Kiongozi Mstaafu wa CCM, Pius Msekwa amesema endapo vyama vya upinzani
vikiungana na kuweka mikakati makini ya muda mrefu, vinaweza kuking’oa
CCM madarakani.
Akizungumza kwenye mahojiano maalumu na mwandishi wetu jana, Msekwa
alisema kwa mtindo wa sasa wa vyama vya upinzani kila kimoja kusimama
peke itakuwa ndoto kukishinda CCM.
“Kama vyama vya upinzani vinataka kuwe na upinzani wenye nguvu dhidi ya
CCM ni lazima viungane vyote. Tena viweke mikakakati ya muda mrefu ya
kujiimarisha,” alisema Msekwa kwenye mahojiano hayo.
Hata hivyo, alisema kuiondoa CCM madarakani siyo kazi rahisi kwa sababu
mizizi yake imeenea kila kona ya nchi huku akisema wazo la upinzani
kuungana halitakuwa rahisi kwa kuwa wengi wao ni walafi wa madaraka na
hakuna atakayekuwa tayari kuvunja chama chake na kuunda kimoja kwa hofu
ya kukosa uongozi.
Akijibu swali kuhusu nguvu ya Chadema kwa sasa Msekwa alisema:
“Wanapambana na CCM kwenye majukwaa ya kisiasa lakini si kuwa na watu
wengi wanaokiunga mkono.”
Alisema CCM kina mizizi hadi ngazi za chini kabisa nchi nzima tofauti na vyama vingine.
Alisema Chadema kiko katika baadhi ya maeneo ya Tanzania Bara wakati
Zanzibar hakina nafasi, tofauti na CUF ambacho alisema angalau
kinaonyesha kuwa na nguvu visiwani huko.
Kuhusu Chadema kuwa na wabunge wengi Tanzania Bara, Msekwa alisema ni
neema iliyokiangukia baada ya CCM kufanya makosa ya uteuzi kwa baadhi ya
majimbo.
Msekwa ambaye aliwahi kuwa Spika wa Bunge alisema pamoja na neema hiyo, Chadema hakiwezi kufikia asilimia 40 ya wabunge wote.
“Kweli Chadema kimejitahidi lakini ukichunguza utabaini ni neema
iliyowaangukia kutokana na makosa ya CCM kuteua watu ambao wapigakura
walikuwa hawawataki,” alisema Msekwa.
Alisema Chadema kimekuwa kikionekana kufanya vizuri kwenye siasa za
majukwaani kwa sababu kina nafasi kubwa ya kukosoa na hata kutoa madai
ya kutunga dhidi ya CCM ili mradi yawe yanawagusa wananchi.
Kuhusu uwezekano wa vyama vya upinzani kuchukua nchi kutokana na CCM
kuwa na makundi mengi ambayo yanaweza kukisambaratisha katika Uchaguzi
Mkuu wa mwaka 2015 Msekwa alisema: “Hakuna mtu anayeweza kuondoka CCM na
kuivunja nguvu. Hata akiwa ni kiongozi mwenye nguvu ya kisiasa kiasi
gani
No comments:
Post a Comment