MIEZI michache baada ya kufunga ndoa na kupata mtoto, Prodyuza na Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Raheem Rummy Nanji ‘Bob Junior’ na mkewe Halima Ally wameachana, Amani linakuhabarisha.
Habari kutoka katika chanzo chetu makini ambacho ni rafiki wa karibu na Bob Junior zinasema kwamba, ndoa hiyo ilivunjika muda mrefu lakini wahusika walikuwa wakifanya siri lakini Amani limeinasa.
BOB JUNIOR TATIZO
Kwa mujibu wa jamaa huyo ambaye hakutaka kuandikwa gazetini, alisema chanzo cha kuparaganyika kwa ndoa hiyo ni Bob Junior mwenyewe kutokana na kutuhumiwa na mkewe kumsaliti.
“Mke wake alikuwa anamtuhumu Bob kutoka kimapenzi na mwanamke mmoja wa Kikenya na pia inasemekana anatembea na Vanessa Mdee (mwanamuziki). Maneno yalivyokuwa mengi, mkewe akaamua kuondoka, hivi ninavyoongea na wewe, yupo kwao,” alisema.
Siku walipopata mtoto.
BOB JUNIOR AKIRIMashitaka yote yalifikishwa kwa Bob Junior kama yalivyo ambapo bila kumung’unya maneno, msanii huyo mwenye mauno sana awapo jukwaani alikubali kutengana na mkewe lakini akachomoa suala la Mkenya na
Vanessa.
“Ni kweli nimeachana na mke wangu kama mwezi mmoja uliopita na ameondoka na mtoto, hayo maneno kwamba nina mwanamke wa Kikenya siyo ya kweli. Vanessa ni msanii mwenzangu, nafanya naye kazi tu, hakuna cha zaidi,” alisema.
YUKO NA NANI SASA?
Alipoulizwa kama ameshafungua ukurasa mwingine wa kimapenzi alisema: “Nimeshasema nimeachana na mke wangu, kwa sasa niko singo, sina mpenzi wala mchumba, niko singo tu.”
Bob Junior alipoulizwa kama atarudiana na mkewe alisema hana uhakika ila kama Mungu ndiye aliyepanga watarudiana lakini kama siyo hawatarudiana.
VANESSA NAYE
Vanessa alipopatikana kwa njia simu na kuelezwa kila kitu, alisema: “Siwezi kuzungumzia suala hilo maana kila jambo huwa lina mipaka yake.”
No comments:
Post a Comment