BI ELIZABETH JOHN AMBAYE AMEZAA NA MZUNGU
Andre akiwa na mzazi mwenzie akimsihi aondoe shauri hilo mahakamani
Andre akiwa na mtoto wake nje ya mahakama
ANDRE LAPIERRE (50) MFANYAKAZI WA MGODI WA BULHYAHULU
Mzungu akitoka kusikiliza shauri lake chumba cha mahakama ambapo shauri hilo lilihairishwa mpaka tar 4.10.2013 ambapo alidhaminiwa na wadhamini wawili na fedha shilingi milioni moja
Raia wa nchini Canada ambaye ni
mfanyakazi wa kampuni ya African Barrick Gold Bulyanhulu aliyefahamika
kwa jina la Andrew Lapierre (50) amefikishwa mahakama ya mwanzo Lunguya
wilayani kahama mkoani shinyanga kwa kosa la kutelekeza mtoto kinyume
cha kifungu namba 166 cha sura ya 16 aliyezaa na Bi Elizabeth John.
Akisoma makosa ya mtuhumiwa, hakimu wa mahakama ya mwanzo Lunguya Derick Masaga ameiambia mahaka kuwa Andre Lapierre mwaka jana alimpata hujauzito Elizabeth John (21) mkazi wa Kakola ambaye alizaa mtoto wa kike aliyefahamika kwa jina la Mariam Andre, na kumtelekeza muda wote bila huduma.
Mtuhumiwa alikana kumtelekeza mtoto huyo na kuiomba mahakama hiyo iagize wakapimwe vipimo vya vinasaba (DNA) ili kubaini ukweli na vipimo vimethibitisha hilo.

No comments:
Post a Comment