Mwili wa kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Rashidi Seleman mkazi
wa Isevya manispaa ya Tabora ambaye amepoteza maisha baada ya Lori
walilokuwa wamepanda kuanguka eneo la Inala barabara ya kwenda
Kigwa,Polisi wamesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva
ambaye amekimbia huku watu wengine wanne wakiwa wamejeruhiwa vibaya
ambao wamelazwa katika hospitali ya Rufaa ya Kitete.
Tatizo la ukosefu la ukosefu wa vifaa vya kuokolea vilisababisha maiti
ya mtu huyo kukaa muda mrefu akiwa amebanwa na Lori hilo ambalo ni mali
ya kampuni ya mkandarasi JOSSAM
Awali jitihada za Polisi na wananchi ziligonga mwamba na kubaki
wakiiangalia maiti hiyo pasipo msaada wowote ajali ambayo imetokea
majira ya saa kumi jioni hapo jana.
Askari wa usalama barabarani wakiongozwa na kamanda wa Polisi kikosi
cha usalama barabarani wilaya ya Tabora Bw.Swaleh Digega hatimaye
wakafanikiwa kuutoa mwili wa marehemu huyo na kuupeleka hospitali ya
mkoa wa Tabora Kitete kwa ajili ya kuuhifadhi....Hata hivyo Jeshi la
Polisi kwa kushirikiana na Sumatra wanakusudia kumfikisha mahakamani
mmiliki wa Lori hilo kwa kitendo cha kusafirisha mizigo na wanadamu
katika gari hilo lenye nambari za usajili T 702 ACR ambalo ni ISUZU TX
No comments:
Post a Comment