Pages

Translate

Monday, 1 July 2013

AFUNGWA MAISHA KWA KESI YA KUKATA UUME WA MUMEWE



 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
Mwanamke mmoja wa California ambaye alituhumiwa kukata uume wa mumewe kabla ya kuutupa kwenye mashine ya kusagia taka amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani.

Catherine Kieu, mwenye miaka 50, alipatikana na hatia ya mashitaka ya kutesa na kosa la kuharibu viungo vya mwili katika shambulio la Julai 11, 2011 na kuhukumiwa kifungo cha maisha jela, lakini anaweza kufikiriwa kupewa msamaha baada ya kutumikia miaka saba.

Alitiwa hatiani Aprili kwa kila kosa moja la kutesa na kuharibu viungo vya mwili.
Muathirika, anayefahamika kama Glen wakati wote wa kesi, alikuwa mahakamani kwa ajili ya hukumu ya jana.

"Natumaini hii itakuwa mara ya mwisho kabisa ninayoweza kumwona," alisema Glen. "Najihisi nafuu kiasi fulani, na ilikuwa siku ya huzuni kubwa kwangu."

Muathirika huyo alikimbizwa hospitali, lakini upasuaji kurejesha uume wake haukufanikiwa.
Wakati wa kesi hiyo, muathirika huyo mwenye umri wa miaka 60 alitoa ushahidi kwamba uume wake hauwezi tena kuunganishwa mahali pake na kwamba anahisi kama ameuawa.

Kieu alikuwa na wivu na hasira kuhusu mipango ya mumewe kumpa talaka sababu alimwona rafiki yake wa zamani wa kike, upande wa mashitaka ulisema.

Kieu alipigilia msumari mlo wa jioni wa mumewe kwa Ambien, akimfunga kitandani kwake kwa kamba za nailoni na kisha kumkata kabisa uume wake kwa kutumia kisu cha jikoni chenye urefu wa inchi 10, kwa mujibu wa upande wa mashitaka.

Kisha akautupa uume huo kwenye mashine ya kusagia taka na kukiharibu kabisa kiungo hicho, mamlaka zilisema.

Mumewe alitibiwa na kuruhusiwa kutoka kwenye Kituo cha Afya cha UC Irvine, lakini madaktari hawakuweza kurejeshea uume wake.

Wanandoa hao waliripotiwa kuwa kwenye mchakato wa kuachana wakati huo, na upande wa utetezi ulibisha kwamba Kieu alikuwa akisumbuliwa na mfadhaiko na masuala mengine ya afya ya kiakili.

No comments:

Post a Comment