MKANDA mzima wa askari bandia wa Kikosi cha Usalama Barabarani
(trafiki), James Juma Hussein (45) aliyekamatwa saa 1:30 asubuhi ya
Agosti, 14, 2013 maeneo ya Tabata Kinyerezi Mnara wa Voda, jijini Dar es
Salaam akiwa ndani ya sare zake za kazi, umepatikana....
Kwa nini James alikamatwa? Asubuhi hiyo, afisa mmoja wa trafiki mwenye
cheo cha ukaguzi alikuwa akipita eneo hilo kwenda kazini, alipomwona
James alisimamisha gari, akashuka kwenda kumsalimia.
Lakini alishangaa kuviona vifungo vya shati lake ni vya kawaida (vya
polisi vinatakiwa kuandikwa police force yaani ‘jeshi la polisi’),
akamtilia shaka.
Afisa huyo Alimkamata ‘askari feki’ huyo mkazi wa Kimara Matangini, Dar
na kumfikisha kwenye Kituo cha Polisi Stakishari, wilayani Ilala, Dar
akafunguliwa jalada namba STK/RB/15305/2013 KUJIFANYA ASKARI ili
taratibu za kisheria zichukuliwe juu yake.
Trafiki huyo alisema kuwa yeye ni mnyamwezi wa Tabora na ana wiki moja tangu ajifanye yeye ni trafiki.
Nguo nyeupe juu ya kofia niliitengeneza kienyeji, krauni, tepe za
usajenti na mkanda ni za shemeji yangu alikuwa polisi Tabora, ni
marehemu, alikuwa akiitwa Shaban.
James aliwaambia polisi kuwa suruali nyeupe ya kitrafiki aliishona
mtaani lakini kamba ya filimbi na kizibao cha kung’ara vilikuwa vya
polisi.
Askari: Uliwahi kuwa polisi?
James: Niliwahi kupata mafunzo ya upolisi katika Chuo cha Polisi Moshi
(CCP) mwaka 1990-91 lakini nilifukuzwa kazi kwa sababu nilikwenda
muziki vitu ambavyo havitakiwi kufanywa na polisi. Nilirudi Tabora nikawa mkulima na mke wangu na mtoto mmoja ambao
wote sasa ni marehemu.
Ndani ya nguo za kitrafiki alizokuwa amevaa James, alikutwa na suruali ya bluu na fulana ya kijani.
James alisema njaa ndiyo iliyomfanya ajifanye trafiki na ‘kuwapiga
mikono’ madereva, hasa wa daladala ili anapowakuta na makosa kwenye
magari yao ajipatie chochote.
Kamishina wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP Suleiman Kova amethibitisha kukamatwa kwa polisi huyo feki
No comments:
Post a Comment