Pages

Translate

Tuesday 30 July 2013

MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU ARUSHA AUNDA NDEGE


Picha ya ndege inayoundwa na kijana, Denis
KIJANA wa Kitanzania ambaye pia ni mwanafunzi wa Chuo kikuu cha Arusha aitwaye Denis, amefanikiwa kuunda ndege ya abiria. Kijana huyo alianza kuiunda ndege hiyo zaidi ya miezi mitatu iliyo pita na sasa ipo katika hatua za mwisho kabla hajaifanyia majaribio.

Hii ni mara ya pili kwa kijana huyu kuunda ndege baada ya kufanya majaribio mengine huko mkoani Mara ambayo yalikuwa na matunda mazuri. Ndege inayo endelea kutengenezwa na kijana huyu ipo katika eneo la Chuo kikuu cha Arusha kilichopo katika mji mdogo wa Usariver karibu na hifadhi ya wanyama ya Arusha (Arusha National Park).

Endapo majaribio ya Denis yakifanikiwa basi atakuwa ameipeperusha vyema bendera ya Tanzania na Africa kwa ujumla. Ni wito wangu kwa Serikali na taasisi binafsi kujitokeza na kumuunga mkono kijana huyu katika majaribio haya makubwa na yakimapinduzi.

ATEMBEA SIKU 4 AKITAFUTA HUDUMA YA HOSPITAL

Nilitembea kwa miguu siku nne kwenda Ludewa kutafuta hospitali huku nikiwa na uchungu wa uzazi."
 
Aliyepata adhani hiyo ni Maria Haule, mkazi wa Lupingu, anayeishi kwa kutegemea kilimo kweye mwambao wa Ziwa Nyasa, mkoani Njombe.
 
Maria ana umri wa miaka 47, alilazimika kutembea kwa miguu kwenda hospitalini Ludewa baada ya kujifungua kienyeji nyumbani kwake Lupingu, lakini mfuko wa uzazi – Placenter ulichelewa kutoka.
 
Ukosefu wa huduma ya uzazi katika kituo cha afya cha Lupingu, ulisababisha Maria  kutembea kwa miguu hospitali ya wilaya ya Ludewa huku mfuko wa uzazi ukining’inia.

Mbali na zahanati ya Lupingu kukosa huduma ya uzazi, pia haina wataalamu, lakini pia umbali kati ya Lupingu na Ludewa ni tatizo ingine kwa sababu hakuna usafiri wa uhakika.


“Ilikuwa safari ngumu ya siku tatu, kupita mbugani usiku na mchana kabla ya kufika Ludewa siku ya nne, mfuko wa uzazi ukiwa unaning'inia,” anasimulia Maria.

Maria hajui umbali kati ya maeneo hayo, lakini anasema inachukua saa nane hadi 10 kutembea kwa miguu kutoka Lupingu kufika Ludewa.

Anasema yeye akiwa mgonjwa alishindwa kutumia muda huo kufika Ludewa, badala yake alifika siku ya nne baada ya safari ya siku tatu mbugani.

Kwa mujibu wa Maria, hospitali ya Ludewa inahudumia watu wengi ambao ni wakazi wa vijiji 76 vya wilaya hiyo.

Anasema juhudi ya kuomba msaada ili aweze kupata usafiri wa gari ilikwama kwa sababu kila aliyemfuatwa kuelezwa shida hiyo alikubali kusaidia lakini kwa malipo makubwa.
 
Anasema kutokana na hali hiyo ilibidi atembee kwa miguu baada ya kukosa fedha za kuwalipa wenye gari ili wamkibize kwenda hospitalini.

“Kabla ya kuamua kutembea niliomba watu wanisaidie, mmoja mwenye gari akaniambia nimlipe sh. 100,000, sikuwa na fedha kabisa,” anasema Maria.

Anasema baada ya kukosa msaada akaanza safari ya kuvuka vilima na mabonde, akilala njiani kila jua linapokuchwa.

Lakini anashukuru, baada ya kuwasili hospitalini madaktari wa hospitali ya Ludewa na wasaidizi wao walimhudumia haraka.

“Madaktari, manesi na wahudumu walisaidia sana kuokoa maisha yangu, hatimaye mfuko wa uzazi ulitoka,” anasema Maria.

Anaongeza kuwa, “kwangu ulikuwa muujiza madaktari waliponiambia wamefanikiwa kuutoa mfuko wa uzazi.”

Mtoto wa kiume wa Maria aliyezaliwa na kufuatiwa na tatizo la mfuko wa uzazi wa mama yake kugoma kutoka hivi sasa anasoma ana umri wa miaka mine.
 
Theresia Kiowi,  pia mkulima  wa Lupingu anasema ukosefu wa huduma ya uzazi ni tatizo sugu linalotishia maisha ya wajawazito.

Anasema mbali na Lupingu, vijiji vya Makonde, Lifuma, Sumba na Nsisi pia vina matatizo ya aina hiyo na pia ubovu wa barabara.
 
Ukosefu wa huduma ya uzazi hauathiri wazazi peke yao, kwani hata watoto wanaozaliwa pia wanakosa huduma mbali mbali za awali ambazo ni pamoja na chanjo.

Maria anajua hilo ni tatizo la maeneo mengi ya vijijini, lakini anaamini hali n mbaya zaidi Lupingu kwa sababu zahanati iliyopo inahudumia watu wengi.

Anasema pamoja na athari nyingine, ukosefu wa huduma ya uzazi kijijini ni hatari kwa sababu unaweza kusababisha wazazi kupoteza maisha wakati wa kujifungua.

Wataalam wanasema mama kujifungua kuna hatua nyingi, ni pamoja na mtoto kutoka salama na mfuko wa uzazi kutoka, usipotoka kwa wakati mzazi anaweza kupoteza maisha.

Apaa Nkya, ni ofisa muunguzi katika hospitali ya Lugalo, inayomilikiwa na Jeshi la Wananchi Tanzania(JWTZ) jijini Dar es Salaam.

Anasema kwa kawaida mfuko wa uzazi unapaswa utoke dakika chache, mara tu baada ya mama kijifungua salama.

Anasema hali ya mfuko wa uzazi kugoma kutoka inaweza kusababisha mzazi kupoteza maisha kwa kutokwa damu nyingi na vle vile iwapo atakosa huduma.

Apaa anasema chanzo cha mfuko huo kugoma kutoka kunasababishwa na matatizo mbali mbali ya kiafya, kama vile upungufu wa baadhi ya madini mwilini.

Anasema matatizo hayo yanatokana na mfuko huo kutojiachanisha kwa urahisi kutoka kwenye kuta za mji wa uzazi – Uterus.

Anasema mama anapokuwa mjauzito, mfuko wake wa uzazi ujitengeneza ndani ya mji wa uzazi, kama ilivyo kwa matunda ndani ya ganda lake.

Mfuko wa uzazi ukikosa aina fulani ya madini yenye kufanya usishikane, unang’ang’ania kwenye kuta za mji huo wa uzazi unaoitwa uterus, anasema Apaa.

Anasema njia inayotumika kuokoa maisha ya mama mwenye tatizo hilo, wataalamu huingiza mkono kupitia njia ya uzazi na kuutoa mfuko huo.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman  Kinana ni miongoni mwa viongozi wa ngazi ya juu nchini wenye uelewa wa kutosha juu ya matatizo ya uchumi na kijamii wilayani Ludewa.

Hivi karibuni alifanya ziara ya mkoa wa Njombe na miongoni mwa mambo aliyoshuhudia ni pamoa na huduma duni katika sekta mbali mbali, afya na barabara zikiwamo, ndio maana wakati wa ziara yake akaahidi zahanati hiyo itatengenezwa na kupandishwa hadhi kuwa kituo cha afya. 
 
Kinana pia aliahidi kupeleka Ludewa jumla ya mabati 500 na mifuko ya saruji 700 kwa ajli ya utengenezaji wa hospitali Lupingu.

Pamoja na Kinana Mbunge wa jimbo hilo Deo Filikunjombe kwa upande wake tayari ametoa sh. milioni 400 kwa ajili ya maboresho ya barabara kati ya Lupingu na Ludewa.

"WAPIGWE TU" YA MIZENGO PINDA


KAULI ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ya kubariki vyombo vya dola kuendeleza kipigo kwa raia wanaokaidi amri imechukua sura mpya baada ya Kituo cha Sheria na Haki za Bindamu (LHRC) kutangaza kumburuza mahakamani wiki hii kutokana na kushindwa kufuta kauli yake.


Juni 20, mwaka huu, wakati akijibu maswali ya papo kwa hapo bungeni, Waziri Mkuu, Pinda, alivitaka vyombo vya dola kuendelea kuwapiga raia, akisema kuwa hakuna namna nyingine kwani serikali imechoka.


Kauli hiyo imekuwa ikipingwa na wananchi, mashirika ya kutetea haki za binadamu na wanasiasa wakimtaka Waziri Mkuu, Pinda, kuifuta kwa kuomba radhi, wakidai kuwa inachochea uvunjifu wa sheria.


Akitangaza kusudio la kituo hicho kufungua kesi dhidi ya Pinda, Mkurugenzi wa maboresho na utetezi, Harold Sungusia, alisema hadi jana walikuwa tayari wameandaa kusudio la shtaka lao.


Alisema kuwa kisheria kilichowafanya kufikia uamuzi huo ni kutokana na waziri mkuu huyo kukiuka Katiba ya nchi inayozungumzia usawa mbele ya sheria.


“Kitendo alichofanya waziri mkuu cha kuwaruhusu polisi kupiga wananchi hakikubaliki hata kidogo na walitegemea kwamba angeomba radhi kutokana na kauli yake hiyo tangu alivyoshinikizwa kufanya hivyo na makundi mbalimbali.


“Badala yake ameendelea kuwa kimya licha ya mkubwa wake, Rais Jakaya Kikwete, hivi karibuni kukiri kwamba mtendaji wake huyo aliteleza,” alisema.


Sungusia aliongeza kuwa Alhamisi wiki hii wataweka bayana kwa waandishi wa habari ni wapi kesi hiyo itafunguliwa.


Pinda alitoa kauli hiyo tata ambayo imehojiwa na wengi wakati akijibu swali la Mbunge wa Kilwa Kaskazini, Murtaza Mangungu (CCM) aliyehoji kama serikali iko tayari kutoa tamko kuhusu vurugu zilizotokea jijini Arusha, Mtwara na maeneo mengine pamoja na hatua ya vyombo vya dola kutumia nguvu.


Katika majibu yake Pinda alisema kuwa suala la amani linawagusa wote, kwamba jukumu ni kwa viongozi wa kisiasa. Alifafanua kuwa kama viongozi wa kisiasa hawatafika mahali wakakubaliana bila kujali vyama vyao nchi itafika pabaya.


Pinda alifafanua kuwa kwa upande wa serikali lazima wahakikishe kwamba wale wote wanaojaribu kuvunja amani kwa namna yoyote ile kazi waliyonayo ni kupambana kweli kweli kwa njia zozote zinazostahili.


“Mimi naomba sana Watanzania, maana kila juhudi zinazoonekana zinaelekea huko, tunapata watu wengine wanajitokeza kuwa mara unajua…unajua. Acheni serikali itimize wajibu wake, kwa sababu jambo hili ni la msingi na wote tulilinde kwa nguvu zetu zote.


“Mheshimiwa Mangungu umeanza vizuri lakini hapa unasema vyombo vya dola vinapiga watu. Ukifanya fujo unaambiwa usifanye hiki, ukaamua wewe kukaidi, utapigwa tu,” alisema.


Waziri mkuu aliongeza kuwa hakuna namna nyingine, maana lazima watu wakubaliane na serikali kwamba nchi hii wanaiendesha kwa misingi ya kisheria.


“Sasa kama wewe umekaidi, hutaki, unaona kwamba ni imara zaidi, wewe ni jeuri zaidi, watakupiga tu, na mimi nasema wapigwe tu, maana hakuna namna nyingine, tumechoka,” alisema

AOZWA KWA NGUVU NA KUBAKWA NA KUNDI LA WANAUME SIKU YA HARUSI...



Mwanamke wa India mwenye miaka 24 amelazimishwa kuolewa na kubakwa na kundi la wanaume kama adhabu ya 'heshima' baada ya kaka yake kutoroka na rafiki yake wa kike, imebainika jana.
Mwanamke huyo - ambaye hakuweza kutajwa kwa usalama wake - aliambiwa anatakiwa kuolewa na mume ambaye ni kaka wa mke wa mchumba mpya wa kaka yake kama 'kisasi' kwa uzinzi wa wawili hao.
Na ndani ya masaa kadhaa za kufunga pingu za maisha na mumewe mpya, akashambuliwa na kubakwa 'bila huruma' na kaka kadhaa wa mchumba wa kaka yake.
Kwa namna ya kushangaza, shambulio hilo ya kutisha lilidaiwa hata kupewa kibali na wazee wa kijiji hicho kilichopo makazi ya vijijini ya Uttar Pradesh, kaskazini mwa India, ambao walidai: "Jicho kwa jicho ni hukumu halisi."
"Ninakubaliana na uamuzi wao sababu ninajua kwamba kungekuwa na umwagaji damu katika kijiji hiki kama ningekataa kuolewa naye," mwanamke huyo aliwaeleza polisi.
"Mashemeji zangu walinibaka bila huruma siku hiyo hiyo niliyofunga ndoa. Ikawa utaratibu wa kawaida.
"Baba mkwe wangu alidai kwamba amekubaliana na ndoa yangu kwa vile alitaka kulipa kisasi (kwa familia yangu) namna hii."
Ajali hiyo mbaya imekuja kujulikana tu pale muathirika alipopata ujasiri wa kufungua madai hayo polisi.
"Machi 26, walifungua kesi dhidi ya kaka yangu na polisi walimkamata yeye na (mke wa mume wangu). Waliachiwa baada ya binti huyo kukiri mbele ya hakimu kwamba aliolewa naye kwa hiari yake," muathirika huyo alidai kwenye madai yake.
Baraza la kijiji au Panchayat, lilidaiwa kumlazimisha mwanamke huyo kuolewa baada ya kaka yake kuwa ametoroka na dada wa mumewe mtarajiwa mnamo Februari 15, mwaka huu.
Panchayat, ambalo liliketi ndai ya siku kumi baada ya kutokomea huko, lilitaka ndoa ya lazima. Mbali na hili, pia liliwataka wazazi wa mwanamke huyo kulipa Rupia 75,000 kama fidia kwa wakwe zake wapya.
Panchayat baadaye lilifafanua hali hiyo iliyojitokeza, likisema 'jicho kwa jicho ni hukumu halisi'.
Watuhumiwa hao wa ubakaji - wanafamilia wanaoshitakiwa -waliripotiwa kuweka bayana kwamba ilikuwa ni ulipizaji wao kisasi kwa kitendo cha utoroshwaji.
Mwanamke huyo kwa namna fulani alifanikiwa kukwepa majaribio yao ya kumkamata Julai 21, mapema asubuhi, na kufungua madai kwa polisi wa Muzaffarnagar mnamo Julai 27.
Mkuu wa polisi, Manzil Saini alisema: "Muathirika huyo amekutana nami. Kesi imefunguliwa chini ya Kifungu 376 ya IPC. Watuhumiwa watakamatwa hivi karibuni."
Kaka mkubwa wa muathirika huyo alidai uamuzi huo uliopelekea tukio hilo ulichukuliwa chini ya usimamizi madhubuti wa Panchayat.
"Polisi walitoa muda kwa watuhumiwa kuondoka kijijini hapo. Mume huyo wa chifu wa panchayat alikuwapo wakati tukio hilo la dada yangu likiamuliwa. Alikuwa msemaji mkubwa na kutaka adhabu kali mno dhidi yetu," alisema.
Mkuu wa panchayat alithibitisha uamuzi wake jana. Alidai aliwataka wafikie suluhisho la amani.
Tukio hilo limekuja wiki mbili baada ya mwanachuo mwenye miaka 20 kubakwa na kundi la wanaume na kisha kuchomwa moto huko Etawah, jimboni Uttar Pradesh, mkoa alikotokea Waziri Mkuu Akhilesh Yadav.
Katika kesi hiyo, kwa namna ya kushitusha, polisi hao si tu kwamba mwanzoni walikataa kufungua kesi lakini pia walionekana kukiuka wajibu wao wa kusimamia sheria na utii.

KESI YA LADY JAYDEE YAPIGWA KALENDA



MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kinondoni, leo imeiaharisha kesi inayomkabili msanii wa kizazi kipya nchini, Judith Wambura 'Lady Jaydee' a.k.a Annaconda dhidi ya uongozi wa Clouds Media Group hadi Agosti 2, mwaka huu.

Kesi hiyo ya madai iliyopo mbele ya Hakimu Athumani Nyamlani, leo ililetwa kwa ajili ya kusikilizwa lakini ilishindikana kutokana na wakili anayemtetea, Jaydee kutotokea mahakamani hapo na kumtuma mwakilishi wake.

Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa wakili huyo wa Jaydee, amekwenda katika Mahakama Kuu kuhudhuria kesi nyingine na hivyo kushindwa kufika mahakamani hapo kuendelea na kesi hiyo na hivyo kuahirishwa hadi Agosti 2, mwaka huu.

Kesi hiyo ya madai ilipelekwa mahakamani hapo na Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo wa Kampuni ya Clouds Media kwa madai ya kuukashifu uongozi huo.

Kwa mujibu wa mdai huyo, ambaye ni uongozi wa Clouds Media ulidai kuwa mdaiwa huyo ambaye ni Lady Jaydee aliandika maneno ya kuukashifu uongozi huo kupitia blogu yake.

MIAKA 30 JELA KWA KUMBAKA MWANAE NA KUZAA NAE

MAHAKAMA ya wilaya ya Mbeya imemhukumu kwenda jela miaka 30 mkazi wa Isanga Mkoani hapa baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumlawiti na kumzalisha binti yake wa kumzaa.

Yusufu Amani (39) aliyembaka mwanaye wa kumzaa kisha kumzalisha baada ya kutengana na mkewe Afungwa miaka 30
Hapa akijifunika sipigwe picha baada ya hukumu
Kulia ni mtoto aliyebakwa na baba yake kisha kuzalishwa akiwa na mtoto wake wakitoka mahakamani kulia ni mama mzazi wa binti aliyebakwa na kuzalishwa


MAHAKAMA ya wilaya ya Mbeya imemhukumu kwenda jela miaka 30 mkazi wa Isanga Mkoani hapa baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumlawiti na kumzalisha binti yake wa kumzaa akiwa na miaka 15( jina linahifadhiwa).



Mwendesha mashitaka wa serikali  Archiles Mulisa  aliiambia mahakamani hiyo Mbele ya Hakimu Gilbert Ndeuruo kuwa Mshtakiwa huyo ni Yusufu Amani (39) anayedaiwa kumbaka mwanaye wa kumzaa kisha kumzalisha baada ya kutengana na mkewe.



Alisema kosa hilo ni kinyume cha sheria kifungu cha 154 (1)a na 155 sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho  mwaka 2002, pamoja na kifungu cha 158(a) cha makosa ya kuzini.


akisoma Hukumu hiyo Hakimu Ndeuruo alidai kuwa Mtuhumiwa alianza kujihusisha kimapenzi na mwanaye Mwaka 2008 baada ya kutengana na mkewe ambapo Mtuhumiwa aliachiwa watoto wote.
Aliongeza kuwa wakati huo binti huyo alikuwa na umri wa miaka 12 na alikuwa akisoma shule ya msingi darasa la Tano jambo ambalo wamedumu nalo kwa Miaka mine hadi ilipogundulika kuwa binti alikuwa mjamzito Mei, 2012.
Alisema mbinu aliyokuwa akiitumia ni kumtishia binti asitoe taarifa kwa mtu yoyote na kwamba baada ya kugundulika kuwa na ujauzito alimwambia amsingizie kijana yoyote mtaani kwao.
Hakimu Ndeuruo alisema Mahakama ilimtia hatiani Mtuhumiwa kutokana na ushahidi wa Mhanga wa tukio hilo ambaye ni binti pamoja na ushahidi wa kitaalamu kutoka kwa Mkemia mkuu wa Serikali.
Alisema ushahidi wa Mkemia Mkuu wa Serikali baada ya kupima Vinasaba kutoka Mtuhumiwa, Mhanga na Mtoto aliyezaliwa ulidai kuwa  Mshtakiwa ndiye baba halali wa Mtoto kutokana na Maeneo 15 ya vipimo vya Vinasaba kati ya Baba na Mtoto aliyezaliwa kufungana kwa asilimia 99.9.
Aidha kabla ya kutoa hukumu Hakimu alimpa nafasi mtuhumiwa kujitetea ili apunguziwe adhabu au asiweze kuhukumiwa kabisa lakini hali ikawa tofauti baada ya Mtuhumiwa kujibu kuwa hana la kujitetea vyovyote itakavyokuwa anachotaka ni nakala ya hukumu.
Kutokana na kushindwa kujitetea Hakimu Ndeuruo alimhukumu kwenda jela miaka 30 na kwamba ana haki ya kukata rufaa katika Mahakama kuu endapo hakuridhika na hukumu hiyo.
Awali katika ushahidi wake Mahakamani hapo Mtuhumiwa huyo alidai kuwa hakutenda kosa hilo bali alitengenezewa na Mkewe ambaye aliapa kumkomesha baada ya kukosana na kumpata mume mwingine jambo ambalo lilipingwa vikali na hakimu na kudai kuwa “ mfa maji haachi kutapatapa”

Na Mbeya yetu

KANISA KATOLIKI PAROKIA YA URU LAKUMBWA NA MAMBO YA KISHIRIKINA


HOFU kubwa imetawala Kanisa Katoliki Parokia ya Uru iliyopo Wilaya ya Moshi Vijijini mkoani Kilimanjaro, kutokana na matukio kadhaa yanayoendelea kutokea katika kanisa hilo huku baadhi ya watu wakiyahusisha na imani za kishirikina. 


  Katekista wa parokia hiyo, Lucian Tesha, aliwaambia waamini waliokusanyika katika ibada ya misa ya kwanza kanisani hapo juzi Jumapili kuwa usalama katika kanisa hilo upo shakani na kuwataka kuwa macho.


Hali hiyo inatokana na kile alichodai kuwa kuna mtu mmoja (mwanaume) kwamba amekuwa akionekana eneo la kanisa akiweka vitu mbalimbali ambavyo havina nia njema na kanisa hilo la Moyo Mtakatifu wa Yesu.
 
“Mtu huyu ameonekana kanisani hapa kwa mara ya nne sasa, hatujui anataka nini, lakini amekuwa akiweka vitu mbalimbali katika sanamu ya Bikira Maria na karibu na sakristi ya mapadri…kwa kweli hali hii inatisha.

 "Ninawaomba tunapotoka kanisani hapa tuende kuangalia katika sanamu hiyo, kwani mtajionea vitu hivyo na wakati mwingine hata kadi za pikipiki,” alisema Tesha na kuacha waamini wakinong’ona.


Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kanisani hapo ni kuwa tangu paroko mpya aingie katika parokia hiyo, aliyefahamika kwa jina moja la Kiondo kumekuwa na matukio ambayo si mazuri.


“Tangu aingie hapa sanamu ya Mtoto Yesu imeibiwa na watu wasiofahamika… hatujakaa vizuri yanajitokeza haya mauzauza ya watu kuweka vitu visivyofahamika kanisani.

“Haifahamiki kama wanampima au la, lakini wengi wanajiuliza ni kwa nini matukio haya hayakuwapo siku zote? Alihoji muumini mmoja.

Siku za hivi karibuni kumekuwa na matukio ya makanisa kushambuliwa na hivyo kuwaweka roho juu waamini na mapadri wanapokuwa wakishiriki ibada takatifu

Monday 29 July 2013

HATUNA UGOMVI NA POLISI........... CHADEMA



     
 
 
 
 Wakati kukionekana kuwapo kwa mvutano mkali kati ya Jeshi la Polisi nchini na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), chama hicho kimesema kuwa hakitakubali kukaa kimya wakati baadhi ya watumishi wa jeshi hilo wakitumiwa vibaya kwa maslahi ya kisiasa kukandamiza raia. Chama hicho kimesema hakina ugomvi na jeshi hilo kwa ujumla wake, isipokuwa askari wachache kiliodai wanatumiwa vibaya kuhujumu haki za binadamu na demokrasia nchini, kikisema hao ndiyo wanalipaka matope jeshi hilo na kuzidi kulikosesha imani kwa wananchi.
   Akihutubia mkutano mkubwa wa hadhara Tabora mjini, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, alisema chama hicho hakitarudi nyuma kutetea haki na matumaini ya Watanzania. Mkutano huo uliofanyika katika Uwanja wa Chipukizi, ukiwa ni sehemu ya kukamilisha kuzindua Kanda ya Magharibi (mikoa ya Kigoma, Tabora na Katavi), ikiwa ni mkakati wa chama hicho wa kujiendesha kwa kanda. “Ndugu zangu watu wa Tabora, wanachama na wapenzi wetu wa Kanda ya Magharibi, katika mapambano haya ya kuing’oa CCM na kuleta mabadiliko makubwa ya mfumo na utawala ndani ya nchi yetu, tumefika mahali utetezi wa haki na matumaini ya wananchi umegeuzwa kuwa ni vurugu au fujo…kila leo mnasikia chama chenu ambacho kimezidi kuwa na ushawishi miongoni mwa Watanzania wengi wenye kiu kubwa ya mabadiliko, kinafanyiwa vituko, kimoja baada ya kingine,” alisema.

    Alisema hivi sasa wafuasi na wapenzi wa chama hicho wanatekwa, wanateswa, kupigwa na hata kuuawa. “Matukio ya namna hii yanazidi na sisi tumesema hatuwezi kuendelea kulalamika na kulialia kwa vyombo husika. Tutajilinda,” alisema. “Tunatambua umuhimu wa vyombo vya ulinzi na usalama. Taifa linawahitaji wawe waadilifu, watimize wajibu na kutenda haki kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi. Chadema tunawatetea hawa ndani na nje ya Bunge, lakini hatutakubaliana na askari wanaotumika vibaya, kwa kupewa amri za hovyo, kama kwenye tukio la bomu Arusha,” alisema Mbowe. Akizungumzia suala la mjadala wa rasimu ya Katiba Mpya, Mbowe alisema mapema mwezi Agosti, mwaka huu, chama hicho kitaanza kuzunguka nchi nzima kwenye operesheni M4C-Katiba Mpya; na kitaendesha mabaraza yake kwa uwazi kwenye mikutano ya hadhara.

WAUZA UNGA WAITEKA AIRPORT YA DAR

WAIFANYA NDIO NJIA YA KUPITIA KILAAINI


 
 
 Nidhahiri kwamba Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), sasa ni kitovu cha kusafirisha dawa za kulevya nje ya nchi. Katika kipindi cha takribani wiki mbili tu, Watanzania wanne wamekamatwa ughaibuni wakiwa na shehena ya dawa hizo ambazo walisafirisha kutoa Tanzania kwenda nje kupitia uwanja huo bila ya kukamatwa. Mara ya kwanza walikuwa ni wasichana wawili, Agnes Jerald (25) na Melisa Edward (24), ambao walikamatwa Afrika Kusini na kushtakiwa nchini humo. Walikamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo wakiwa na shehena ya kilo 150 ya dawa aina ya Crystal Methamphetamine zenye thamani ya zaidi ya Sh. bilioni 6.8. Wasichana hao walikamatwa Julai 5, mwaka huu baada ya kuwasili Johannesburg wakitokea Tanzania wakisafiri kwa ndege ya Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA) na walikamatwa na Maofisa wa Mamlaka ya Mapato ya nchi hiyo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo, uliopo eneo la Kempton Park.
 
    Ijumaa wiki hii, Watanzania wengine wawili, walikamatwa Hong Kong wakiwa na dawa za kulevya aina ya cocaine na heroine zenye thamani ya bilioni 7.6 akiwamo mmoja aliyekamatwa akitokea Dar es Salaam kupitia Dubai hadi Honh Kong. Matukio haya yote yanatokea wakati wakuu wa Uwanja wa ndege wa Julius Nyerere zinakopitishwa wakiwa hawana cha kusema juu ya uharamia huo unaotokea kwenye kitovu cha mawasiliano cha nchi.Jana, Kamanda wa Polisi Kikosi cha Viwanja vya Ndege Nchini, Deusdedit Kato, alisema jalada la upelelezi kuhusu tukio la kukamatwa kwa wasichana Afrika Kusini litapelekwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) leo ingawa hakuwa tayari kutaja watuhumiwa ni nani hasa wanaoshirikiana na wafanyabiashara ya dawa hizo.

     Kato alisema hawezi kutaja majina ya watu waliobainika kwa sababu kilichofanyika ni uchunguzi  tu na kwamba DDP ndiye mwenye mamlaka  ya kuamua juu ya uchunguzi huo. “Siwezi kukuambia ni nini kimepatikana katika uchunguzi wala kutaja majina ya watu, kwa kuwa mimi ninapeleka nilichokichunguza kwa sababu naweza kukuambia lakini ikawa sio hivyo kwani huu ni uchunguzi tu,” alisema. Aliongeza: “Naweza kupeleka jalada langu la uchunguzi kwa DDP lakini kutokana na utalaam wake akagundua kuna mapungufu, hapo tayari nitakuwa nimepotosha umma. Lakini pia akiona upelelezi unajitosheleza yeye ndiye anaweza kuamua kupeleka Mahakamani.” Kuhusu taarifa za kukamatwa kwa Watanzania wengine na dawa za kulevya Julai 26,  mwaka huu  huko huko mjini Hong Kong, Kato alisema bado wanafanya jitahada za kupata kwa undani  taarifa hizo.

     “Na mimi nimesikia, lakini hatujapata taarifa zaidi ili kujua majina yao na kama kweli ni Watanzania. Inakuwa ngumu kupata taarifa kwa sababu aina  ya mawasiliano wanayotumia hawa Polisi wa Kimataifa (Interpol ) ni tofauti na ya kwetu kwa hiyo tunategemea wao ndiyo watupe taarifa,” alisema Kato. Naye Waziri wa Uchunguzi, Dk. Harrison Mwanyembe, ambaye amejipatia sifa za utendaji katika siku za hivi karibuni, kwa kuendesha timua timua katika taasisi zinazosimamiwa na wizara yake kwa tuhuma za uzembe, amekuwa kimya na pengine kukwepa kabisa kutia mguu katika sakata la dawa za kulevya JNIA. Wiki iliyopita NIPASHE lilimtafuta Dk. Mwakyembe mwenye dhamana ya Viwanja vya Ndege nchini kujua ni hatua gani amechukua, lakini alijibu kwamba hana taarifa za kina kuhusu sakata hilo.

        Uharamia huo wa dawa za kulevya umempa pia kigugumizi Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Kamishna Robert Manumba, ambaye amekwepa kuzungumzia sakata hilo na kusema liko kwa Kamanda wa Polisi, Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Geofrey Nzowa. Kamanda Nzowa alipoulizwa alisema upelelezi bado unaendaelea kubaini mambo mbalimbali yaliyoko nyuma ya tukio hilo.  Alipoulizwa ikiwa Polisi wamebaini mmiliki pamoja na maofisa walioruhusu kupitishwa kwa dawa, Nzowa alisema uchunguzi unaangalia mambo mengi na ndiyo huo utakuja na taarifa kamili. Taarifa kutoka Hong Kong za Ijumaa wiki iliyopita zinaeleza kwamba, maofisa ushuru wa Uwanja wa Ndege wa Hong Kong (HKIA), walimkamata kijana mmoja mwenye umri wa miaka 26 akitokea Tanzania na alikuwa na dawa za kulevya aina ya heroin kilo 1.6 zenye thamani ya Sh. bilioni 1.5, kwenye mzigo wake wa mkononi.

       Taarifa zilieleza kwamba baadaye jioni siku hiyo hiyo, maofisa hao walimkamata Mtanzania mwingine mwenye miaka 45 ambaye alipelekwa hospitali na kutolewa gramu 240 za dawa za kulevya aina ya heroin. Taarifa zaidi zilieleza kuwa Mtanzania mwingine mwenye miaka 28 alikamatwa akiwa na kilo 2.03 za cocaine. Takwimu zinaonyesha kumekuwa na wimbi kubwa la Watanzania wanaojiingiza katika biashara haramu ya dawa za kulevya ndani na nje ya nchi na kwamba, katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, watuhumiwa 10,799 walikamatwa kwa kujihusisha na uharamia huo. Katika kipindi hicho, Watanzania 240 walikamatwa katika nchi za Brazil, Pakistan na Afrika Kusini, na kuharibu taswira ya nchi na kusababisha Watanzania wasio na hatia kupata usumbufu na masharti magumu wanapotaka kusafiri kwenda nchi mbalimbali duniani.

"NIKIKUTA NINA VIRUSI VYA UKIMWI NI LAZIMA NIJIUE MAANA SIPO TAYARI KUCHEKWA".....BABY MADAHA




Msanii  wa  filamu  bongo,Baby Madaha  amefunguka  kwamba  siku  akianza  kuona  dalili  za  ugonjwa  wa  UKIMWI  ndani  ya  mwili  wake   atakunywa  sumu  kwa  kuhofia  kuchekwa  na  jamii.

Akiongea  na  mwandishi  wetu,Madaha  amedai  kuwa  kwa  sasa  anaamini  hana  ngoma  maana  siku  zote  hutumia  Kinga (kondom)   ili  asiambikizwe  gonjwa  hilo  japo  hana  uhakika  asilimia  zote  maana  hiyo  ni  mipango  ya  mungu.

"Siukatai  ugonjwa  huo  kwa  kuwa  sijui  ni  lini  naweza  kuupata  hasa  ukizingatia  kwamba  mimi  bado  ni  kijana  mbichi  ambaye  bado  nahitaji  kuifurahia  dunia"...Alisema  Baby Madaha..

Katika  mazungumzo  hayo, Madaha  anadai  kwamba  mpaka  sasa  hakuna  mpenzi  wake  yeyote  aliyekufa  kwa  Ngoma  ingawa  wapo  waliofariki  kwa  maradhi  ya  kawaida  na  ajali....

"Nikijua  tu  nina  ngoma  ni  lazima  ninywe  sumu  ili  kukwepa  balaa  la  wabongo.Najitahidi  kujilinda  ili  nisiudake  mapema"..Alisema Madaha  

Madaha  anadai  kwamba  kitendo  cha  yeye  kujiua  mapema  kitasaidia  kuwaondolea  wasiwasi  wasanii  wenzake  ambao  wataanza  kujiuliza  maswali  mengi  kuhusu  watu  aliowahi  kutoka  nao  kimapenzi

"Nitawasaidia  wasanii  wengine  ambao  nimewahi  changia  nao  mabwana.Najua  wataumia  sana, lakini  ndo  hivyo  tena, hakutakuwa  na  jinsi.

"Sijasema  nina  UKIMWI,Hapana,nimesema  kwamba  ikitokea  maana  watu  hawakawii  kupindisha  maneno"..Madaha

TAIFA STARS WALIVYOONDOKA KWA MAJONZI JIJINI KAMPALA


NI BAADA YA KUBORONGA TENA KWENYE MICHUANO YA CHAN.



Michuano ya soka watanzania ilishatushinda toka enzi za ........ ni bora kuanza na moja ama sivyo tuongeze nguvu kwenye michezo mingine tunayoona wachezaji wake wanatunyanyua watanzania ili tutokee huko.

MCHUNGAJI MBALONI KWA KUMLAWITI MTOTO DAR

 

Mchungaji wa kanisa moja la kilokole lililopo Kichangani majohe ,Dar es salaam aliyeitwa kwa jina moja la Benard anadaiwa kutiwa mbaroni kwa tuhuma za ulawiti wa mtoto wa kiume (jina tunalo)mwenye umri wa miaka 15. Kwa mujibu wa mdogo wa mchungaji huyo aliyejitambulisha kwa jina la Hamis, kaka yake huyo alikamatwa wiki iliyopita baada ya watu waliojitambulisha kuwa ni askari kufika nyumbani na kumuweka chini ya ulinzi.


Alisema kuwa katika kuishi na kaka yake huyo, aliwahi kumuona huyo mtoto anayedaiwa kulawitiwa mara moja tu kwani yeye bado ni mgeni.

 
Kwa mujibu wa mtoto aliyedaiwa kuingiliwa, alikutana na mchungaji huyo mwaka jana maeneo ya Stendi ya Banana-Ukonga, Dar ambapo alimuomba na kumwambia kuwa alikuwa anatafuta mtoto wa kumfanyia biashara ya mayai huko Majohe nyumbani kwake.

Alisema kuwa alikataa na kumwambia hawezi kwenda naye bali aende akazungumze na wazazi wake nyumbani.

 
Alisimulia kuwa baada ya hapo, aliongozana na baba mchungaji hadi kwa wazazi wake ambapo walikubaliana kuwa kila mwezi atamlipa mshahara wa shilingi 30,000.

 
Baada ya makubaliano hayo mtoto huyo alisema kuwa aliondoka na mchungaji na baada ya kukaa kwa muda mfupi huku akiendelea na biashara ya mayai, mchunga kondoo huyo wa Mungu alianza tabia ya kumfanyia unyama huo huku akimdanganya kuwa atampa simu.

 
“Kuna wakati kweli ananipa simu kwa muda na kuninyang’anya.
“Kwa siku moja alikuwa ananiingilia mara mbili, asubuhi na jioni,” alisema mtoto huyo kwa uchungu.

 
Alisema kuwa baba mchungaji aliendelea kumfanyia ‘usodoma’ kwa muda mrefu.

 
Alisema baada ya kufika nyumbani kwa wazazi wake, mama yake alimgundua na kumtaka kueleza ukweli.

 
“Nilimweleza baba na mama jinsi mchungaji anavyonifanyia ukatili, walimwita nyumbani wakiwa tayari wameshaandaa polisi jamii, alipofika aliwekwa chini ya ulinzi lakini aliwaomba msamaha polisi jamii hao pamoja na wazazi huku akiahidi kutorudia tena.

 
“Kila mtu alikubaliana na msamaha na kumpa masharti kwamba afilisiwe vitu vyake vyote kama faini ya kosa.

 
“Alikubali, akafilisiwa vitu vyote  vikakabidhiwa kwa wazazi wangu ambapo baba yangu alikuwa mgonjwa hivyo kutokana na kukosa uwezo aliviuza vitu hivyo kwa ajili ya matibabu na mwishowe akafariki dunia,” alisema.

 
Mtoto huyo aliendelea kusimulia kuwa baada ya kuachana na mchungaji huyo kwa muda mrefu, kuna msichana mmoja mtaani kwao anayejulikana kwa jina la Asha ambaye alimfuata na kumbembeleza kuwa waende tena kwa mchungaji huyo, naye akakubali na baada ya kufika huko huku wakiwa wameambatana na mtoto mwingine wa kiume (17), mchungaji huyo alimfanyia tena mchezo huo na kumpa fedha huyo msichana hivyo akawa kama yeye ndiye aliyeenda kuwauza.

 
“Juzi hapa mtaani kwetu aliuawa mwizi mmoja, baada ya kuona kile kifo nilimuita mama yangu na kumwambia natubu maovu yangu ndipo nikaanza kumwelezea jinsi nilivyorudi tena kwa mchungaji kwa kushawishiwa na huyo Asha,” alisema mtoto huyo.

 
Huku mchungaji huyo akiwa na tuhuma hiyo ya kufanya mchezo huo na mmoja chumbani na mwingine sebuleni, mwanaume ambaye ni rafiki wa mchungaji huyo aliyetajwa kwa jina moja la Rahim naye akaingia kwenye mkumbo na kuendeleza dhambi ya kuwasulubu vijana hao. 

 
Mchungaji huyo, rafiki yake na Asha, wote waliswekwa nyuma ya nondo za mahabusu katika Kituo cha Polisi cha Stakishari, Dar na kufunguliwa shitaka namba STK/RB/13160/2013-ULAWITI wakisubiri kesi yao kuanza kuunguruma.

 
Wanahabari wetu walifanikiwa kuzungumza na askofu wa mchungaji huyo, Grace Joseph ambaye alikuwa na haya ya kusema: 

 
“Kwa jinsi ninavyomjua mchungaji wangu siamini kama amefanya kitendo hicho hivyo tuhuma hizo sikubaliani nazo kabisa ila polisi wanaendelea na uchunguzi.”

KAHABA APIGWA NA WENZIE KISA KIKIWA NI KUJIUZA KWA BEI RAHISI

kahaba mmoja katika mji wa Naivasha, jimboni Rift Valley, Kenya alinusurika kufa baada ya kupewa kichapo cha mwizi na makahaba wenzake kwa sababu wamekerwa na kitendo chake cha kuuza ngono kwa bei rahisi na kuwaharibia soko.


Wenzake hao wenye hasira walimtwanga kwa mangumi na mateke, wakimshutumu kwa kutokuwa na ushirikiano na “kuharibu soko” hasa ukizingatia ilikua ni kipindi cha mwisho wa mwezi, ambapo wateja wamejaa mkwanja na mahitaji ya kununua ngono yameongezeka.
Wakati wakimpa kichapo, walitaka kumkeketa (kumtahiri mwanamke) kwa kutumia chupa iliyovunjika “ili iwe funzo” lakini akaokolewa na walinzi wa usiku (wengi wao ni wateja wake) kabla hajafanyiwa kitendo hicho.
Msuguano ulianza mwezi uliopita pale msichana huyo mwenye umbo nyororo na la kuvutia alihamia mitaa hiyo kitu ambacho kiliwakera makahaba wazoefu hapo maana walimuona kama tishio kutokana na urembo wake.
Kwa mujibu wa dereva wa bodaboda anayeitwa Peter, kahaba huyo amekua ni kivutio na anayependwa na wengi kutokana na uzuri wa umbo lake na rangi nyeupe ya ngozi yake. Zaidi ya “kupunguza bei,” inadaiwa kuwa kahaba huyo pia anatoa “huduma” kwa mkopo, kitu ambacho wenzie hawafanyi, hivyo kuzidi kuwaaribia biashara zaidi.
“Kwa kawaida, bei ni kati ya Ksh 100 mpaka Ksh 500 (kama TZ Shs 2,000 mpaka 10,000) inategemeana na mteja. Lakini “Brownie” anauza kwa hata Kshs 50 (TShs 1,000)” alidai Peter.
Idadi ya wateja wake ilikua kwa wingi na kwa kasi, kitu kilichopelekea wivu na chuki kutoka kwa makahaba wengine, ndipo walipofikia uamuzi wa kufanya njama za kupanga kumpa kichapo “ili iwe fundisho.”
Makahaba hao walitekeleza lengo hilo pale walipomzingira kwenye kona, gizani akiwa peke yake, na kumshambulia kikatili.
“Kwani unafikiria sisi tutakula wapi kama utaendelea kujiuza hii bei hasara.” Mmoja wa wanawake hao alimkaripia kwa sauti ya juu.
Kahaba huyo alipiga mayowe na kuomba msamaha kutoka kwa wanawake hao wenye hasira wakati anashambuliwa, ndipo walinzi waliposikia na kukimbilia kumuokoa.
Walinzi hao walipofika, walikaripiwa na makahaba hao wakiambiwa kuwa hiyo ni ishu ya wanawake, na wao haiwahusu.
““Unajua huyu mama huwa ananipatia kwa mkopo siku ninazokuwa nimechacha hivyo siwezi muacha auliwe na hawa mikora” alisema mmoja wa walinzi hao wakati wakijaribu kumuokoa mwanamke huyo.
“Wateja” wake wengine wakaingilia kumuokoa kahaba huyo ambaye alikua ameumizwa vibaya, na kumkimbiza hospitali.
Inaonekana makahaba wazoefu maeneo hayo wanatawala “ngome” yao na lazima wakatiwe panga na makahaba wapya, ambao lazima wajitambulishe kabla ya kujiunga kwenye “soko” lao.
“Brownie” bado yuko hospitali akipatiwa matibabu huku wateja wake wakimsubiri apone, ili waendelee kupata “huduma” zake kwa bei nafuu, na kwa mkopo.
“Maisha imekuwa ngumu sana na bei ya kila kitu, hata ya hawa wasichana imepanda sana. Tunaomba serikali iingilie kati ,” mmoja wa walinzi hao alilalamika.

DIAMOND ANUNUA MTAA


WAKATI Wema Isaac Sepetu akiongeza idadi ya magari kwa kununua mkoko wa maana, zilipendwa wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amemziba mdomo baada ya kununua eneo kubwa ambalo ndani yake kuna nyumba tatu, jirani na anapoishi Miss Tanzania huyo wa mwaka 2006, Ijumaa Wikienda lina maelezo kamili.
Tukio hilo lilijiri hivi karibuni Mtaa wa Kaprikoni-Kijitonyama jijini Dar na kusababisha watu kupigwa na butwaa na kudai kuwa kweli ‘dogo’ ana jeuri ya fedha kwa kitendo hicho cha kununua karibia mtaa wote huo.
Akizungumza na gazeti, hili muda mfupi  baada ya kukamilisha kila kitu kuhusiana na ununuzi wa eneo hilo ambalo kwa mujibu wake anatarajia kujenga jengo lenye ghorofa nne na nyumba za kawaida tatu, Diamond alisema kuwa anajitahidi kuongeza idadi ya mijengo anayomiliki kwa kuwa ndicho kitu cha thamani kuliko magari.
“Najua (nyumba) zitanisaidia endapo muziki wangu utakosa soko. Mimi na mama yangu (Sanura Kassim ‘Sandra’) tuliishi kwa dhiki sana na sasa kwa kipindi hiki ambacho Mungu ananisaidia na kuniwezesha kupata fedha kwa wingi, siwezi kuishi maisha ya anasa ya kununua magari ya kifahari,” alisema.
Katika hali iliyotafsiriwa kuwa ni kumtunishia msuli Wema, jamaa alitupia maneno: “Mimi siyo kama hao wanaokimbilia kununua magari ya kifahari ili mradi waonekane wako juu kifedha.
Eneo alilonunua Diamond anayemiliki nyumba zaidi ya tano Dar lipo mtaa wa nne kutoka anapoishi Wema.

MSHIRIKI WA TANZANIA (NANDO ) ATIMULIWA BIG BROTHER BAADA YA KUGOMBANA NA MSHIRIKI MWENZAKE

Jana usiku mara tu baada ya Sulu na Annabel kutolewa kwa kura za watazamaji, Big Brother aliwaita washiriki pamoja katika kikao cha dharura kufuatia ugomvi uliotokea kati ya Nando na Elikem.

Itakumbukwa kwamba siku ya ijumaa ilitokea hali ya kutoelewana kati ya Nando na Elikem. Wawili hawa walitukanana sana na kutishiana mno. Ugomvi huo ulianzishwa na Nando.

Kwa mujibu wa sheria za Big Brother mwaka huu, kuanzisha ugomvi ni kosa ambalo hupelekea kupata 'strike' ama onyo.

3 strike rule ni mtindo unaotumika msimu huu. Kwa mujibu wa Big brother, yeyote atakaye fanya makosa matatu makubwa na kupewa maonyo matatu basi moja kwa moja anatakiwa atimuliwe..

Sheria hiyo imetumika kumtimua Nando kwa sababu 1. Alianzisha ugomvi siku ya Ijumaa, 2. Alishiriki ugomvi na Elikem na 3. Alitishia maisha, "I feel like stabbing him. A nigga like that deserves to die"...

Katika kipindi cha wiki 9 za ushiriki wake katika jumba hilo, Nando amekutwa na misuko suko kadhaa ikiwemo kuwahi kukutwa na kisu katika Party ya Channel O pia kukutwa na mkasi chini ya kitanda kitu ambacho ni kinyume cha sheria za big brother.

Kutokana na ugomvi huo Elikem alipata strike moja.

Big brother alimtaka Nando aondoke katika jumba lake hilo na kutumia fursa hiyo kuwataka washiriki wengine waishi kama watu wazima.