Pages

Translate

Wednesday, 24 July 2013

TANSEED INTERNATIONAL NA MIKAKATI YA KUHAMASISHA WAKULIMA KUTUMIA MBEGU BORA YA MPUNGA YA TXD 306 'SARO 5' KATIKA BONDE LA WAMI-DAKAWA MVOMERO MOROGORO.

Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Joel Bendera (katikati) akidadisi jambo kwa Mkurugenzi wa Tanseed Inetrnational, Isaka Mashauri kulia kwake wakati wa maonyesho ya mbegu bora ya mpunga ya TXD 306 (Saro 5) katika shamba la mkulima wa zao la mpunga Nassibu Katoto mbele lililopo katika bonde la Wami-Dakawa wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro.  

Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Joel Bendera akifafanua jambo wakati akiongea na wakulima wa zao la mpunga baada ya mkuu huyo kutembelea maonyesho ya mbegu bora ya mpunga ya TXD 306 (Saro 5) kulia ni Mkuu wa wilaya ya Mvomero Anthony Mtaka na kushoto ni Mkurugenzi wa Tanseed Inetrnational, Isaka Mashauri.

Mkuu wa wilaya ya Mvomero Anthony Mtaka naye akizungumza jambo katika mkutano huo, kutoka kushoto ni, Isaka Mashauri na Mkuu wa mkoa Joel Bendera.
Mkurugenzi wa Tanseed Inetrnational, Isaka Mashauri kushoto akifafanua jambo kwa Mkuu wa mkoa Morogoro Joel Bendera.

Mkurugenzi wa Tanseed Inetrnational, Isaka Mashauri akielezea faida ya mbegu bora ya mpunga ya TXD 306 (Saro 5) mara baada ya Mkuu wa mkoa na viongozi mbalimbali wa serikali kutembelea maonyesho hayo kabla ya kuongea na wakulima.Sehemu ya shamba la mpunga lililopandwa mbegu bora ya mpunga ya TXD 306 (Saro 5).
Mkulima wa zao la mpunga, Veronica Urio akizungumza jambo kwa mkuu wa mkoa wa Morogoro (hayupo pichani) juu ya uhaba wa maji wanaopata wakulima katika mashamba ya umwagiliaji wa bonde la Wami-Dakawa yaliyopo wilaya ya Mvomero wakati wa maonyesho hayo.
 
Viroba vyenye mchele na meza yenye mchele na mpunga kwa ajili ya maonyesho ya mbegu bora ya mpunga ya TXD 306 (Saro 5).
  
Sehemu ya wakulima wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea.
  
Mkuu wa wilaya ya Mvomero Anthony Mtaka
Mkuu wa mkoa Joel Bendera akiangalia mchele huku akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Tanseed Inetrnational, Isaka Mashauri na kulia mwenye sharti ya kijani ni Mkuu wa wilaya ya Mvomero, Anthony Mtaka. 
 Mkurugenzi wa Tanseed Inetrnational, Isaka Mashauri kushoto akimwonesha Mkuu wa mkoa na wilaya ya mVomero wali uliopigwa kutokana na mchele wa mbegu bora ya mpunga ya TXD 306 (Saro 5).
 Wakulima wakiangalia mpunga na mchele wa mbegu bora ya mpunga ya TXD 306 (Saro 5).
 
Afisa Msindikaji na Mtaalamu wa Mapishi Kampuni ya Tanseed International, Skolastica Mashauri (mwenye fulana ya kijani) akipakua chakula kwa wakulima waliodhudria maonyesho ya mbegu bora ya mpunga ya TXD 306 (Saro 5). Kulia ni secretary wa kampuni hiyo, Caroline Chimtembo.

No comments:

Post a Comment