Pages

Translate

Wednesday, 3 July 2013

RAIS WA MISRI MOHAMED MORSI AMEPINDULIWA NA JESHI

  

 



Generali Abdul Fattah al-Sisi akizungumza moja kwa moja kutoka televisheni ya taifa ya Misri




Hatimaye jeshi la Misri limejitokeza live kwenye televisheni ya Misri na kutangaza rasmi kuifuta katiba ya nchi hiyo.

Generali Abdul Fattah Al-Sisi, amesema kuanzia sasa mwanasheria mkuu wa mahakama ya katiba ndiye atakuwa anakaimu madaraka yote ya raisi na kutangaza rasmi kutomtambua bwana Mohamed Morsi

Wapinzani wa raisi Morsi waliandamana na kukusanyika katika uwanja wa Tahrir Square na kuonekana wakishangilia kwa nguvu wakati Generali Abdul akitoa tangazo hilo la kumpindua raisi Morsi

Mchakato huo wa kumng'oa bwana Morsi ni kufuatia maandamano ya umma ya siku nne kumtaka raisi huyo aachie madaraka na kutii amri ya jeshi ambayo imeisha usiku wa leo

Aidha kituo cha TV kilichokuwa kikimilikiwa na bwana Morsi cha Muslim Brotherhood kilizimika sekunde chache baada ya Generali Abduli kumaliza hotuba ya kumpindua rais Morsi aliyeingia madarakani baada ya kumpindua aliyekuwa raisi wa nchi hiyo .

No comments:

Post a Comment