Mtoto Shabani Maulidi akiwa tayari melala kitandani katika hospitali ya wilaya ya Geita.
   Mama mzazi wa mtoto Shabani menye kilemba kichwani akiwa amepigwa bumbuazi  maeneo ya hospitali.
 Eneo ambalo mawe yanaonekana nyuma ya nyumba ndipo Mtoto huyo  alipo zikwa
Wadogo zake na Shabani nao wakiwa wameshikwa na mshangao kama walivyokutwa  nyumbani kwao.
WATU WAPIGWA BUMBUWAZI
WANANCHI WAMIMINIKA HOSPITALI KUSHUHUDIA
Na Denice Stephano-Geita yetu Blog                                 
MTOTO
 anayedaiwa kufariki miaka miwili iliyopita  na kufanyiwa matanga 
ameonekana  akiwa hai  Septemba 28 majira ya mchana baada ya kukutana na
 mama yake mzazi uso kwa uso  wakati akienda kwenye shughuli zake za 
kibiashara.
Mtoto
 huyo Shabani Maulidi (15) alifariki tarehe 03.01.2010 alishindwa kurudi
 nyumbani kwao tarehe 01.01.2011  wakati alipokuwa amepeleka Mbuzi 
machungani kisha kushindwa kurudi nyumbani na baadaye kuonekana baada 
siku tatu akiwa amefia kwenye kisima cha maji.
Kwa
 mujibu wa Baba mzazi wa mtoto huyo Maulid Shabani alisema mtoto wake 
hakurudi nyumbani siku hiyo waliendelea kumtafuta bila mafanikio na 
ndipo baada ya siku tatu walimkuta akiwa amefia ndani ya kisima cha maji
 kilicho maeneo ya Kijiji cha Nyankumbu Kitongoji cha Mwembeni.
Baba
 huyo alisema baada ya hapo walitoa taarifa Polisi kisha waliruhusiwa 
kuuchukua mwili wa mtoto wao na kwenda kuuzika nyumbani kwa kitongoji 
cha 14 Kambarage ndani ya mji wa Geita.
Alisema
 walifanya shughuli zote za matanga na wakajua tayari mtoto wao 
ameishafariki na kwamba hawakuwa na wazo lolote na kumpata siku zote 
akiwa hai kama ilivyotokea  akisema ni tukio la kustaajabisha kwake.
Mama
 mzazi wa mtoto huyo Aziza Ramadhani akisimulia namna alivyokutana na 
mtoto wake alisema alikuwa akienda kwenye shughuli zake za ujasiriamali 
kama mfanyabiashara ya mbogamboga akiwa amefika eneo la Nyankumbu nje 
kidogo sana na mji wa Geita eneo la Mwembeni alikutana uso kwa uso na  
mtoto wake.
Alisema
 alipomuona alimwita kwa jina lake akisema "mwanagu Shabani ni wewe naye
 akamwitikia ni mimi kisha alimshika mkono huku akiwa haamini macho yake
 ndipo alipompigia simu mumewe naye akaja wakamchunguza vizuri 
wakaabaini  kuwa ndiye mtoto wa Shabani aliyesadikiwa kuwa alifariki na 
kuzikwa.
Akithibitisha
 zaidi mama wa mtoto huyo alisema mwanae alikuwa na alama ya kinundu 
kwenye paji la uso na mguuni akiwa na alama ya kovu mguuni 
iliyosababishwa na kuchomwa na mwiba pia alikuwa na mwanya uliofanan na 
wa baba yake mzazi.
Mtoto
 huyo aliyevuta hisia za watu wengi  mjini Geita ameendelea 
kuthibitishwa na walimu wake wa shule ya Msingi Mwatulole alikokuwa 
anasoma darasa la tano kabla ya kifo hicho cha utata kwa sasa.
Akiongea na Mwandishi wa
 Makamu mkuu wa shule ya msingi Mwatulole Joseph Nungula aliyekuwa 
akifuatilia kwa karibu tukio hilo alisema kweli mtoto huyo anaonekana ni
 yeye bila kutia shaka yoyote .
Mwalimu
 huyo alisema amemtambua mtoto huyo kwa sura na alama hasa ya usoni huku
 akimwelezea mtoto huyo kuwa alikuwa na mahudhurio mazuri shuleni pia 
maendeleo yake kitaaluma yalikuwa mazuri.
Mtoto
 huyo ambaye anaendelea kupewa huduma ya kitabibu katika Hospitali ya 
wilaya ya Geita kwa uchunguzi zaidi wa kiafya anaongea kwa shida 
wanapokuwepo watu watu wengi hata hivyo amemtambua Baba na mama yake 
mzazi ambapo wanapomuuliza baadhi ya maswali anawajibu.
Jeshi
 la Polisi mkoani hapa ambalo lilikuwa likiwa likifuatilia tukio hili 
kwa ukaribu sana limethibitisha kutokea kwa tukio hili huku wakiahidi 
kuendelea kutoa habari zaidi ambazo tutaendelea kuwajulisha huku 
wananchi wakisubiri kibali cha mahakama kufukua kaburi alililokuwa 
amezikwa mtoto huyo.
 
No comments:
Post a Comment