Diamond akipozi na madansa wake siku alipoingia na jeneza katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, Dar.
Diamond ambaye wimbo wake mpya wa
‘Number One’ upo katika chati ya juu katika muziki huo, usiku wa
kuamkia Jumapili iliyopita aliingia na jeneza hilo katika Viwanja vya
Leaders Club, Kinondoni, Dar na kusababisha maswali mengi tata kutoka
kwa mashabiki waliojazana kwenye onesho la Serengeti Fiesta 2013.
ILIKUWA SAPRAIZI
Mapaparazi waliokuwa wamejaa katika
viwanja hivyo wakihakikisha wananasa matukio muhimu hasa yale
‘exclusive’, walipenyezewa mapema kuhusu Diamond kuingia na jeneza.
Mtoa habari alisema Diamond
aliingiza jeneza viwanjani humo kwa lengo la kupanda nalo jukwaani
wakati akiimba wimbo wake uitwao Nikifa Kesho ambao mashabiki wake
wengi wanasema amejichulia kifo.
Kwa sharti la kutoandikwa jina lake , mtoa habari huyo ambaye ni mtu wa karibu na Diamond alisema:
“Diamond amekuja na jeneza,
limefichwa kule nyuma wanakobadilishia nguo wasanii, atapanda nalo
jukwaani. Anataka kuwafanyia sapraizi mashabiki wake.”
SAPRAIZI YAKWAMA
Hata hivyo, baada ya matatizo ya
kiufundi yaliyojitokeza, Diamond hakuweza kupanda jukwaani Jumamosi
usiku huo na badala yake akatakiwa kupanda kesho yake Jumapili ambapo
pia hakulitumia jeneza hilo kama mawazo yake ya awali yalivyokuwa.
Mapaparazi wetu walisaka sehemu
lilipohifadhiwa jeneza hilo na kufanikiwa ambapo pia walikuta baadhi ya
watu wakilishangaa na kuulizana maswali.
MASWALI TATA
Nurdin Ali, mkazi wa Mbagala, Dar aliyeliona jeneza la Diamond alisema:
“Mimi namkubali sana huyu bwana mdogo lakini sasa mambo ya majeneza jukwaani ya nini tena?
“Sikubaliani na hili suala. Hata
wimbo wake wa Nikifa Kesho sioni kama una mantiki. Ni kama tu
anajitabiria kifo. Anapita mlemle alimopita marehemu Kanumba, maana
naye aliimba wimbo akielezea itakavyokuwa siku akifa, ikawa kweli.
“Lakini Diamond amekwenda mbele
zaidi kwa kuamua kuja na jeneza kabisa stejini. Sijui amenunua au
amekodisha, ila sikubaliani naye hata kidogo.”
MATUMIZI YA JENEZA
Mwingine aliyekataa kuandikwa jina lake alisema:
“Halafu kama lengo lake lilikuwa
kuonesha uhalisia wa kifo katika wimbo wake, kwa nini asingekuja na
jeneza la imani yake? Angalia, jeneza lina msalaba ambao unakubalika
katika imani ya Kikristo, kwa nini asije na jeneza la Kiislamu au
sanduku ambalo halina msalaba?”
Akaongeza: Au inawezekana huyu
jamaa anataka kubadili dini ili aoane na Penny (Penniel Mungilwa)
ambaye ni Mkristo kwa sababu huku ni kukana imani yake kimyakimya.”
ALIWAHI KUTANGAZA KUJENGA MSIKITI
Shabiki mwingine alikwenda mbali
zaidi na kusema kama Diamond ni muumini mzuri wa Kiislamu tena mwenye
lengo la kujenga msikiti kama alivyowahi kutangaza siku za nyuma,
anatakiwa kutofungamana kabisa na ishara zinazoonesha anaunga mkono
imani nyingine.
“Anapaswa kuwa makini na mambo yake
na awe na washauri wazuri, vinginevyo atakuwa anafanya mambo yanayoibua
maswali mengi kwa jamii inayomwamini,” alisema shabiki huyo
aliyejitambulisha kwa jina moja la Jennifer.
HUYU YUPO TOFAUTI
Shabiki aliyejitambulisha kwa jina la Hamadi Hajj (34) mkazi wa Kijitonyama, Dar alisema:
“Hakuna uhusiano wowote kati ya hili jeneza na mambo ya kubadilisha dini au kuiunga mkono. Kikubwa ni lengo alilotaka litimie.
“Ukiachana na hilo, mambo mengine
yako wazi jamani. Upatikanaji wa majeneza ya Kikristo ni rahisi zaidi
tofauti na ya Kiislamu. Wabongo wanapenda sana kukuza mambo,” alisema
Hajj.
Siku hiyohiyo, usiku huohuo, mapaparazi wetu walimbana Diamond kuhusu kutinga Leaders na jeneza ambapo alijitetea hivi:
“Ni swaga tu zile.”
Alipobanwa zaidi na kuulizwa ni swaga gani zinazochanganywa na vitu vinavyoashiria huzuni na imani ambayo si yake, alisema:
“Nilitaka kuwafurahisha mashabiki
wangu na kuwapa uhalisia wa ule wimbo wangu wa Nikifa Kesho, sikuwa na
nia ya kukashifu imani ya mtu.”
FIESTA PART II
Baada ya shoo yake kushindikana na
kuhamishiwa siku iliyofuata (Jumapili), timu yetu ilitinga viwanjani
hapo ili kujua kama Diamond angepanda na jeneza hilo kama alivyotarajia
lakini jeneza halikuwepo eneo lilipohifadhiwa awali.
Diamond alipofuatwa na kuulizwa kama mpango wake bado uko palepale, alijibu:
“Lile jeneza nilipanga kupanda nalo
jukwaani wakati nikiwa naimba wimbo wangu wa Nikifa Kesho lakini kwa
bahati mbaya sikuweza kupanda kuimba kutokana na matatizo ya kiufundi,
leo (Jumapili) nisingeweza kupanda nalo kwa kuwa muda tuliopewa ni
mfupi sana,” alisema Diamond.
Alipobanwa kuhusu kutumia jeneza la Kikristo na kuhusishwa na fununu za kubadili dini, alisema hana mpango huo kabisa.
“Naomba nieleweke, mimi sikuwa na
nia tofauti zaidi ya kuwakilisha kilichopo katika wimbo wangu. Lengo
lilikuwa kuonesha uhalisia tu wa kibao changu cha Nikifa Kesho, siyo
zaidi ya hivyo,” alisema.
Inasemekana kwamba Diamond aliamua
kubadilisha uamuzi wake wa kupanda na jeneza jukwaani siku hiyo baada
ya kunyetishwa na watu wanaomtakia mema kuwa asingeonesha picha nzuri
kwa jamii, hasa kwa vile jeneza hilo lilikuwa na msalaba juu ya mfuniko.
katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, Dar
No comments:
Post a Comment