Pages

Translate

Friday, 23 August 2013

TFF: YANGA WAMEONGEZA ADHABU YA MRISHO NGASSA



Mrisho Ngassa.
Na Khatimu Naheka
IMEFAHAMIKA kuwa Klabu ya Yanga, ndiyo iliyochangia ukubwa wa adhabu aliyopewa kiungo wake mshambuliaji Mrisho Ngassa, Championi Ijumaa limebaini.
Taarifa hiyo inakuja wakati ambao Ngassa amefungiwa kucheza mechi sita za mashindano pamoja na kuilipa Simba jumla ya shilingi milioni 45, sababu kubwa ikiwa ni kusaini mikataba miwili, ule wa Yanga na ule wa Simba.
Boniface Wambura ambaye ni Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ameliambia Championi Ijumaa kuwa, adhabu ya kufungiwa michezo sita kwa Ngassa imewekwa maalum, kutokana na Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji kutaka mchezaji huyo apate uchungu wa makosa aliyoyafanya na siyo kutegemea kulipiwa na klabu.
Wambura alisema adhabu hiyo imetokana na kasumba ya klabu mbalimbali ambazo zimekuwa zikiamua kulipa faini wanazokatwa wachezaji wao kwa makosa mbalimbali, maamuzi ambayo yanasababisha wachezaji kurudia makosa hayo.
“Adhabu kama hii ni maalum kuweza kumfanya mchezaji aone makali ya kosa alilofanya ili asiweze kurudia wakati mwingine, kamati imebaini kuwa makosa kama haya kila wakati yanakuwa yakijirudia kwa kuwa klabu ndizo zinazosababisha hilo,” alisema Wambura na kuongeza:
“Hata huku TFF, tunaona jinsi klabu zinavyofanya, endapo mchezaji fulani anapofanya makosa na kuhukumiwa utaiona klabu ndiyo inakuja na kuilipa faini husika, maamuzi kama hayo yanasababisha mchezaji asijue makali ya makosa anayofanya, ndiyo maana adhabu hii ikawa kali zaidi.”

No comments:

Post a Comment