Daladala aina ya Toyota
Coaster lenye namba za usajili T 960 AQY linalofanya safari zake mjini
Iringa mara baada ya kugongana na lori aina ya Isuzu lenye namba za
usajili SM 3363 katika Mlima wa Ipogolo eneo la Kisima cha Bibi mkoani
Iringa.
Taxi ambayo nayo ilihusishwa katika ajali hiyo ikiwa eneo la tukio, huku askari polisi wakilinda usalama wa mali za abiria.
Wananchi wa mji wa Iringa wakitazama ajali hiyo katika mlima wa Ipogolo.
Coaster likiwa nyang'anyang'a baada ya ajali hiyo ambayo imejeruhi watu zaidi ya 38.
Majeruhi 38 katika ajali hiyo wamelazwa kwenye Hospitali ya Rufaa mkoani Iringa.
Akizungumzia hali ya majeruhi wa tukio hilo, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa mkoa wa Iringa, Dk. Deogratius Manyama amesema wamepokea majeruhi 38 na waliolazwa ni 8 huku majeruhi watatu wakiwa na hali mbaya na kuwa majeruhi wengi wameumia zaidi kichwani na kifuani, huku majeruhi 27 wakiruhusiwa kurudi nyumbani kutokana na kutokuwa na majeraha makubwa.
No comments:
Post a Comment