Na Waandishi Wetu
Vijana wa Kamishina wa Polisi Kanda
Maalum ya Dar es Salaam, CP Suleiman Kova kwa kushirikiana na
Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers wamefanikiwa
kulifumua danguro linalodaiwa kufuga madenti wa vyuo mbalimbali jijini
Dar.
Madenti hao walikamatwa mwanzoni mwa
wiki hii kwenye danguro hilo lililopo ndani ya baa maarufu iliyopo
maeneo ya Buguruni-Sokoni, Dar.
KERO
Awali kikosi kazi cha OFM kilipokea
malalamiko kutoka kwa wazazi waishio maeneo hayo wakilalamikia ufuska
wa kutisha unaofanyika kwenye danguro hilo.
Mzazi:Halooo…nazungumza na OFM?
OFM: Ndiyo…tukusaidie nini?
Mzazi: Mna habari?
OFM: Tunazo nyingi lakini ukitupatia ya kwako tutaifanyia kazi ipasavyo.
Mzazi: Tunawaamini OFM mnatisha kama
njaa. Sisi ni wazazi wa hapa Buguruni-Sokoni. Kuna danguro hapa kwa
kweli yanayofanyika ni aibu tupu. Tunaomba mje mjionee wenyewe mfanye
kazi yenu.
OFM: Nini hasa kinafanyika?
Mzazi: Yaani vitendo vya ngono
vinafanyika na sasa hivi hata kwa nje wapo watu wanafanya biashara
haramu ya ngono hivyo watoto wetu wanashuhudia vitu vya ajabu na
kondomu zimezagaa kila kona.
OFM: Sawa, tuachie tufanye kazi yetu.
Mzazi: Oke, lakini naomba
chondechonde msinitaje wala kuonesha namba yangu kwa sababu hii ni
biashara ya watu nitamwagiwa tindikali bure!
OFM: Tunaheshimu vyanzo vyetu hatuwezi kukutaja popote kwani siyo maadili ya kazi yetu.
OFM KAZINI
Kabla ya kuwataarifu polisi juu ya
kero hiyo kwa wakazi wa eneo hilo, vijana wa OFM waliingia kazini ili
kujikusanyia ushahidi ambapo walipofika walishuhudia vitendo hivyo
vikifanyika mchana kweupe bila kujali kama kuna serikali.
Baadhi ya makachero wa OFM
walijifanya wauzaji na wengine wanunuaji ambapo walijikusanyia data za
kutosha huku wakiwarekodi wahusika (madenti wanaojiuza na wanaume
wanaowanunua) kwa kutumia vifaa vya kazi bila wao kushtuka.
BEI
Kuhusu bei, wapo wa bei chee kuanzia
buku mbili hadi tano na wa bei mbaya ambao siyo wengi, wao wakianzia
dau la elfu kumi na kuendelea.
Mmoja wa vijana hao wa OFM
alifanikiwa kuingia ndani baada ya kukubaliana bei na mmoja wa wauzaji
ambapo alipofika na kujionea mazingira halisi aliahirisha kwa kigezo
kuwa alikuwa amepokea simu ya dharura.
USHUHUDA MBAYA
Hata hivyo, alichokishuhudia ndani,
anasimulia: “Nilishuhudia watu wakiwa kwenye ‘pea’ wakijiachia kwa
ngono na suala la kondom ilikuwa ni uamuzi wa mtu.
“Kondom zilizotumika zilikuwa
zimezagaa kila kona yaani nilihisi mwili kunisisimka na kuwaza sana juu
ya janga la Ukimwi. Kwa hali ile tumekwisha.”
TAARIFA POLISI
Ili kufanikisha zoezi la kulifumua
danguro hilo, OFM iliwasiliana na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ilala,
Marietha Minangi na kumweleza mchezo mzima wa uchafu unaofanyika eneo
hilo.
Bila kusita, kamanda huyo aliteua
vijana wake kutoka Kituo Cha Buguruni ambao walitekeleza kwa kiwango
cha oparesheni hiyo maalum.
Walipofika eneo la tukio, polisi hao waliwakamata wahusika wote akiwemo mmiliki wa biashara hiyo.
DENTI IFM
Wakati watuhumiwa hao wakihenyeshwa
na polisi, mmoja wa madenti hao anayesoma Chuo cha IFM, Peter Davis
alisema kwa upande wake aliamua kuweka makazi yake ndani ya chumba
kimoja cha danguro hilo.
Katika utetezi wake, denti huyo alidai kuwa aliamua kuishi hapo kwa kuwa mazingira hayo ni mazuri kwake kwa ajili ya kujisomea.
Mwingine aliyenaswa ndani ya kiwanja
hicho cha maasi ni denti aliyejitambulisha kwa jina la Mwanahamisi
(hakutaja chuo) ambaye alidai kuwa tangu siku hiyo atauacha uchangudoa
na kuapa kuwa akiachiwa huru ataenda kusoma kwa bidii.
Denti mwingine aliyekamatwa katika
msala huo alijitambulisha kwa jina moja la Angel ambaye alidai kuwa
anasoma chuo kimoja kilichopo Kariakoo, Dar na wengine hawakutaja
majina zaidi ya kukiri kuwa ni wanafunzi.
MUUZA KONDOM NAYE MBARONI
Ndani ya gesti hiyo pia alinaswa
njemba mmoja aliyekuwa ameweka maskani na kazi yake kubwa ilikuwa kuuza
kondom kwa madenti hao ambao humwingizia kipato chapuchapu.
Hata hivyo, jamaa huyo alitiwa mbaroni kwa uchunguzi zaidi.
Mbali na oparesheni hiyo, pia polisi
hao waliendeleza msako maeneo mengine ya Buguruni ambapo dadapoa kibao
walikamatwa huku mmoja akiangua kilio na kutamani kujiua kuliko mumewe
kujua kuwa anauza mwili.
NYUMA YA NONDO
Baada ya kuhojiwa kuhusika na
biashara haramu ya ngono na kukiri, watuhumiwa hao wote waliwekwa nyuma
ya nondo kwenye Kituo cha Polisi cha Buguruni na kufunguliwa jalada la
kesi namba BUG/RB/13114/2013 - UMALAYA, wakisubiri sheria kuchukua
mkondo wake.
WAZAZI SOMENI HAPA
Uchunguzi wa gazeti hili ulionesha
kuwa madenti hao na wengine wengi jijini Dar, wamekuwa wakiaga kwao
kuwa wanakwenda masomoni lakini kumbe wanaishia kwenye madanguro
yaliyojazana jijini kwa ajili ya kujiuza.
Huku wazazi wakitoa fedha nyingi na
huduma nyingine wakiamini watoto wao wanasoma, hali ni tofauti kwani
madenti wengi wamekuwa wakiishia kwenye vitendo vya kihuni na kufeli
masomo na maisha kwa jumla kisha kugeuka mzigo kwa familia.
Gazeti hili linawataka wazazi
kufuatilia mienendo ya watoto wao wanaowasomesha ili kuwakanya juu ya
kujiingiza kwenye uhuni ambao huhatarisha maisha yao -Mhariri.
No comments:
Post a Comment