Mnamo tarehe 21/07/2012 majira ya saa 23:30hrs huko kijiji cha Nkwangu wilaya ya Chunya mkoa wa Mbeya, Seni Sandu, miaka 20, Msukuma, mkulima na mkazi wa Nkwangu aliuawa kwa kupigwa fimbo kichwani na Tolo Seko, miaka 20, Msukuma, mkulima na mkazi wa Nkwangu.
Chanzo ni ugomvi wa kumgombania msichana aitwaye Holo d/o Kulwa, miaka 16, Msukuma mkulima na mkazi wa Nkwangu.
Mtuhumiwa amekamatwa na taratibu za kumfikisha mahakamani zinaandaliwa.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya kamishna msaidizi wa polisi diwani athumani anatoa wito kwa jamii kutojichukulia sheria mkononi kwani ni kinyume cha sheria na kudhibiti hasira zao kwa kuyatatua matatizo ya kimapenzi kwa njia ya mazungumzo ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza.
Signed by, [Diwani Athumani – ACP] kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya.
No comments:
Post a Comment