Ni katoto ka kike kenye afya teleee na ana siku tatu tu toka
kuzaliwa.Bahati mbaya amezaliwa katika mazingira ambayo mama yake
hayupo tayari kumlea na ilikuwa amtupe wasamaria wema wakaokoa jahazi.
Mama wa mtoto ndio huyu pichani anadai hana wazazi walifariki.Akawa
analelewa na dada yake huko Sinza na akapata ujauzito.Baada ya kupata
ujauzito dada akamfukuza nyumbani na aliyempa ujauzito akamkataa.
Kina mama pichani wakimwogesha mtoto baada ya kuzuia zoezi la mama kutupa mtoto
Inavyosemekana mama wa mtoto alienda dispensary kuchoma sindano mimba
itoke.Bahati nzuri mtoto siku zilikuwa zimetimia akamzaa.Alipozaliwa na
kuwa hai mama mtoto akawa hamtaki anataka kumtupa.Mama wa mtoto hamtaki
kabisaaaa mwanae.
Kina mama baada ya kuzima zoezi la mtoto kutupwa wakakaa na binti
kuelewa nini kinamsibu.Wakamuogesha mtoto na mama yake pia
akaogeshwa.Akapewa maneno ya kumsaidia kisaikolojia lakini haikusaidia
mama msimamo wake ukawa ule ule.Mama aliyekuwa akimuogesha mtoto yupo
radhi kumchukua mtoto na kumlea kama wa kwake maana mama yake hamtaki.
Niliwahi kuona movie zamani inafanania na hili binti mdogo alipata
ujauzito lakini hakuwa tayari kuwa mama na akamtoa mwanae kwa mtu na
mkewe waliokuwa wanamatatizo ya kupata mtoto.Alimtoa kwasababu yeye
asingeweza kulea na kumpa mahitaji yote.Yule baba na mkewe ndio
walikuwa wakihitaji mtoto zaidi yake.
No comments:
Post a Comment