BODI YA UKAGUZI YAIPIGA STOP FILAMU YA FOOLISH AGE YA LULU
Bodi ya ukaguzi wa filamu na michezo ya
kuigiza nchini imeipiga stop filamu ya Foolish age ya msanii wa kike
mwenye mvuto Bongo Elizabeth Michael ‘Lulu’ baada ya kukuta picha zilizo
nje ya maadili ya Kitanzania katika filamu hiyo, filamu hiyo ambayo
ilipanga kuzinduliwa mwezi huu tarehe 30 katika ukumbi wa Mlimani City
inahitaji marekebisho.
Kikwazo kilichoikumba filamu hiyo ni nguo
fupi zilizotumika katika waigizaji walioshiriki katika filamu hiyo
ambayo inatabiriwa kufanya vizuri katika soko la filamu Bongo kama
itafanikiwa kuzinduliwa na kuingia sokoni, juhudi zinafanyika
kuhakikisha kuwa marekebisho yanafanyika ili kwenda na ratiba kama
ilivyopangwa.
Hivi sasa baada ya urasimishaji wa filamu mamlaka na taasisi zinazohusika na masuala ya filamu zimekuwa makini na kuhakikisha kuwa filamu zinazoingia sokoni na zile zinazozinduliwa kukaguliwa kabla ya kufanyika kwa matukio hayo kama ilivyokuwa awali, kama filamu hiyo ya Foolish age itashindwa vigezo vya madaraja yanayotolewa na Bodi hiyo haitaonyeshwa.
Lulu ndio mwigizaji bora wa kike kwa mwaka 2013 kupitia tamasha la filamu la kimataifa la ZIFF katika kipengere cha tuzo za Bongo movie kilichopewa jina la Zuku Bongo movie Awards zilizotolewa katika ukumbi wa Ngome Kongwe.

Soma zaidi: http://mwanahabariuswazi.blogspot.com/2013/08/bodi-ya-ukaguzi-yaipiga-stop-filamu-ya.html#ixzz2cotm3ptI
No comments:
Post a Comment