Pages

Translate

Monday, 9 September 2013

MTOTO WA MIAKA 5 ALIYEBEBA UJAUZITO NA KUJIFUNGUA MTOTO WA KIUME:

World's Youngest Mother LINA akiwa amelezwa mara baada ya kujifungua kwa njia ya upasuaji. 






















 


LINA MEDINA
 
LINA AKIWA MJAMZITO.
  
LINA AKIWA NA MTOTO NA MMOJA WA MADAKTARI WALIOMFANYIA UPASUAJI NA KUJIFUNGUA MTOTO HUYO KATIKA KITANDA CHA WATOTO CHA MATAIRI MANNE.

LINA Medina aliyezaliwa tarehe 27 Sept. 1933, huko Ticrapo, mkoa wa Huancavelica, nchini Peru, anatajwa kua Mama mwenye umri mdogo kuwahi kutokea katika historia ya Ulimwengu.

Tarehe 14 Mei 1939 Lina akiwa na umri wa miaka 5 na miezi 7, alijifungua mtoto wa Kiume aliy
e mpa jina la Gerardo Medina.

Ilianzaje?
Mwanzoni mwa mwezi Machi 1939 wazazi wa Lina ~ Tiburelo Medina na Victoria Losea waliamua kumpeleka Hospitali baada ya kuona tumbo likiongezeka kupita kiasi.

Wazazi wa Lina walidhani huenda ana uvimbe tumboni, lakini madaktari waligundua kua alikua ana ujauzito wa miezi 7.

Dr. Gerardo Lozada aliamua kumpeleka Lina kwa wataalam zaidi nao wakathibitisha kua ni kweli alikua mja mzito.

Alizaaje ?.
Mwezi mmoja na nusu baada ya kupelekwa hospitali kwa mara ya kwanza, Lina alijifungua mtoto wa kiume kwa njia ya upasuaji, kutokana na njia yake ya uzazi kua ndogo.

Upasuaji ulifanywa na Dr. Lozada, Dr. Busalleu, na Dr. Colareta.

Alivunja Ungo lini?.
Dr. Edmundo Escomel alitoa ripoti kamili juu ya kesi ya Lina kupitia jarida maalum la maswala ya kiafya na matibabu liitwalo La Presse Médicale.

Ripoti hii ilibainisha kwamba Lina alianza kupata siku zake tangu akiwa na umri wa miezi 8, alitofautiana na ripoti ya awali iliyosema kua amekua akiona siku zake tangu alipokua na umri wa miaka 3.

Ripoti hii pia ilisema kua Lina alianza kuota maziwa akiwa na umri wa miaka 4, alipofikisha miaka 5 nyonga yake ilikua imesha tanuka.

Alizaa mtoto gani ?.
Mtoto alizaliwa na uzito wa kilo 2.7 na alipewa jina la daktari wake Gerardo.

Gerardo alilelewa akijua kwamba lina ni dada yake lakini alikuja kujua ukweli akiwa na umri wa miaka 10.

Gerardo aliendelea kukua akiwa mtoto mwenya afya njema lakini alifariki mwaka 1979 akiwa na miaka 40 kwa ugonjwa wa mifupa ujulikanao kwa jina la kitaalam la Bone marrow.

Nani Baba wa mtoto ?.
Lina hajawahi kumtaja baba wa mwanae wala mazingira yaliyopelekea yeye kupata mimba.

Dr. Escomel alipendekeza kwamba inawezekana hata Lina mwenyewe alikua hajui, na kusema kuwa hakutoa majibu yanayojitosheleza.

Tuhuma kwa baba mzazi:
Hata hivyo Baba mzazi wa Lina alikamatwa na kushitakiwa kwa kosa la Unyanyasaji wa kingono wa mtoto (Child Sexual Abuse) lakini aliachiwa baadae baada ya kukosekana ushahidi wa kutosheleza.

Na hivyo basi Baba halisi aliyempa mimba Lina hakuwahi kujulikana.

Maisha ya Lina baadae:
Miaka kadhaa baadae Lina aliolewa na Raúl Jurado ambaye mwaka 1972 walipata mtoto wa kiume.

Lina yupo hai mapaka sasa na anaishi maisha ya kimasikini huko Lima nchini Peru

No comments:

Post a Comment