JESHI
la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watu 12 akiwemo Mwenyekiti wa
Kitongoji cha Mshewe wakituhumiwa kwa kosa la kuua mtu kwa kumzika akiwa hai.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwani Athumani, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo
na kuongeza kuwa lilitokea juzi majira ya saa 08:30 mchana novemba 6 mwaka huu katika kijiji
cha Mshewe, kata ya Mshewe , tarafa ya bonde la Usongwe
wilaya ya Mbeya vijijini Mkoani hapa.
Alimtaja
marehemu kuwa ni Alison maarufu kwa jina la Hanahela Mwakabana(80) kyusa,
mkulima, mkazi wa kijiji cha Mshewe ambaye aliuawa na kundi la wananchi
walioamua kujichukulia sheria mkononi.
Alisema
wauaji hao walikuwa wakiongozwa na Julius Katisha Ngole
ambaye ni mwenyekiti wa kijiji cha Mshewe baada ya kumfukia ndani
ya kaburi akiwa hai.
Alisema
chanzo cha mauaji hayo ni tuhuma za kishirikina baada ya marehemu
kutuhumiwa kumuua mtoto wake Juma Hanahela(48) kyusa, fundi ushonaji, mkazi wa
kijiji cha Mshewe aliyefariki dunia Novemba 5, mwaka huu kwa maradhi
ya kiharusi ambayo alianza kuugua Oktoba 29, Mwaka huu na kulazwa
hospitali teule ya Ifisi.
Kamanda
Diwani alisema mbinu iliyotumika ni watuhumiwa baada ya
kumaliza kuchimba kaburi walimwambia marehemu aingie ndani ya
kaburi ili apime kama linatosha kumzika mtoto wake ndipo walipomfukia, kisha
kuchimba kaburi lingine pembeni na kumzika mtoto wake Juma Hanahela.
Kwa
mujibu wa Mjomba wa Marehemu ambaye alikuwa shuhuda wa tukio hilo,Edward
Mwaikasu aliliambia JamboLeo kuwa wakati taratibu za mazishi ya mtoto wao
zinaendelea aliwashauri kumwita mchungaji yeyote wa kanisa lililokaribu jambo
ambalo liliafikiwa na Mwenyekiti wa Kitongoji.
Alisema
wakati wakisubiri taratibu hizo kufanyika Mwenyekiti alisikika akimtuhumu
Marehemu kuwa ndiye aliyemuua mwanae hivyo adhabu inayostahili dhidi yake inaandaliwa
na lazima naye ashughulikiwe.
Alisema
wakati Mwenyekiti akiongea hivyo waliokuwa wakichimba kaburi kwa ajili ya
kumzika Marehemu walimwita wakitaka asaidie kuchimba shimo ambapowalimtaka
kuingia ndani ya shimo na kutoa udongo ambapo baada ya kufanya hivyo walianza
kumrushia udongo na kumfukia.
Alisema
kutokana na tukio hilo Mwenyekiti alishauriwa apige simu polisi akidai kuwa
Marehemu alifanya tukio msibani hivyo wananchi wenye hasira kali wamemuua hivyo
nay eye kukubaliana na ushauri huo.
Kutokana
na tukio hilo Jeshi la Polisi linawashikilia watuhumiwa kumi na mbili 12
kuhusiana na tukio hili wakiongozwa na Mwenyekiti Julius Katisha Ngole(52)
msafwa, wote wakazi wa kijiji cha mshewe.
Kamanda
Diwani alisema taratibu zinafanywa ili watuhumiwa wafikishwe mahakamani
na pia mwili wa marehemu ufukuliwe na kufanyiwa uchunguzi wa kitabibu ili
uzikwe upya kwa heshima na taratibu zinazopaswa.
lakini
mpaka hivi sasa mwili haujaweza fukuliwa
na pia wananchi wametoweka kijijini hapo hivyo shughuli za kiuchumi
kuzorota.
|
No comments:
Post a Comment