Mwanadada
anayefanya vizuri sana kwenye muziki na filamu,baby Madaha amelamba
bingo ya uhakika na kampuni ya Candy n’ Candy Records Label ya jijini
Nairobi iliyomsainisha mkataba msanii mwingine wa Tanzania Mr.Nice hivi
karibuni.
Akizungumza
kwa simu na bongomovies leo meneja wa msanii huyo Joe Kariuki amesema
kuwa pamoja na msanii huyo kupewa mkataba huo wa million hamsini (50)
pia wamempa mwanadada huyo gari ya kutembelea ya kisasa aina ya AUDI TT na nyumba kali mitaa kijitonyama jijini Dar es salaam.
Pamoja
na hayo pedeshee huyo wa Mr.Nice ambaye ndio mmiliki wa studio hiyo
amesema wanataka kumuhamishia msanii huyo jijini Nairobi nchini Kenya
kwa kipindi cha mwaka mmoja ili afanye nao kazi huko kwani wamegundua
kuwa anakubalika sana nchini humo na wapenzi wa muziki.
Baby
madaha ambaye anatarajia kutua nchini leo akitoka Nairobi pamoja na
meneja wake kwa ajili ya kuachia video ya wimbo wake wa kwanza
aliofanya na Label hiyo uitwao (Summer Holiday) ambao umefanywa huko
huko jijini Naironi
No comments:
Post a Comment