HAWA NDIYO MASTAA WA BONGO WALIONASA MIMBA ZIKACHOLOPOKA PASIPO SABABU KUWEKWA WAZI..!!
DHAMIRA
ya watu wengi ni kutunza mimba hadi kufikia hatua ya kujifungua lakini
wakati mwingine ujauzito unaweza kuchoropoka kutokana na sababu tofauti,
iwe kwa kukusudia au bahati mbaya.Kwenye maisha ya mastaa wetu wa Bongo, wapo waliowahi kupata mimba lakini kutokana na sababu tofauti, zilichoropoka.Amani linakumegea baadhi ya mastaa hao ambao wengine walianika sababu za mimba hizo kuchoropoka huku wengine wakifanya siri:
|
AUNT EZEKIEL |
Februari,
2011 aliripotiwa kuwa na ujuzito wa mwanaume ambaye mwenyewe hakumtaja
lakini haikupita muda mrefu, mimba hiyo ilichoropoka pasipo kuweka wazi
sababu.
|
JINI KABULA |
Mwaka
jana alijinadi kuwa na ujauzito wa Mbongo Fleva, Maximiliam Bushoke.
Mimba hiyo ikadumu kwa miezi kadhaa, ghafla ikachoropoka yenyewe kwa
bahati mbaya.
|
WEMA SEPETU |
Kwa
upande wake alitundikwa kibendi na aliyekuwa mpenzi wake, Nasibu Abdul
‘Diamond’ lakini miezi kadhaa mbele ikatoka yenyewe kutokana na sababu
za kitaalam.
|
LULU |
Mwaka
jana aliripoti kwenye vyombo vya habari kuwa na mimba ya muigizaji
mwenzake, marehemu Steven Kanumba. Wakati mapaparazi wakiendelea kufanya
uchunguzi, ghafla ikadaiwa ‘kuyeyuka’ pasipo kujulikana chanzo.
|
LADY JAYDEE |
Huyu
ni mke halali wa Mtangazaji, Gardner Habash. Mwaka 2011 mitandao ya
kijamii iliripoti kuwa ni mjamzito na kudaiwa kuwa habari hiyo ilimpa
faraja mumewe lakini furaha hiyo iliyeyuka ghafla wakati Lady Jaydee
akionekana na tumbo kubwa, ikadaiwa mimba imechoropoka bila sababu
kutajwa.
|
Baby Madaha |
Mwaka
2010 mkali huyo wa filamu na muziki Bongo, alidaiwa kuwa na mimba
ingawa mwenyewe hakutaka kuweka wazi lakini baadaye ilidaiwa kuwa
alikwenda kuichoropoa nchini Kenya.
|
JACK WA CHUZ |
Mapema
mwaka huu aliripotiwa kuwa ni mjamzito lakini mwenyewe hakupenda kuweka
mambo yake hadharani. Hata hivyo, vyanzo makini vilidai kuwa mimba hiyo
ilikuwa ya mfanyabiashara mmoja jijini Dar lakini baadaye aliichoropoa
pasipo kufahamika sababu.
No comments:
Post a Comment