VITA dhidi ya biashara ya
 madawa ya kulevya ni ngumu sana, dirisha la mafanikio ya kudhibiti 
linafungwa na vigogo wauza unga ambao wana fedha nyingi zinazoyumbisha 
sheria kuchukua mkondo wake.
Pointi nambari moja ni 
uwepo wa ripoti za ukamatwaji wauza unga lakini hukumu hazitolewi, swali
 kwa nini hawahukumiwi likipashwa moto ili kuunguza mamlaka 
zinazohusika, Uwazi linafichua siri nzito kuhusu madai ya vigogo 
waliokamatwa na kuachiwa.
 Watu wanne ambao wanatajwa kuwa miongoni mwa vinara wa madawa ya 
kulevya nchini, walikamatwa na madawa ya kulevya yenye thamani ya 
shilingi bilioni 6.2 kisha wakafikishwa mahakamani ambako inadaiwa 
wameachiwa katika mazingira tatanishi.
 Watu wanne ambao wanatajwa kuwa miongoni mwa vinara wa madawa ya 
kulevya nchini, walikamatwa na madawa ya kulevya yenye thamani ya 
shilingi bilioni 6.2 kisha wakafikishwa mahakamani ambako inadaiwa 
wameachiwa katika mazingira tatanishi.
Vigogo hao wanne, wapo 
Watanzania wawili na wengine ni raia wa Pakistan ambao sasa hivi 
inadaiwa wameshatoroka kwenda nje ya nchi.
Februari 21, 2011, jeshi 
la polisi kupitia kitengo cha kudhibiti na kupambana na madawa ya 
kulevya, kiliwakamata wafanyabiashara hao ambao majina yao ni William 
Chonde na Kambi Zuberi (Watanzania) pamoja na Wapakistan, Abdul Ghan 
Peer Bux na Shahbaz Malk.
 Watu hao, walikamatwa na mzigo huo Mbezi Jogoo, Dar es Salaam kwenye 
nyumba ya Chonde, wakiwa na madawa ya kulevya aina ya heroine, yenye 
uzito wa kilo 179 ambayo thamani yake ni shilingi 6,265,000,000.
 Watu hao, walikamatwa na mzigo huo Mbezi Jogoo, Dar es Salaam kwenye 
nyumba ya Chonde, wakiwa na madawa ya kulevya aina ya heroine, yenye 
uzito wa kilo 179 ambayo thamani yake ni shilingi 6,265,000,000.
Sera ya Uwazi ni 
kuendeleza safari iliyoianzisha kwa vile ndilo liliandika pale 
walipokamatwa zaidi ya miaka miwili iliyopita. Wiki mbili zilizopita, 
lilianza upekuzi kujua kesi hiyo imefikia wapi.
Uchunguzi wa waandishi 
wetu uliweza kubaini kuwa watuhumiwa hao wa madawa ya kulevya waliachiwa
 na mahakama kuu kwa dhamana, kinyume na sheria ya madawa ya kulevya 
inavyoeleza.
Sheria ya madawa ya 
kulevya ya mwaka 1996, sura ya 95, kipengele nambari 9, kifungu nambari 
27, kifungu kidogo nambari 1A, kinasema: “Yeyote atakayekamatwa na 
madawa ya kulevya yenye thamani zaidi ya shilingi milioni 10 hapaswi 
kupewa dhamana.”

Vilevile, sheria hiyo 
inaendelea katika kifungu kidogo nambari 1B ambacho kinasema: “Yeyote 
atakayekamatwa akisafirisha madawa ya kulevya hapaswi kudhaminiwa.”
Mkuu wa Kitengo cha 
Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa, 
alipoulizwa kuhusu kile anachokifahamu kufuatia kuachiwa kwa watuhumiwa 
hao, alijibu:
“Mimi sijui, waliachiwa 
mahakamani. Kazi yetu sisi ilikuwa ni kuwakamata, kila kitu kikapelekwa 
kwa DPP (mkurugenzi wa mashtaka), baada ya hapo kesi ilikwenda kwa 
msajili wa mahakama.
“Nijuavyo mimi ni kwamba walifikishwa mahakamani na nilisikia waliachiwa kwa dhamana,” alisema Nzowa.
Yapo madai kwamba baada 
ya watuhumiwa hao kupewa dhamana, walikabidhiwa hati za kusafiria 
(passport) ambazo ziliwawezesha kutoroka. Uwazi lambana Nzowa;
MWANDISHI: Unaweza kufahamu kigezo kipi kilitumika kuwapa dhamana watuhumiwa hao? Maana sheria inakataza.
NZOWA: Nadhani mahakama ndiyo inapaswa kuulizwa swali hilo. Siwezi kuisemea, maana ule ni mhimili mwingine huru.
MWANDISHI: Inadaiwa wewe ndiye uliwapa passport zao na sasa tunaambiwa walishatoroka nchini, hili limekaaje? 
NZOWA: Ni kweli tuliwapa passport zao, tuliagizwa na mahakama kufanya hivyo.

Msajili wa Mahakama Kuu, 
Benedict Mwingwa, alipoulizwa kuhusu kuachiwa kwa watuhumiwa hao kwa 
dhamana, aling’aka, kisha akaahidi kufuatilia kujua kisa na mkasa.
“Nimeshtushwa sana na 
hilo jambo. Ni kweli sheria inakataza, sasa watuhumiwa kama hao 
hawakupaswa kudhaminiwa. Nalifanyia kazi, nitakutana na jaji 
anayesikiliza kesi hiyo aniambie sheria aliyotumia,” alisema Mwingwa.
Uchunguzi uliofanywa 
umebaini kwamba baada ya malalamiko ya muda mrefu kuhusu kusuasua kwa 
kesi za madawa ya kulevya ambayo yanaelekezwa Mahakama Kuu, Jaji 
Kiongozi, Fakhi Jundu, aliitisha mkutano wa dharura wiki mbili 
zilizopita.
Mkutano huo ulishirikisha
 majaji wa mahakama kuu, idara ya usalama wa taifa, Takukuru, ofisi ya 
DPP, mkemia mkuu wa serikali, magereza, polisi na kitengo cha kudhibiti 
na kupambana na madawa ya kulevya.
Vyanzo vyetu vinasema 
kuwa katika mkutano huo, maazimio ya pamoja ni kila idara kutimiza 
wajibu wake bila kutazama sura wala nafasi ya mtu ili haki ionekane 
ikitendeka, huku ikisisitizwa kesi kuharakishwa na hukumu kutolewa.
 
 
No comments:
Post a Comment