Mkunga huyo akionyesha mkeka unaotumika kuwatandikia wajawazito wanaokuja kujifungulia katika kliniki yake
Mkunga
akionyesha vibali vinavyothibitisha ruhusa aliopewa na Serikali kwa ajili ya
kutoa huduma ya kuwazalisha akina mama wajawazito.
Mwanamke mmoja anayejulikana kwa jina la MATRIDA ERICK mwenye umri wa miaka ishirini mkazi wa magamba ,wilaya ya chunya
,amejifungua mtoto jinsi ya kiume na wakati huohuo na chura.
Mkunga aliyemzalisha bi AGGRIPINA SIKANYIKA mkazi wa MBUYUNI
wilaya ya chunya amesema tukio hilo limetokea majira ya saa tisa alasiri agosti
13 mwaka huu,mara mwanamke huyo
kufikishwa kwa mkunga huyo na mumewe aitwaye BUNDALA JOSEPHAT ISANDU mwenye
umri wa miaka thelathini na tano
MATRIDA amesema huo ni uzao wake wanne na kwamba alishangazwa na kiumbe hicho
ingawa wakati anajifungua hakupata tatizo
lolote na pia alifurahia kupata mtoto wa kiume mwenye afya na
alisikitishwa kupata hicho kiumbe ambacho kilikuwa na miguu ya mbele yenye
vidole vinne na miguu ya nyuma vidole vitano vya binadamu.
Kwa upande wake AGGRIPINA amesema mtoto alikuwa katika kondo
lake na chura alikuwa katika kondo lake la nyuma la uzazi wa mwanamke huyo na
pia ameeleza kuwa hilo ni tukio la tatu ambapo la kwanza mwanamke alijifungua kichwa cha ng’ombe
mwaka jana na la pili mwaka huu mwezi wa tano ambapo mwanamke alijifungua chura
badala ya binadamu kwa hiyo hili ni tukio la tatu hivyo hakushangazwa na tukio hilo.
Hata hivyo mume wa Matrida amesema katika familia yao hilo
ni tukio la kwanza na kwamba limewashangaza.
Baada ya tukio hilo mkunga alimtafuta mwenyekiti wa kijiji
cha MBUYUNI bwana CONRAD WAMBOKA ambaye alimtaarifu mtendaji wa kijiji MICHAEL
SANZIMWA ambao walishuhudia tukio hilo na walimwamuru mkunga huyo kuondoa
kiumbe hicho ‘’CHURA’’ kwenye kondo la uzazi.
Aidha chura hicho kilikufa na ndugu siku moja baadae ambapo
ndugu walikabidhiwa na taratibu za mila zilifuatwa.
Baadhi ya ndugu wamehusisha kitendo hicho na imani za
kishirikina zilizokithiri huko wilayani chunya.
|
No comments:
Post a Comment