Binti mdogo wa rais Barack Obama,
Sasha, alikua jijini New York hivi karibuni akifanya shopping huku
amevaa kikaptura kifupi (short shorts, al maarufu kama daisy dukes.) Mapaparazzi
walimpiga picha binti huyo akiwa mitaani na raha zake na kuuliza
mitandaoni kama ni sahihi kwa binti wa miaka 12, kuvaa kaptura fupi
hivyo. Kama kawaida za mitandaoni, kilichozuka ni ubishi mkali kati ya
wanaoona si sahihi, hasa kwa binti ya rais, na wale wanaoona ni poa tu.
Wewe upo kwenye camp ipi? Unaweza ruhusu binti yako avae kaptura kama
hii?
No comments:
Post a Comment