Tokea enzi ya uhai wa Julius Kambarage
Nyerere Faili la LOWASA kufahamika kuwa na utajiri wa kutosha
linafahamika sana,na haijaanza leo kwa Lowasa kusemwa na kupewa shutuma
kama hizo wala hazikuanza jana.
Zimeanza tokea kipindi Mwalimu Nyerere
yuko hai,na hadi alishafikia hatua ya kuhoji utajiri wa Lowasa enz hizo
akiwa kijana kama wa miaka 42 hivi,na kwa wakati huo miaka 42 huonekana
kijana kweli kweli tofauti na sasa vijana katika umri kama huo washakuwa
wazee tayari kutokana na ugumu wa maisha na frustuations zake.
Je,unafaham ni kwa nin MALECELA kwa kawaida tuh tokea hapo kale hampendi Edward Lowasa??
Hii vita haikuanza leo.,wanaccm hawa
wawili na wenye ushawish kwenye chama hiko wameanza msuguano na
malumbano tokea enzi hizo John Malecela akiwa Waziri Mkuu na Lowasa
akiwa Waziri mwandamizi katika ofisi ya waziri ya waziri mkuu,kwa
mantiki hiyo kwamba alikuwa chini ya malecela na kwa kumsaidia majukumu
ya kazi ya siku zote za kuendesha serikali.
Enzi hizo wabunge wa jamhuri ya muungano
wa tanzania walikuwa hawana magari ya kusafiria kama haya
wanayokopeshwa kwa sasa,hali iliyokawa inawapa ugumu sana kuwatembelea
wananchi wao majimboni hata wakati mwingine ugumu pia wa kuwahi bungeni
kwa wakati kutokana na aina ya magari waliyokawa wanayatumia kipindi
hiki kukosa stability ya kumudu safari na ukizingatia ubovu wa bara bara
wa kipindi huko maeneo mbali mbali ya nchi hiyo.
Hili suala lilikua linaumiza sana
serikali kipindi hiko chiniya utawala na usimamiz wake wazir mkuu wa
kipindi hicho ndug john malecela.
Kutokana na kuwaza na kuwazua likaja
wazo la kupeleka idea kwa serikali ya watu wa japan ili kuona ni kwa
namna gani wanaweza kuwasaidia kihali na mali ili iweze kujikwamua
katika tatizo hilo,
Mungu si Athumani,serikali ya japan enzi
hizo wakakubali kuwaunganisha serikali ya tanzania na kiwanda cha
toyota na kuwapa ushirikiano wa hali ya juu katika mazungumzo baina yao
na kiwanda hicho hadi ikafikia tamati ya makubaliano kwamba serikali ya
tanzania inaweza kukopeshwa magari hayo kisha wakawa wanalipa pole pole
ili kusaidia kukizi na kuikubali changamoto hiyo.
Serikali baada ya kufanikisha plan hiyo
ikaja kwa wabunge na kuwaeleza kwamba wanaweza kukopeshwa magari kwa
mkopo,wabunge waliingia na wasi was kias flan na kusema wao wataweza
kulipa vpi gharama hzo ukizingatia pesa waliyokawa wanachukua kipindi
hiko isingetosha kulipa mkpo huo??
Serikali kupitia kw wazir mkuu malecele
wakawaambia nyinyi chukuen tuh,sisi serikali tutajua tunawasaidia
vipi,kwaiyo chukuen kwanza ili mukabiliane na changamoto ya usafiri
kwanza.
Wabunge walikubali wazo lile na deal likafanyika,mambo yakafana kisawa sawa.
Sasa baada ya hapo mtu pekee ambae
alikuwa anafuatilia mchakato mzima ni wazir wa nchi ofisi ya wazir mkuu
enzi hizo akiwa ni edward lowasa,alikuwa anafuatilia suala hilo kwa
ukaribu sana.
Wale wajapan walipolipwa chao,kumbe kuna
makubaliano ambayo yakishafiikiwa baina yao na wazir mkuu malecela ya
kumpatia kifuta jasho kwa kufanikisha deal ile kufanyika kwa ukamilifu
wake.
Na yasemekana kifuta jasho hiko kilikuwa cha maana sana,cha maana sana sana,
Bahati mbaya sana wale wajapan
walipofika ofcn kuleta kifuta jasho kile walianzia kwanza kwa ofisi ya
wazir wa nchi ili wapate nafas ya kumuona wazir mkuu,sasa walipokutana
na lowasa yasemekana akawauliza mnafuatia nin tena mheshimiwa ili hali
deal ilishafanyika kikamilifu??kwan kuna tatizo??wale wajapan
wakamwambia kwamba kuna kifuta jasho yapasa tumkabidh muheshimiwa wazir
mkuu malecela.
Lowasa,,akastaajabu..!!akasema
,,"mnasema"???hicho kifuta jasho mnataka kumfikishia vipi mheshimiwa
hamjui kuwa yule ni mtu mkubwa sana??kuna utaratibu wa kumfikishia kwa
protokali ya serikali,sasa sikilizen bwana....
Hiyo pesa nipen mimi nitamfikishia,kwan
kwa sasa hata hivyo yupo safarin hadi arudi,so nipeni mimi
nitamkabidh,wale wajapan kwa kuwa wanafaham katika mchakato mzima wa ile
deal lowasa nae alikuwa anaifuatilia kwa karibu hawakuwa na was was
sana kumwachia amana kama ile.,,wakamwachia na kusign nae kisha
wakageuza zao.
Kilichotokea hapo sasa mungu mwenyew ndie anaejua,
Lowasa akapiga kimya,kimya na yeye,yeye
na kimyaa,muda ukawa unazid kwenda naskia ile pesa akaanza kuifanyia
michakato ya kuizungusha na kuwekeza kwenye biashara ya real estate kwa
haraka haraka na kuzikodisha kwa taasisi binafsi hata balozi mbali mbali
za nchi mbali mbali,
Naskia ipo moja ambayo aliikodisha kwa
ubaloz wa south afrika hapa hapa nchini,na hadi leo naskia iyo nyumba ni
mali ya lowasa pamoja na vitu vingine vingi,kwa ufupi lowasa kawa DON
tokea kitambo sana.
Sasa maskin mzee malecela akaona siku
zinakwenda na kifuta jasho kutoka japan hakifiki,,akaamua kunyanyua simu
na kuwavutia uzi jamaa na kuwauliza,ebwan vipi ile kitu yangu??mbona
nyinyi wajapan wabaya kias hiko??ina maana baada ya deal kufanyika
mnatupa jongoo na mti wake??
Wajapan wakasema Booossi,mbona kifuta
jasho tulishaleta mda mrefu sana??tulimkabidh bwana Edward yule wazir
wako wa nchi katka ofc yako na alisema atakukabidh kwan ulikuwa
safarini..!!!
Malecela kikamshuka,kikampoa na asijue hata awajibu nini,
Ikabid sasa amwite edward na kumuuliza,wewe edward pesa yangu iko wapi??na nani alikuambia uichukue kwa niaba yangu??
Edward akasema Boooss,kwa kweli pesa
nilichukua lakin sasa kwa kuwa ulikua safarini nikaona niiweke kwanza
hadi urudi,,sasa kama unavyojua pesa tena mzee,kulitokea fursa za
uwekezaji nikaamua kujikopesha ili niizungushe kisha nitakurejeshea
lakin sasa mambo hayajaenda kama yalivyopangwa ndio kwa maana unaona
kimya hiv sijakutafuta.
Sasa malecela presha ikampanda na
kumshukaaa,atasema nini??na ile pesa ni chafu na ya deal ukizingatia
yeye ni wazir mkuu??kumbuka nyerere yupo hai kipindi hicho na akifaham
ishu kama hizo panakua hapatoshi..!!
Ikabid malecela ajikaze kisabun na kufa na tai yake shingoni huku lowasa akiendelea kupimp na kujitanua kwa raha zake.
Kwa kias kikubwa hapo ndipo LOWASA
alipoanza kuwapiga GAPE LA KIPATO wenzake walio wengi,na kwa kias
kikubwa wenyewe hao ambao wako ndan ya system wanalijua hilo.
Ndio kwa maana tokea zama hizo VITA
baina ya LOWASA na MALECELA haiwez kuisha kamwe,kwan mambo
waliyofanyiana wawili hao yanatishaa.
Hiyo ndiyo siasa ya bongo ilivyo,DO OR DIE.
No comments:
Post a Comment