Victoria Mukama (10) baada ya matibabu
KATIKA
hali isiyokuwa ya Kawaida, Baba mmoja aliyejulikana kwa jina la Oscar
Mukama mkazi wa Isengo Airport Jijini Mbeya amemjeruhi vibaya binti
yake Victoria Mukama (10) kwa kumpiga sehemu mbali mbali za mwili wake
akitumia vifaa vyake vya ulinzi likiwemo Lungu.
Kwa
mujibu wa Mwalimu wa zamu wa Shule ya Msingi Airport, Damali Obadia
alisema tukio hilo la ajabu lilitokea majira ya saa mbili na nusu
asubuhi ambapo akiwa ofisini alimuona mzazi huyo akiwa na mtoto huku
akiendelea kumpiga wakielekea ofisini.
Alisema
mzazi huyo baada ya kufika walimu walimpokea na kumuuliza kwa nini
anampiga kiasi hicho mtoto wake alijibu mtoto ni wa kwake mwenyewe na
alizaa kwa manufaa yake hivyo haoni sababu ya kuulizwa kuhusu kipigo
kwa mwanaye.
Aliongeza
kuwa baada ya walimu kumweleza kuwa kitendo alichokifanya ni cha
kinyama na hakipaswi kutendeka Mzazi huyo alitoa kisu na kuwatishia
walimu ikiwa ni pamoja na kutoa matusi makali dhidi yao ambapo walimu
walifanikiwa kumtuliza na kumuomba amwache mtoto ili walimu wamwadhibu.
Alisema
baada ya mzee huyo kuondoka na kumwacha mtoto walimpigia simu mama wa
mtoto ambaye baada ya kufika shule alizimia kutokana na hali aliyomkuta
nayo mtoto wake ambapo Walimu walitoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Mtaa
kasha kwenda Polisi kuchukua Fomu namba tatu (PF3) kwa ajili ya
matibabu.
Mama
mzazi wa binti huyo Teodora Paulo alisema yeye na mume wake hawakuwepo
nyumbani ambapo baada ya kurejea kutoka Msibani majira ya asubuhi
walimkuta binti yao hajaenda shule na walivyomuuliza sababu ya kutoenda
shule alijibu alikuwa havioni viatu vyake.
Alisema
baada ya kumsaidia kutafuta na kutofanikiwa kuviona baba yake ambaye
nayeb alikuwa amejiandaa kwa ajili ya kwenda kazini kwake anakofanya
kazi ya Ulinzi alimwamuru mwanaye kuvaa sare za shule na kwenda naye
hivyo hivyo kwa kile alichodai anampeleka shule.
Alisema
alishikwa na butwaa hadi kupoteza fahamu baada ya kumkuta mtoto
amejeruhiwa huku akiwa amepigiwa simu na mumewe kwamba aende shule
kumchukua mtoto wake lakini hakujua kama amepigwa kiasi cha kumjeruhi
mtoto sehemu mbali mbali za mwili wake.
Akizungumzia
kisa cha kupigwa kwake baada ya kupatiwa matibabu katika Hospitali ya
Rufaa ya Mbeya katika Chumba cha dharula, Victoria Mukama (10) ambaye
ni mwanafunzi wa darasa la nne katika Shule ya Msingi Airport alisema
wakiwa njiani kuelekea shuleni alishangaa akianza kupigwa bila kuelezwa
sababu ni nini.
Alisema
alianza kupigwa tangu wanatoka nyumbani hadi wanafika shule iliyoumbali
wa Mita 250 kutoka Nyumbani hadi Shuleni akitumia Virungu na fimbo huku
akiwa ameshika kisu mkononi kwa ajili ya kuwatishia wanataka kumuokoa.
Kutokana
na tukio hilo Jeshi la Polisi linaendelea kumtafuta Mtuhumiwa huyo wa
unyanyasaji wa watoto baada ya kufunguliwa kwa jarada lenye namba MB/IR/9563/2013 katika kituo cha kati cha Polisi Mbeya.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Pambogo Esia Edward ambaye pia ni
Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Shule hiyo alisema kitendo kilichofanywa
na mtuhumiwa huyo hitendo hakipaswi kufumbiwa macho hivyo ni lazima
sheria ichukue mkondo wake kwa kuhakikisha vitendo hivyo vinakomeshwa
ndani ya jamii.
Aliongeza
kuwa hajawahi kusikia mtuhumiwa huyo kama amewahi kujihusisha na
ukatili wa namna hiyo na kuongeza kuwa huwa anatoa ushirikiano vizuri
katika ngazi ya mtaa na kuhudhuria vikao mbali mbali vinavyoitishwa
pamoja na kuchangia mada.
Nao
majirani wa mtuhumiwa huyo walidai kuwa tabia ya Mwanaume huyo kufanya
unyanyasaji inafichwa na mkewe ambaye anaonekana kuwa muoga wa kupigwa
na mumewe na kuongeza kuwa anatabia ya kuandika makosa anayotendewa na
mkewe.
Walisema
awali amewahi kuoa mke na kuzaa nae watoto watatu lakini mkewe huyo
alikimbia baada ya kuona tabia ya unyanyasaji imezidi kutoka kwa
Mwanaume huyo aliyetajwa kuwa ni jamii ya watu wa Mosoma Mkoani Mara
ambako tabia kandamizi dhidi ya wanawake na watoto bado zinafanyika.
CREDIT: MBEYA YETU
|
No comments:
Post a Comment