Polisi Mbeya wakipambana kwa mikono na Lusajo Kabuje mkazi wa Iwindi Mbeya Vijijini baada ya Bunduki kugoma kufanya kazi ambapo mmoja wa askari alipata majeraha ya visu alivyokuwa navyo mtuhumiwa kabla hajadhibitiwa.
Baba mzazi wa mtuhumiwa. mzee Emmanuel Kabuje ambaye pia alikusudiwa kuuawa na kijana wake, akizungumza na kalulunga blog eneo la tukio muda mfupi baada ya mwanae kukamatwa na polisi.
Ujumbe aliouandika kijana Lusajo kabla hajatimiza adhima yake ya kufanya mauaji ya kutisha kwa mkewe, Baba yake mzazi, Dada yake na kisha kujiuua yeye mwenyewe.
Makazi ya mtuhumiwa
Wananchi wakishangaa baada ya kukamatwa mtuhumiwa huyo
Jeneza likiwa ndani katika nyumba ya mtuhumiwa
Polisi wakiwa wamemdhibiti mtuhumiwa Lusajo Kabuje eneo la Isanga kijiji cha Iwindi wilaya ya Mbeya mkoani Mbeya leo Julai 2, 2013.
Kulia ni askari kanzu akiwa na moja ya kisu alichotaka mtuhumiwa kumchoma askari huyo kifuani kabla ya kudhibitiwa ambapo askari huyo alilazimika kukidaka kisu hicho kwa kushika sehemu ya makali.
Mke wa mtuhumiwa. Oliver Mwaluanda akizungumza baada ya kujitokeza kutoka mafichoni baada ya mumewe kukamatwa na polisi. Oliver akisema kuwa aliruka ukuta huku akiwa na mtoto mgongoni kwa ajili ya kunusuru maisha yake baada ya kuona mumewe anataka kumuua kikatili.
Baadhi
ya wananchi wa kijiji cha Iwindi wakitoa jeneza ndani kwa Lusajo Kabuje
na kwenda kulipakia kwenye gari la polisi ambapo mtuhumiwa alipoambiwa
alale ndani ya jeneza hilo alikataa huku akisema kuwa anaogopa...
KIJANA
Lusajo Kabuje mkazi wa kitongoji cha Isanga kijiji cha Iwindi wilaya ya Mbeya
Vijijini mkoani hapa, amekamatwa na polisi kabla ya kutekeleza mpango wake wa
kufanya mauaji ya kutisha kwa ndugu zake.
Mtuhumiwa
huyo alikamatwa na polisi majira ya saa 11;24 jioni eneo la klabu ya pombe ya
Isanga Julai 2, mwaka huu huku akiwa na visu viwili ambavyo alikusudia kufanyia
unyama huo huku akiwajeruhi polisi waliofika kumkamata kabla hajatekeleza
adhima yake hiyo ovu.
Kabla ya
kukamatwa, mtuhumkiwa alitaka kumchoma kisu kifuani mmoja wa askari nwaliofika
eneo hilo ambapo askari huyo aliyekuwa amevaa nguo za kiraia alifanikiwa
kukwepa na kukamata kisu hicho sehemu ya ncha kali huku askari aliyeshika
bunduki, risasi zikiwa zinagoma kuingia kwenye Magazine ili kufyatua risasi
juu.
Baada ya
kumkamata na kumvisha pingu, askari polisi walifika nyumbani kwake na kukuta
jeneza, mslaba, katoni ya chumvi na mafuta ya kupikia ambavyo vyote aliviandaa
kwa ajili ya mazishi yake, mkewe, Baba yake mzazi na Dada yake.
Baba mzazi
wa Lugano, Emmanuel Kabuje, alimwambia mwandihi wa habari hizi kuwa kijana wake
hajawahi kuwa na matatizo ya akili lakini Juni 28, mwaka huu alimtishia kumuua
kwa kumkatakata vipande.
‘’Hajawahi
kuugua ugonjwa wa akili lakini tarehe 28, mwezi wa sita alinitishia kuniua
ndipo nikaenda kutoa taarifa kituo cha polisi Mbalizi’’ alisema Kabunje.
Mke wa mtuhumiwa
asema aliruka ukuta kujiokoa
Mke wa
mtuhumiwa huyo Oliver Mwaluanda, alijitokeza na watoto wake watatu kutoka
mafichoni ambako walishinda na njaa kutoka majira ya saa tisa alasiri.
Baada ya
mumewe kukamatwa na polisi, Oliver alijitokeza mbele ya umati wa wananci na
kuwashukuru kufanikiwa mumewe kukamatwa kabla hajatekeleza adhima yake ya
kumuua yeye, wifi yake, Baba Mukwe na mtuhumiwa mwenyewe.
‘’Alikuwa
akinipiga mara kadhaa na aliyekuwa akiniokoa ni Baba mukwe na ndiyo chanzo cha
kumchukia na aliahidi kuniua kwa kutumia shoka, muache aende labda leo na
watoto wangu tutaweza hata kula chakua kwa uhuru’’ alisema Oliver huku akiwa na
watoto wake wakitetemeka kwa baridi baada ya kutoka mafichoni.
Alisema kuwa,
mchana alifika nyumbani hapo na kumwambia kwa yeye si binadamu wa kawaida bali
siku hiyo atakufa na kufanya mauaji mengine kabla yeye hajajiua ambapo
naliahidi kumuua dada yake aitwaye Mariam Kabuje.
Alipoulizwa matatizo
ya mumewe anayoyafahamu, alisema kuwa hakuwa na matatizo ya akili bali tatizo
lake alikuwa akinywa sana pombe aina za viroba ambazo anahisi kuwa zilichangia
kufikia hatua hiyo ya kutaka kuchukua maamuzi ya kufanya mauaji.
Baadhi ya
wananchi wanaoifahamu familia hiyo, walisema kuwa mzee Kabuje alipewa taraka na
mkewe miaka mingi hali iliyompelekea kukataa kuoa mke mwingine akiwahofia
watoto wake kuteswa na mama wa kambo na kufanya jitihada za kuwasomesha watoto
wake wote ambapo baadhi ni wafanyabiashara na mmoja yupo chuo kikuu.
No comments:
Post a Comment