Kiongozi wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda leo amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi mkoa wa Morogoro kujibu mashitaka matatu yanayomkabili ambayo ni kutotii amri halali, kutoa maneno yenye nia ya kuharibu imani za dini na kushawishi kutenda kosa.
Sheikh Ponda amefikishwa mjini Morogoro na helkopta
 ya jeshi la polisi majira ya saa tano asubuhi  chini ya ulinzi mkali 
ambapo askari waliimarisha ulinzi kwa muda wote huku kikosi cha kutuliza
 ghasia FFU wakiwa na silaha mabomu na mbwa ambapo hali hiyo 
imesababisha kusimama kwa baadhi ya shughuli zingine za kiofisi katika 
ofisi zilizopo jirani na mahakama ya hakimu mkazi wakati kesi hiyo 
ikiendelea ...
Akisoma shataka mbele ya hakimu mkazi Richard Kabate , wakili
 mkuu wa serikali kanda ya Morogoro Benard  Kongola amedai kuwa shekh 
Ponda anadaiwa kutenda makosa hayo matatu Agosti 10 mwaka huu majira ya 
jioni katika viwanja vya shule ya msingi kiwanja cha ndege manispaa ya 
Morogoro.
Katika shitaka la kwanza la shekhe Ponda anadaiwa 
kutotii amri halali ambapo shitaka la pili anadaiwa kutoa maneno yenye 
nia ya kuharibu imani za dini kwa kutoa maneno kuwa serikali iliamua 
kupeleka jeshi  Mtwara kushughulikia suala la vurugu iliyotokana na gesi
 kwa kuwaua na kuwatesa wananchi kwa sababu asilimia 90 ya wakazi wa 
Mtwara ni Waislamu. 
Shitaka la tatu linalomkabili shekh Ponda ni 
kushawishi na kutenda kosa ambapo anadaiwa kuwa alitoa maneno ya 
ushawishi kwa kuwataka  waislaam wasikubali uundwaji wa kamati za ulinzi
 na usalama za misikiti kwani zinaundwa na Bakwata ambao ni vibaraka wa 
CCM na serikali, na kama kamati hizo zitajitokeza aliwaamuru wafunge 
milango na madirisha ya misikiti kuwapiga.
  
Baada ya kusomewa mashitaka hayo shekh Ponda 
anayetetewa na mawakili wasomi Barthoromew Tarimo na Ignas Punge  alikataa mashataka yote matatu na hivyo upande wa mashitaka 
kupinga dhamana kwa madai kuwa shekh Ponda anatumikia kifungo cha nje na
 kwamba hakutakiwa kufanya kosa, hata hivyo anakabiliwa na makosa 
mengine.
 





 
No comments:
Post a Comment