Pages

Translate

Tuesday, 30 July 2013

AOZWA KWA NGUVU NA KUBAKWA NA KUNDI LA WANAUME SIKU YA HARUSI...



Mwanamke wa India mwenye miaka 24 amelazimishwa kuolewa na kubakwa na kundi la wanaume kama adhabu ya 'heshima' baada ya kaka yake kutoroka na rafiki yake wa kike, imebainika jana.
Mwanamke huyo - ambaye hakuweza kutajwa kwa usalama wake - aliambiwa anatakiwa kuolewa na mume ambaye ni kaka wa mke wa mchumba mpya wa kaka yake kama 'kisasi' kwa uzinzi wa wawili hao.
Na ndani ya masaa kadhaa za kufunga pingu za maisha na mumewe mpya, akashambuliwa na kubakwa 'bila huruma' na kaka kadhaa wa mchumba wa kaka yake.
Kwa namna ya kushangaza, shambulio hilo ya kutisha lilidaiwa hata kupewa kibali na wazee wa kijiji hicho kilichopo makazi ya vijijini ya Uttar Pradesh, kaskazini mwa India, ambao walidai: "Jicho kwa jicho ni hukumu halisi."
"Ninakubaliana na uamuzi wao sababu ninajua kwamba kungekuwa na umwagaji damu katika kijiji hiki kama ningekataa kuolewa naye," mwanamke huyo aliwaeleza polisi.
"Mashemeji zangu walinibaka bila huruma siku hiyo hiyo niliyofunga ndoa. Ikawa utaratibu wa kawaida.
"Baba mkwe wangu alidai kwamba amekubaliana na ndoa yangu kwa vile alitaka kulipa kisasi (kwa familia yangu) namna hii."
Ajali hiyo mbaya imekuja kujulikana tu pale muathirika alipopata ujasiri wa kufungua madai hayo polisi.
"Machi 26, walifungua kesi dhidi ya kaka yangu na polisi walimkamata yeye na (mke wa mume wangu). Waliachiwa baada ya binti huyo kukiri mbele ya hakimu kwamba aliolewa naye kwa hiari yake," muathirika huyo alidai kwenye madai yake.
Baraza la kijiji au Panchayat, lilidaiwa kumlazimisha mwanamke huyo kuolewa baada ya kaka yake kuwa ametoroka na dada wa mumewe mtarajiwa mnamo Februari 15, mwaka huu.
Panchayat, ambalo liliketi ndai ya siku kumi baada ya kutokomea huko, lilitaka ndoa ya lazima. Mbali na hili, pia liliwataka wazazi wa mwanamke huyo kulipa Rupia 75,000 kama fidia kwa wakwe zake wapya.
Panchayat baadaye lilifafanua hali hiyo iliyojitokeza, likisema 'jicho kwa jicho ni hukumu halisi'.
Watuhumiwa hao wa ubakaji - wanafamilia wanaoshitakiwa -waliripotiwa kuweka bayana kwamba ilikuwa ni ulipizaji wao kisasi kwa kitendo cha utoroshwaji.
Mwanamke huyo kwa namna fulani alifanikiwa kukwepa majaribio yao ya kumkamata Julai 21, mapema asubuhi, na kufungua madai kwa polisi wa Muzaffarnagar mnamo Julai 27.
Mkuu wa polisi, Manzil Saini alisema: "Muathirika huyo amekutana nami. Kesi imefunguliwa chini ya Kifungu 376 ya IPC. Watuhumiwa watakamatwa hivi karibuni."
Kaka mkubwa wa muathirika huyo alidai uamuzi huo uliopelekea tukio hilo ulichukuliwa chini ya usimamizi madhubuti wa Panchayat.
"Polisi walitoa muda kwa watuhumiwa kuondoka kijijini hapo. Mume huyo wa chifu wa panchayat alikuwapo wakati tukio hilo la dada yangu likiamuliwa. Alikuwa msemaji mkubwa na kutaka adhabu kali mno dhidi yetu," alisema.
Mkuu wa panchayat alithibitisha uamuzi wake jana. Alidai aliwataka wafikie suluhisho la amani.
Tukio hilo limekuja wiki mbili baada ya mwanachuo mwenye miaka 20 kubakwa na kundi la wanaume na kisha kuchomwa moto huko Etawah, jimboni Uttar Pradesh, mkoa alikotokea Waziri Mkuu Akhilesh Yadav.
Katika kesi hiyo, kwa namna ya kushitusha, polisi hao si tu kwamba mwanzoni walikataa kufungua kesi lakini pia walionekana kukiuka wajibu wao wa kusimamia sheria na utii.

No comments:

Post a Comment