Mchungaji Harris Kapiga wa kanisa la Nchi ya Ahadi
lililoko Sinza Kamanyola, ameamua kuanzisha klabu ya usiku kama zilivyo
klabu nyingine za starehe.
Klabu hiyo iliyozinduliwa hivi karibuni maeneo ya Mbezi Tangibovu katika hoteli inayoitwa Mak Hotel, imeonekana kuvutia vijana wengi ambao walionekana wakifurahia mandhari na muziki uliokuwa ukipigwa ndani yake.
Tofauti na klabu nyinginezo, Mchungaji Kapiga
anasema kutakuwa na udhibiti wa vishawishi vya dhambi ikiwa pamoja na
ulevi, mavazi yasiyo na staha na aina ya muziki unaopigwa.
Anasema tangu alipoanzisha wazo hilo, watu wengi hasa wachungaji walikuwa na wasiwasi kuhusu vishawishi hivyo.
“Tangu nimeanza wazo langu hili nimekumbana na
vikwazo vingi. Imeshtua watu wengi, japo wengi wamelikubali na kuna
baadhi hawakubali ila hawawezi kusema wazi,” anasema na kuongeza:
“Wengine wanajiuliza nitawezaje kudhibiti vipi
hali ya klabu kwa sababu maeneo haya kunakuwa na anasa, ulevi na masuala
ya mavazi watu watavaaje, na mimi nawajibu.”
“Mtu akija hapa na mavazi mabaya hataingia,
tutakuwa makini sana katika hili. Mtu avae nguo yenye staha, siyo mtu
aje nusu uchi, tutamtoa kwa nia njema tu. Hata mtu aliyelewa tutamtoa
labda tusimgundue.”
Hata hivyo baadhi ya wakristo mitaani wanalalamika wakidai kuwa ukristo unapoteza muelekeo kwa kufanya mambo kama kwenda club. Lakini pia wapo wengine waliofananisha club hiyo na mikesha inayofanyika katika nyumba nyingi za ibada karibu kila ijumaa.
No comments:
Post a Comment