Dar es
Salaam. Ofisa mmoja wa Usalama wa Marekani (FBI), akiwa na mbwa jana
aliingia Makao Makuu ya Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam na kufanya
ukaguzi.
Tukio hilo lilitokea muda mfupi kabla ya msafara wa
magari ya Marekani kupita yakitokea Ikulu kwenda Uwanja wa Ndege wa
Julius Nyerere kumlaki Rais Barack Obama.
Polisi ambaye hakutaka kutajwa alisema ofisa huyo aliingia na mbwa hadi maeneo ya mapokezi, lakini muda mfupi walitoka.
“Walikwenda
moja kwa moja mapokezi wakafanya ukaguzi, kisha wakatoka nje ya jengo
na kama hiyo haitoshi, ofisa huyo akiwa na mbwa alikwenda sehemu ya
kuegesha magari yenye kesi na yale ya kawaida na kuanza kufanya ukaguzi,
baada ya hapo waliondoka,” alisema polisi huyo na kuongeza:
“Licha
ya mimi kutokuwa na cheo pale, lakini hili la kutukagua na mbwa, ni
kama wametudhalilisha... sisi ndiyo tunaaminika kwa usalama, leo hii
wanatukagua na mbwa. Tena Kituo Kikuu.”
Hata hivyo, usalama
kwenye vituo vingi ikiwamo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Juliusu
Nyerere, vilikuwa chini ya usimamizi na uangalizi wa makachero wa
Marekani.
No comments:
Post a Comment