Mchungaji
wa kanisa moja la kilokole lililopo Kichangani majohe ,Dar es salaam
aliyeitwa kwa jina moja la Benard anadaiwa kutiwa mbaroni kwa tuhuma za
ulawiti wa mtoto wa kiume (jina tunalo)mwenye umri wa miaka 15.
Kwa mujibu wa mdogo
wa mchungaji huyo aliyejitambulisha kwa jina la Hamis, kaka yake huyo
alikamatwa wiki iliyopita baada ya watu waliojitambulisha kuwa ni askari kufika
nyumbani na kumuweka chini ya ulinzi.
Alisema kuwa katika
kuishi na kaka yake huyo, aliwahi kumuona huyo mtoto anayedaiwa kulawitiwa mara
moja tu kwani yeye bado ni mgeni.
Kwa mujibu wa mtoto
aliyedaiwa kuingiliwa, alikutana na mchungaji huyo mwaka jana maeneo ya Stendi
ya Banana-Ukonga, Dar ambapo alimuomba na kumwambia kuwa alikuwa anatafuta
mtoto wa kumfanyia biashara ya mayai huko Majohe nyumbani kwake.
Alisema kuwa alikataa na
kumwambia hawezi kwenda naye bali aende akazungumze na wazazi wake nyumbani.
Alisimulia kuwa baada ya hapo, aliongozana na baba
mchungaji hadi kwa wazazi wake ambapo walikubaliana kuwa kila mwezi atamlipa
mshahara wa shilingi 30,000.
Baada ya makubaliano hayo mtoto huyo alisema kuwa aliondoka na mchungaji na baada ya kukaa kwa muda mfupi
huku akiendelea na biashara ya mayai, mchunga kondoo huyo wa Mungu alianza
tabia ya kumfanyia unyama huo huku akimdanganya kuwa atampa simu.
“Kuna wakati kweli
ananipa simu kwa muda na kuninyang’anya.
“Kwa siku moja alikuwa ananiingilia mara mbili,
asubuhi na jioni,” alisema mtoto huyo kwa uchungu.
Alisema kuwa baba
mchungaji aliendelea kumfanyia ‘usodoma’ kwa muda mrefu.
Alisema baada ya kufika
nyumbani kwa wazazi wake, mama yake alimgundua na kumtaka kueleza ukweli.
“Nilimweleza baba na mama
jinsi mchungaji anavyonifanyia ukatili, walimwita nyumbani wakiwa tayari
wameshaandaa polisi jamii, alipofika aliwekwa chini ya ulinzi lakini aliwaomba
msamaha polisi jamii hao pamoja na wazazi huku akiahidi kutorudia tena.
“Kila mtu alikubaliana na
msamaha na kumpa masharti kwamba afilisiwe vitu vyake vyote kama faini ya kosa.
“Alikubali, akafilisiwa
vitu vyote vikakabidhiwa kwa wazazi wangu ambapo baba yangu alikuwa
mgonjwa hivyo kutokana na kukosa uwezo aliviuza vitu hivyo kwa ajili ya
matibabu na mwishowe akafariki dunia,” alisema.
Mtoto huyo aliendelea
kusimulia kuwa baada ya kuachana na mchungaji huyo kwa muda mrefu, kuna
msichana mmoja mtaani kwao anayejulikana kwa jina la Asha ambaye alimfuata na
kumbembeleza kuwa waende tena kwa mchungaji huyo, naye akakubali na baada ya
kufika huko huku wakiwa wameambatana na mtoto mwingine wa kiume (17), mchungaji
huyo alimfanyia tena mchezo huo na kumpa fedha huyo msichana hivyo akawa kama
yeye ndiye aliyeenda kuwauza.
“Juzi hapa mtaani kwetu
aliuawa mwizi mmoja, baada ya kuona kile kifo nilimuita mama yangu na kumwambia
natubu maovu yangu ndipo nikaanza kumwelezea jinsi nilivyorudi tena kwa
mchungaji kwa kushawishiwa na huyo Asha,” alisema mtoto huyo.
Huku mchungaji huyo akiwa
na tuhuma hiyo ya kufanya mchezo huo na mmoja chumbani na mwingine sebuleni,
mwanaume ambaye ni rafiki wa mchungaji huyo aliyetajwa kwa jina moja la Rahim
naye akaingia kwenye mkumbo na kuendeleza dhambi ya kuwasulubu vijana hao.
Mchungaji huyo, rafiki
yake na Asha, wote waliswekwa nyuma ya nondo za mahabusu katika Kituo cha
Polisi cha Stakishari, Dar na kufunguliwa shitaka namba
STK/RB/13160/2013-ULAWITI wakisubiri kesi yao kuanza kuunguruma.
Wanahabari wetu
walifanikiwa kuzungumza na askofu wa mchungaji huyo, Grace Joseph ambaye
alikuwa na haya ya kusema:
“Kwa jinsi ninavyomjua
mchungaji wangu siamini kama amefanya kitendo hicho hivyo tuhuma hizo
sikubaliani nazo kabisa ila polisi wanaendelea na uchunguzi.”
No comments:
Post a Comment