MSANII wa filamu nchini Jacqueline Wolper ameenda kujichimbia Afrika Kusini akifanya mazoezi ili ajiweke katika nafasi ya kuzichapa na mbunge wa CHADEMA Halima Mdee, katika tamasha la Matumaini litakalofanyika Julai 7 mwaka huu.
Wolper ambaye atapigana na Halima Mdee, alisema kuwa amejikita nchini humo kwa ajili ya kujiweka sawa ili aweze kumkabiri mbunge huyo.
Alisema mbali ya kujiweka fiti kwa ajili ya kumkabili mbunge huyo pia anajiweka fiti kwa ajili ya kujenga mwili wake ili kupunguza magonjwa pamoja na kujinginga na magonjwa ya kisukali yanayotokana na mafuta.
"Naamini nitamgaragaza mbunge huyo na sitochukua hata dakika tano kwenye mchezo huo kwani naamini mazoezi yangu ninayoyafanya ni njia moja wapo ya kujiweka vizuri kimwili" alisema Wolper.
Siku ya Usiku wa Matumaini utapambwa na mashindano kibao yakiwemo mbunge wa viti maalumu Ester Bulaya ambaye naye anatarajia kuzichapa na Aunt Ezekiel, huku Zitto Kabwe atazichapa na Vincent Kigosi
No comments:
Post a Comment