Wananchi wakiwa wamekusanyika eneo la mlipuko nje ya msikiti wa Sunni uliopo jijini Tripoli, Lebanon.
Wananchi wakiangalia uhalibifu uliotokea baada ya mlipuko.
Magari yaliyohabiriwa katika mlipuko huo.
Mwananchi huyu akchukua picha katika simu yake ya mkononi.
(PICHA ZOTE NA AP)
MILIPUKO mikubwa miwili imetokea leo nje
ya misikiti katika jiji la Tripoli lililopo Kaskazini mwa Lebanon
jirani na Syria. Katika milipuko hiyo, watu 27 wanadaiwa kupoteza
maisha, wakati 350 wakijeruhiwa. Milipuko hii imeongeza mvutano nchini
Lebanon ikiwa ni matokeo ya vita ya wenyewe kwa wenyewe inayoendelea
nchini Syria kati ya wafuasi na wapinzani wa utawala wa Rais wa Syria,
Bashar Assad.
No comments:
Post a Comment