Naam, Tanzania yetu imewahi kuwa na viongozi
mbalimbali wabovu, lakini linapokuja suala la mawaziri wakuu, basi Mizengo
Kayanda Pinda, anaweza kabisa kuingia kwenye kumbukumbu kama WAZIRI MKUU MBOVU
KULIKO WOTE KATIKA HISTORIA YA NCHI YETU.
Ndio, Kuna Edward Lowassa,
aliyeng'oka kwa kashfa ya Richmond, lakini angalau yeye hakuwa m-babaishaji
katika kauli zake. N apengine kilichmosaidia Lowassa ni kutambua busara kuwa
mdomo sharti ushirikiane na ubongo kabla ya kutoa kauli yoyote ile.
Pinda, anayeitwa Mtoto wa Mkulima,
amekuwa maarufu zaidi kwa kauli zake za kipuuzi kuliko utendaji
kazi.Mbabaishaji huyo aliwahi kuzua sokomoko huko nyuma alipohalalisha MAUAJI:
kwa uzembe tu wa kufikiri, Pinda alidai kuwa anaguswa sana na mauaji ya
maalbino,kwahiyo ni ruksa kwa wananchi kuwauwa WATUHUMIWA wa mauaji hayo. Japo
kitaaluma mwanasheria, lakini Pinda hakuona tatizo katika kauli yake hiyo
ambayo kimsingi ilikuwa inahamisha nguvu za polisi na mahakama na kuzikabidhi
kwa umma.Kwa lugha nyingine, mzembe huyo alikuwa anahalalisha mob justice.
Badala ya ku-behave kama mtu mzima,
Pinda akenda bungeni na kujitetea kwa KULIA KAMA MTOTO.Lakini kwa bahati nzuri,
wengi wa wabunge wetu wapo bize zaidi na posho zao kuliko kuwatendea haki
wananchi wanaowawakilisha, na machozi hayo ya kinafiki ya Pinda yakamnusuru.
Katika kuonyesha kuwa Tanzania kwa
sasa ni kama haina Waziri Mkuu kwani Pinda anayeshikilia nafasi hiyo ni so
useless kiasi kwamba uwepo au kutokuwepo kwake hakuna tofauti, majuzi
akakurupuka tena na kauli nyingine ya kibabaishaji.Akatangaza kuwa ni ruksa kwa
polisi kupiga raia ZAIDI...Yaani kana kwamba unyanyasaji unaofanywa na polisi
hautoshi, na sasa wanahamasishwa kutoa vipigo zaidi.
Watu tumesema weee kuhusu kauli hiyo
ya kihuni lakini kwa vile aliyemteua Pinda kushika nafasi hiyo hana tofauti
sana na Pinda, Waziri Mkuu huyo bado yupo madarakani hadi dakika hii.
Na uwepo wake huo umepelekea ujinga
mwingine. Majuzi kumezuka sokomoko la kodi mpya ya SIM kadi.Badala ya kusikia
kilio cha mamilioni ya Watanzania wanaopinga kodi hiyo, mropokaji Pinda akadai
eti "wanaopinga
kodi hiyo hawaitakii mema nchi yetu..." COMPLETELY USELESS!
Bahati nzuri, safari hii Rais
Kikwete kaamua kutumia busara, na kwa namna flani, amemudu KUMUUMBUA PINDA.
Rais amezitaka mamlaka husika kukaa pamoja kutafuta ufumbuzi wa haraka kuhusu
kodi hiyo inayolalamikiwa na wananchi wengi. Rais aliyasema hayo alipokutana na
viongozi wa Wizara ya Fedha, na wale wa Wizara ya Sayansi na Teknolojia, na
Mamlaka ya Mawasiliano TCRA.
No comments:
Post a Comment