Pages

Translate

Thursday 20 June 2013

WACHINA WAKANYAGANA KWA AJILI YA DAVID BECKHAM


Beckham stampede
Vurugu tupu: Ofisa wa usalama na watu wengine wakijaribu kumbeba askari wa kike aliyepata majeruhi katika mapokezi hayo yaliyojaza umati  mkubwa sana
David BeckhamKabla ya fujo: Maelfu ya watu wamejitokeza kumpokea nyota Beckham katika chuo kikuu cha Shanghai
PolicewomanMaskini askari: Askari wa kiume akiwa amelala chini ya sakafu baada ya kujeruhiwa katika mapokezi hayo
Beckham crushFujo zaanza:  Maofisa wa polisi wameshindwa kuwazuia maelfu ya watu katika mapokezi hayo.
 
Nyota wa zamani wa Manchester United,  Los Angel Galaxy, Real Madrid, PSG na timu ya taifa ya England, David Beckham amewasili leo nchini China na kusababisha wanafunzi watano kujeruhiwa vibaya katika harakati za kumpokea  katika chuo cha Tongji University ambapo umati mkubwa ulifurika kupita kawaida.
 
Beckham ameenda kuwatembelea wanachama wa klabu ya mpira wa miguu ya chuo hicho kama sehemu ya ziara yake ya siku saba nchini humo yenye lengo la kuiamusha ligi kuu ya China.
Licha ya watu wengi waliofurika kuhitaji kushikana mikono na nyota huyo, imekuwa ngumu sana kulingana na watu kusukumana na kusababisha watu kujeruhiwa wakiwemo maaskari polisi.
Lengo la Beckham kuzungumza na wanachama hao limeshindwa kutimia kufuaia fujo hizo za watu wengi waliofurika, lakini ameandika katika mtandao wake wa kijamii wa Facebook akiwaomba radhi mashabiki wake kwa kile kilichotokea.
Samahani sana jamani, nimeshindwa kuiona timu ya chuo kikuu pale uwanjani, kiukweli ilikuwa ngumu sana kupenya umati ule. Nimesikia watu wachache wamejeruhiwa, natumaini wanaendelea vizuri na nawatakiwa kheri wapone salama”. Alisema Beckham baada ya kuondoka uwanjani hapo.
Takribani watu elfu moja walikuwepo katika mapokezi hayo na kuhitaji kumshika nyota huyo,na tayari jeshi la polisi limethibitisha kuwa maofisa wake watatu wamejeruhiwa katika fujo hizo
Beckham mwenye umri wa miaka 38 amestaafu kucheza soka msimu uliopita ambapo aliwasaidia PSG kutwaa ubingwa wa ligi kuu nchini Ufaransa, Ligue 1.

No comments:

Post a Comment