Pages

Translate

Tuesday, 21 January 2014

JANUARY 20 ILIVYOPITA NA KUACHA HISTORIA YA VIFO VYA WATANZANIA KWA AJALI




Baadhi ya miili ya watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo wakiwa mtaroni.. Kwakweli inasikitisha sana, hiyo ikiwa ni ajali mbaya kutokea kwa januari 20 baada ya ajali nyingine mbili ikiwemo ya Noah iliyoua watu na ile ya Mbeya kugongana magari manne kwa wakati mmoja mji mdogo wa Mbalizi
LEO majira ya saa nane alasiri Basi lenye maarufu kama ALLHAMDULILAH lilipata ajali mbaya huko mkoani Lindi watu kumi walipoteza maisha papohapo na 28 mahututi wapo Hosptali ya mkoa wa lindi sokoine,


Chanzo cha ajali hilo ni baada ya Basi hilo kugongana na
lori la mizigo wakati basi hilo likitokea Dar kuelekea Mtwara ma kupoteza mwelekeo na kupinduka mita kadhaa kutoka barabarani hali iliyochanganya na utelezi mkali kutokana na mvua kubwa iliyonjesha muda mchache kabla ya ajali. 

 

Na Mbeya mambo yalikuwa si mambo baada ya magari zaidi ya matano kugongana katika mji mdogo wa mbalizi na gaadae kuzuka kimbunga ambacho kiliezua nyumba zaid ya 10 na kuwaacha wananchi wa mji huo mdomo wazi. Ama hakika january 20 ni ya kukumbukwa kwa matukio haya


Magari yakiwa yamegongwa Mbalizi Mbeya
Watu mbalimbali wakiwa wanashangaa ajali hiyo iliyosababisha Gari moja kugonga magari mengine zaidi ya matano
Mashuhuda wakiwa wanashuhudia ajali hiyo
 
wakazi wa mbalizi wakishuhudia upepo ukiezua bati kati ya moja ya nyumba zilizopitiwa na kimbunga
 
 
Nako Singida mambo yakawa zaidi pale ambapo watu 13 kupoteza maisha papo hapo baada ya gari aina ya Noah kugongana uso kwa uso naa roli



Hivyi ndivyo ambavyo tarehe 20 ilipita na kuacha watanzania wakijiuliza maswali Mengi kuwa ni nini kinatokea na kuwaacha bila majibu. Wenye Hekima ya Kristo husema ng'ang'ania sana kuwa na Yesu kwani utakuwa na moyo usiokufa, ukipita duniani kama wasemavyo ya kuwa duniani tu wapitaji utaishi milele Mbinguni. Mwenye sikio na asikie na mwenye macho kasoma.

No comments:

Post a Comment