDOM NAYE MBARONI
Ndani ya gesti hiyo pia alinaswa njemba mmoja aliyekuwa ameweka maskani na kazi yake kubwa ilikuwa kuuza kondom kwa madenti hao ambao humwingizia kipato chapuchapu.

Hata hivyo, jamaa huyo alitiwa mbaroni kwa uchunguzi zaidi.
Mbali na oparesheni hiyo, pia polisi hao waliendeleza msako maeneo mengine ya Buguruni ambapo dadapoa kibao walikamatwa huku mmoja akiangua kilio na kutamani kujiua kuliko mumewe kujua kuwa anauza mwili.

NYUMA YA NONDO
Baada ya kuhojiwa kuhusika na biashara haramu ya ngono na kukiri, watuhumiwa hao wote waliwekwa nyuma ya nondo kwenye Kituo cha Polisi cha Buguruni na kufunguliwa jalada la kesi namba BUG/RB/13114/2013 - UMALAYA, wakisubiri sheria kuchukua mkondo wake.

WAZAZI SOMENI HAPA
Uchunguzi wa gazeti hili ulionesha kuwa madenti hao na wengine wengi jijini Dar, wamekuwa wakiaga kwao kuwa wanakwenda masomoni lakini kumbe wanaishia kwenye madanguro yaliyojazana jijini kwa ajili ya kujiuza.

Huku wazazi wakitoa fedha nyingi na huduma nyingine wakiamini watoto wao wanasoma, hali ni tofauti kwani madenti wengi wamekuwa wakiishia kwenye vitendo vya kihuni na kufeli masomo na maisha kwa jumla kisha kugeuka mzigo kwa familia.
Gazeti hili linawataka wazazi kufuatilia mienendo ya watoto wao wanaowasomesha ili kuwakanya juu ya kujiingiza kwenye uhuni ambao huhatarisha maisha yao -Mhariri.

AJALI MBAYA MKOANI IRINGA, WATU 38 WAJERUHIWA



Daladala aina ya Toyota Coaster lenye namba za usajili T 960 AQY linalofanya safari zake mjini Iringa mara baada ya kugongana na lori aina ya Isuzu lenye namba za usajili SM 3363 katika Mlima wa Ipogolo eneo la Kisima cha Bibi mkoani Iringa.
 
l_dd9a2.jpg
m_74746.jpg
Taxi ambayo nayo ilihusishwa katika ajali hiyo ikiwa eneo la tukio, huku askari polisi wakilinda usalama wa mali za abiria.
n_7bc78.jpg
Wananchi wa mji wa Iringa wakitazama ajali hiyo katika mlima wa Ipogolo.
 
o_fbf87.jpg
Coaster likiwa nyang'anyang'a baada ya ajali hiyo ambayo imejeruhi watu zaidi ya 38.
ZAIDI ya abiria 38 wamejeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari manne mjini Iringa, baada ya daladala aina ya Toyota Coaster lenye namba za usajili T 960 AQY linalofanya safari zake mjini Iringa kufeli breki na kuyagonga magari matatu.
Ajali hiyo limetokea katika mlima wa Ipogolo, eneo maarufu mjini Iringa kama "Kisima cha bibi" jana baada ya Coaster kuyavaa magari matatu ambayo ni lori aina ya Isuzu la Manispaa ya Iringa, Tax pamoja na Hiace.
Majeruhi 38 katika ajali hiyo wamelazwa kwenye Hospitali ya Rufaa mkoani Iringa.
Akizungumzia hali ya majeruhi wa tukio hilo, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa mkoa wa Iringa, Dk. Deogratius Manyama amesema wamepokea majeruhi 38 na waliolazwa ni 8 huku majeruhi watatu wakiwa na hali mbaya na kuwa majeruhi wengi wameumia zaidi kichwani na kifuani, huku majeruhi 27 wakiruhusiwa kurudi nyumbani kutokana na kutokuwa na majeraha makubwa.

USWISS YAKUBALI KUYAREJESHA MABILIONI YALIYOFICHWA HUKO.



Sakata la vigogo kuficha mabilioni ya shilingi katika benki za Uswisi, limechukua sura mpya baada ya Serikali ya nchi hiyo kutunga sheria inayowabana walioweka fedha kwenye benki zake kuzithibitisha, la sivyo zitarejeshwa katika nchi husika. 
  
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe alifanya mazungumzo na Serikali ya nchi hiyo ambayo imemweleza kuwa imebadili sheria zake ili kuwadhibiti wageni wanaoficha fedha nchini humo.
 
 
Akizungumza na Mwananchi , Zitto alisema amepata taarifa hizo juzi baada ya kukutana na Waziri wa Fedha wa nchi hiyo ambaye alimwandalia mazungumzo na watalaamu wake.
 
 
Alibainisha kuwa tangu kuibuka kwa sakata hilo mwaka 2012 na Bunge kuiagiza Serikali kufuatilia, Serikali haijaomba taarifa yeyote kutoka Uswisi kuhusu Watanzania waliohifadhi fedha nchini humo.
 
 
“Jana nilikutana na Waziri wa Fedha na akatuacha na mazungumzo na wataalamu wake. Wamesema hadi sasa, Tanzania haijasaini mkataba wa kubadilishana taarifa za kikodi (Multilateral convention on administrative assistance in tax matters),” alisema Zitto na kuongeza;
 
 
“Kwa kutosaini, Tanzania inajinyima haki ya kupata taarifa hizi na kutoza kodi kwa watu walioficha fedha huku (Uswisi), maana Sheria ya Kodi ya Tanzania inataka kila Mtanzania popote anapopata kipato halali lazima alipe kodi.”
 
 
Zitto alieleza kuwa kitendo cha Serikali ya Uswisi kubadili sheria zake, kinaiwezesha nchi hiyo kutoa taarifa za benki za watu walioweka fedha nchini humo wakiwamo Watanzania, ambao sasa watatakiwa kuthibitisha kama fedha hizo ni safi au la.
 
 
“Kiufupi, Tanzania haijaomba taarifa yeyote kutoka Uswisi. Ila Uswisi wamebadili sheria yao na sasa mmiliki wa fedha ndiyo anapaswa kuthibitisha kwamba ni safi, na ikithibitika kuwa hazina mwenyewe wala maelezo, zitarudishwa nchi husika,” alisema.
 
 
Zitto alisema mbali na kukutana na watendaji hao wa Serikali amezungumza na Umoja wa Mabenki wa nchi hiyo uliobainisha kuwa Uswisi ina Watanzania wachache wenye fedha.
 
 
“Wamesema Watanzania wengi wana fedha Uingereza, Jersey, Cayman Islands na Mauritius. Dubai pia imetajwa sana,” alisema Zitto.

 Zitto alielezea kuwa umoja huo wa benki za Uswisi umeanzisha mkakati wa kusafisha fedha uitwao ‘clean money strategy’, na wamegundua watu wengi ambao ni wanasiasa, wamezuia akaunti zao na kupeleka majina kwenye Serikali zao.
 
 
“Tanzania haijafanya maombi rasmi hapa Uswisi na hivyo wao kama benki hawawezi tu kutoa taarifa bila kuombwa. 

Sheria yao imerekebishwa ambapo sasa ni wajibu wa mwenye akaunti kusema kama fedha zake ni halali au hapana,” alisema Zitto na kuongeza.
 
 
Hivi sasa hawapokei pesa kutoka nchi za Afrika au wanapokea kwa tahadhari sana, maana kuna reputational risk (kupoteza heshima),” alisema.

Wito wa timu ya uchunguzi
Zitto alipendekeza timu iliyoundwa kuchunguza fedha hizo itoe taarifa yake kwenye Mkutano wa Bunge unaoanza Oktoba 29, mwaka huu, akieleza kuwa, “Kuendelea kukaa na taarifa, kutaongeza tetesi za kweli au za uwongo.”
 
Alisema mpango huo wa kusaka fedha zilizofichwa nchini Uswisi, umelenga zile zilizofichwa na watu binafsi kutokana na rushwa au kuuza dawa za kulevya na kampuni kubwa za kimataifa.
 
Alibainisha kuwa wengi waliotambulika ni wanasiasa, vigogo wa jeshi na wakuu wa mashirika ya umma na watendaji wa Serikali.
 
“Katika mabenki ya Uswisi, kuna kiasi cha Dola za Marekani 197 milioni. Fedha nyingi zipo katika benki za Uingereza na visiwa vyake, Dubai na Mauritius,” alisema na kuongeza;
 
“Wapo watu waliopata fedha kihalali, lakini wanaficha fedha hizo na mali zao nje ili kukwepa kodi. Wengi wa hao ni wafanyabiashara wakubwa nchini. Tanzania inapoteza Dola za Marekani 1.25 bilioni kati ya mwaka 2001 na 2012 kwa njia hizi.”
 
Alibainisha kuwa Tanzania lazima itunge sheria ya kufilisi mali ambazo mtu anashindwa kuthibitisha amezipataje.
“Tayari ninafanyia kazi muswada binafsi wa sheria wa kubadilisha sheria ya makosa ya jinai ya mwaka 1991. 

Wasaidizi wangu wanafanyia kazi muswada huo ili usomwe kwa mara ya kwanza kwenye mkutano wa Bunge unaonza Oktoba 29 na kueleza kuwa sheria ya sasa ina upungufu,” alisema.
 
Madai hayo ya Zitto yamekuja ikiwa umepita mwaka mmoja tangu Bunge kuipa Serikali muda wa kuchunguza sakata la vigogo walioficha mabilioni katika benki za Uswisi.
 
Zitto ndiye aliibua sakata hilo mwishoni mwa mwaka 2012. Kufuatia hoja hiyo, Serikali iliunda timu kutokana na Azimio la Bunge lililotolewa mwishoni mwa mwaka jana.

Werema ahoji...

Ni Bunge? 
Timu hiyo inayongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema ambaye jana baada ya kutafutwa na gazeti hili alisema, “Uchunguzi kuhusu walioficha fedha Uswisi bado haujakamilika.”
 
Viongozi wengine wanaounda tume hiyo ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hosea, Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Othman Rashid na Gavana wa Benki Kuu (BoT), Profesa Benno Ndulu.
 
Alipoulizwa kama kuna uwezekano wa ripoti hiyo kuwekwa wazi katika Mkutano ujao wa Bunge, Werema alisema, “Kwa nini, kwani wewe ndiyo Bunge. Uchunguzi bado unaendelea”

Hata hivyo, kwa mujibu wa agizo la Bunge, tume hiyo inatakiwa kuwa imekamilisha uchunguzi wake mwezi huu na kuwasilisha ripoti yake katika mkutano huo wa Bunge.
 
Alipoulizwa kuhusu ripoti hiyo, Naibu Spika, Job Ndugai alisema, “Wiki ijayo katika kikao cha Kamati ya Uongozi, Serikali itatakiwa kutoa taarifa za uchunguzi huo na kama haujakamilika kikao hicho kitaamua jambo la kufanya na endapo uchunguzi utakuwa umekamilika zitapangwa taratibu za kuiwasilisha ripoti bungeni.”
 
Waziri wa Fedha anena
Naye Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa alisema jana kuwa sheria za kimataifa zipo wazi kwamba fedha chafu zinazogundulika kufichwa nchi fulani, hurejeshwa katika Serikali ya nchi husika.
 
“Lengo la sheria hizi za kimataifa ni kuhakikisha kuwa fedha za wizi zinazoibwa nchi fulani, haziwezi kuhifadhiwa katika nchi nyingine,” alisema.
 
Alipoulizwa kama wizara yake ina taarifa zozote kuhusu Watanzania walioficha fedha Uswisi alisema, “Kuna Tume iliundwa na Bunge kufuatilia suala hilo nadhani ndiyo itakuwa na majibu sahihi.”
 
Uchunguzi wa walioficha mabilioni ya Uswisi uliibuka baada ya Benki ya Taifa ya Uswiss (SNB) kutoa taarifa mapema Juni 2012 kuhusu raia wa kigeni wanaomiliki akaunti za benki nchini humo.
 
Orodha hiyo inadaiwa kuwa na majina ya baadhi ya Watanzania wenye akaunti zinazofikia Dola milioni 196 za Marekani ambazo ni sawa na Sh323.4 bilioni.

-Mwananchi