MSANII na mtayarishaji wa filamu Bongo Zahra Chambo Mohamed aka Zamo anasema kuwa anachukizwa sana na tabia ya baadhi ya watu ambao wamekuwa wakimuongelea bila kujua ukweli kuhusu maisha yake halisi, jambo ambalo limekuwa likimkwaza hasa ni kuambiwa yeye ana jinsi mbili kitu ambacho si kweli na kwanini wamuongelee vitu hivyo?
“Mtu anasema kuwa mimi nina jinsi mbili aliwahi kunichungulia hadi aseme hivyo, na kama kweli sasa mimi ninajisaidiaje nikiwa na jinsia mbili jamani? Watu wanapoteza muda wao kwa kunijadili mimi kuhusu jinsia yangu iwasaidie nini siku hizi kuna mambo ya utandawazi, unaweza kumuona mtu yupo hivi au vile lakini isiwe jibu sahihi kwako, jibu ni Question Mark,” anasema Zamo.
Msanii huyo amelalamika kwa kusema kuwa kuna mtangazaji mmoja wa Televisheni alimletea matatizo sana katika familia yake baada ya kuongelea vitu ambavyo yeye anasema vya kijinga kwa kushangaa jina lake kitu ambacho alisema ni tofauti na malengo, akiongea na mtandao mahiri wa habari za filamu Bongo anasema kuwa kuanzia sasa hatokuwa na urafiki na watu au watangazaji wanaotaka kiki kutoka kwake.
Hivi sasa Zamo anatamba na filamu yake ya Question Mark sinema anayosema inaelezea maisha yake kwa asilimia kubwa, na hata wale wenye mashaka na jinsia yake waitafute na kuiangalia kwa ajili ya maisha halisi ya Zamo na kumaliza utata kuhusu yeye ni nani?
No comments:
Post a Comment