Sakata la vigogo kuficha mabilioni ya shilingi katika benki za Uswisi, limechukua sura mpya baada ya Serikali ya nchi hiyo kutunga sheria inayowabana walioweka fedha kwenye benki zake kuzithibitisha, la sivyo zitarejeshwa katika nchi husika.
Mbunge
wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe alifanya mazungumzo na Serikali ya
nchi hiyo ambayo imemweleza kuwa imebadili sheria zake ili kuwadhibiti
wageni wanaoficha fedha nchini humo.
Akizungumza
na Mwananchi , Zitto alisema amepata taarifa hizo juzi baada ya
kukutana na Waziri wa Fedha wa nchi hiyo ambaye alimwandalia mazungumzo
na watalaamu wake.
Alibainisha
kuwa tangu kuibuka kwa sakata hilo mwaka 2012 na Bunge kuiagiza
Serikali kufuatilia, Serikali haijaomba taarifa yeyote kutoka Uswisi
kuhusu Watanzania waliohifadhi fedha nchini humo.
“Jana
nilikutana na Waziri wa Fedha na akatuacha na mazungumzo na wataalamu
wake. Wamesema hadi sasa, Tanzania haijasaini mkataba wa kubadilishana
taarifa za kikodi (Multilateral convention on administrative assistance
in tax matters),” alisema Zitto na kuongeza;
“Kwa
kutosaini, Tanzania inajinyima haki ya kupata taarifa hizi na kutoza
kodi kwa watu walioficha fedha huku (Uswisi), maana Sheria ya Kodi ya
Tanzania inataka kila Mtanzania popote anapopata kipato halali lazima
alipe kodi.”
Zitto
alieleza kuwa kitendo cha Serikali ya Uswisi kubadili sheria zake,
kinaiwezesha nchi hiyo kutoa taarifa za benki za watu walioweka fedha
nchini humo wakiwamo Watanzania, ambao sasa watatakiwa kuthibitisha
kama fedha hizo ni safi au la.
“Kiufupi,
Tanzania haijaomba taarifa yeyote kutoka Uswisi. Ila Uswisi wamebadili
sheria yao na sasa mmiliki wa fedha ndiyo anapaswa kuthibitisha kwamba
ni safi, na ikithibitika kuwa hazina mwenyewe wala maelezo,
zitarudishwa nchi husika,” alisema.
Zitto
alisema mbali na kukutana na watendaji hao wa Serikali amezungumza na
Umoja wa Mabenki wa nchi hiyo uliobainisha kuwa Uswisi ina Watanzania
wachache wenye fedha.
“Wamesema Watanzania wengi wana fedha Uingereza, Jersey, Cayman Islands na Mauritius. Dubai pia imetajwa sana,” alisema Zitto.
Zitto alielezea kuwa umoja huo wa benki za Uswisi umeanzisha mkakati wa kusafisha fedha uitwao ‘clean money strategy’, na wamegundua watu wengi ambao ni wanasiasa, wamezuia akaunti zao na kupeleka majina kwenye Serikali zao.
Zitto alielezea kuwa umoja huo wa benki za Uswisi umeanzisha mkakati wa kusafisha fedha uitwao ‘clean money strategy’, na wamegundua watu wengi ambao ni wanasiasa, wamezuia akaunti zao na kupeleka majina kwenye Serikali zao.
“Tanzania haijafanya maombi rasmi hapa Uswisi na hivyo wao kama benki hawawezi tu kutoa taarifa bila kuombwa.
Sheria yao imerekebishwa ambapo sasa ni wajibu wa mwenye akaunti kusema kama fedha zake ni halali au hapana,” alisema Zitto na kuongeza.
Sheria yao imerekebishwa ambapo sasa ni wajibu wa mwenye akaunti kusema kama fedha zake ni halali au hapana,” alisema Zitto na kuongeza.
Hivi
sasa hawapokei pesa kutoka nchi za Afrika au wanapokea kwa tahadhari
sana, maana kuna reputational risk (kupoteza heshima),” alisema.
Werema ahoji...
Ni Bunge?
Hata hivyo, kwa mujibu wa agizo la Bunge, tume hiyo inatakiwa kuwa imekamilisha uchunguzi wake mwezi huu na kuwasilisha ripoti yake katika mkutano huo wa Bunge.
Wito wa timu ya uchunguzi
Zitto
alipendekeza timu iliyoundwa kuchunguza fedha hizo itoe taarifa yake
kwenye Mkutano wa Bunge unaoanza Oktoba 29, mwaka huu, akieleza kuwa,
“Kuendelea kukaa na taarifa, kutaongeza tetesi za kweli au za uwongo.”
Alisema
mpango huo wa kusaka fedha zilizofichwa nchini Uswisi, umelenga zile
zilizofichwa na watu binafsi kutokana na rushwa au kuuza dawa za
kulevya na kampuni kubwa za kimataifa.
Alibainisha kuwa wengi waliotambulika ni wanasiasa, vigogo wa jeshi na wakuu wa mashirika ya umma na watendaji wa Serikali.
“Katika
mabenki ya Uswisi, kuna kiasi cha Dola za Marekani 197 milioni. Fedha
nyingi zipo katika benki za Uingereza na visiwa vyake, Dubai na
Mauritius,” alisema na kuongeza;
“Wapo
watu waliopata fedha kihalali, lakini wanaficha fedha hizo na mali zao
nje ili kukwepa kodi. Wengi wa hao ni wafanyabiashara wakubwa nchini.
Tanzania inapoteza Dola za Marekani 1.25 bilioni kati ya mwaka 2001 na
2012 kwa njia hizi.”
Alibainisha kuwa Tanzania lazima itunge sheria ya kufilisi mali ambazo mtu anashindwa kuthibitisha amezipataje.
“Tayari ninafanyia kazi muswada binafsi wa sheria wa kubadilisha sheria ya makosa ya jinai ya mwaka 1991.
Wasaidizi wangu wanafanyia kazi muswada huo ili usomwe kwa mara ya kwanza kwenye mkutano wa Bunge unaonza Oktoba 29 na kueleza kuwa sheria ya sasa ina upungufu,” alisema.
Wasaidizi wangu wanafanyia kazi muswada huo ili usomwe kwa mara ya kwanza kwenye mkutano wa Bunge unaonza Oktoba 29 na kueleza kuwa sheria ya sasa ina upungufu,” alisema.
Madai
hayo ya Zitto yamekuja ikiwa umepita mwaka mmoja tangu Bunge kuipa
Serikali muda wa kuchunguza sakata la vigogo walioficha mabilioni
katika benki za Uswisi.
Zitto
ndiye aliibua sakata hilo mwishoni mwa mwaka 2012. Kufuatia hoja hiyo,
Serikali iliunda timu kutokana na Azimio la Bunge lililotolewa mwishoni
mwa mwaka jana.
Werema ahoji...
Ni Bunge?
Timu
hiyo inayongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema
ambaye jana baada ya kutafutwa na gazeti hili alisema, “Uchunguzi
kuhusu walioficha fedha Uswisi bado haujakamilika.”
Viongozi
wengine wanaounda tume hiyo ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hosea, Mkurugenzi wa Usalama
wa Taifa, Othman Rashid na Gavana wa Benki Kuu (BoT), Profesa Benno
Ndulu.
Alipoulizwa
kama kuna uwezekano wa ripoti hiyo kuwekwa wazi katika Mkutano ujao wa
Bunge, Werema alisema, “Kwa nini, kwani wewe ndiyo Bunge. Uchunguzi
bado unaendelea”
Hata hivyo, kwa mujibu wa agizo la Bunge, tume hiyo inatakiwa kuwa imekamilisha uchunguzi wake mwezi huu na kuwasilisha ripoti yake katika mkutano huo wa Bunge.
Alipoulizwa
kuhusu ripoti hiyo, Naibu Spika, Job Ndugai alisema, “Wiki ijayo katika
kikao cha Kamati ya Uongozi, Serikali itatakiwa kutoa taarifa za
uchunguzi huo na kama haujakamilika kikao hicho kitaamua jambo la
kufanya na endapo uchunguzi utakuwa umekamilika zitapangwa taratibu za
kuiwasilisha ripoti bungeni.”
Waziri wa Fedha anena
Naye
Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa alisema jana kuwa sheria za
kimataifa zipo wazi kwamba fedha chafu zinazogundulika kufichwa nchi
fulani, hurejeshwa katika Serikali ya nchi husika.
“Lengo
la sheria hizi za kimataifa ni kuhakikisha kuwa fedha za wizi
zinazoibwa nchi fulani, haziwezi kuhifadhiwa katika nchi nyingine,”
alisema.
Alipoulizwa
kama wizara yake ina taarifa zozote kuhusu Watanzania walioficha fedha
Uswisi alisema, “Kuna Tume iliundwa na Bunge kufuatilia suala hilo
nadhani ndiyo itakuwa na majibu sahihi.”
Uchunguzi
wa walioficha mabilioni ya Uswisi uliibuka baada ya Benki ya Taifa ya
Uswiss (SNB) kutoa taarifa mapema Juni 2012 kuhusu raia wa kigeni
wanaomiliki akaunti za benki nchini humo.
Orodha hiyo inadaiwa kuwa na majina ya baadhi ya Watanzania wenye akaunti zinazofikia Dola milioni 196 za Marekani ambazo ni sawa na Sh323.4 bilioni.
-Mwananchi
-Mwananchi
No comments:
Post a Comment